Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w00 9/15 uku. 32
  • Upendo wa Kikristo Ni Zaidi ya Maneno Tu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Upendo wa Kikristo Ni Zaidi ya Maneno Tu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
w00 9/15 uku. 32

Upendo wa Kikristo Ni Zaidi ya Maneno Tu

MOTO ulipoteketeza makao ya familia ya Bartholomew huko Trinidad, walipoteza vitu vyao vyote isipokuwa uhai wao. Mtu fulani wa ukoo mwenye kuishi karibu aliwakaribisha kwake, lakini hilo halikuwa mwisho wa tukio hilo.

Olive Bartholomew ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova, nao washiriki wa kutaniko lake—kutia ndani makutaniko ya eneo la karibu—walianza kutoa michango ya kutumiwa kujenga upya nyumba ambayo yeye na washiriki wengine wa familia yake walikuwa wamepoteza. Halmashauri iliundwa ili kuendesha mradi huo, na ujenzi ukaanza. Mashahidi wapatao 20, pamoja na majirani kadhaa walikuwepo kwenye ujenzi huo. Hata vijana walijiunga na kazi, watu wengine nao wakaleta viburudisho.

“Washiriki wa familia yangu wamevutiwa sana,” akasema Olive, kama ilivyoripotiwa na gazeti Sunday Guardian la Trinidad. “Wao si Mashahidi, na mume wangu bado ameduwaa kutokana na yale anayoyaona.”

Akitoa muhtasari wa jitihada hiyo, mratibu wa mradi huo wa ujenzi alikazia kuwa matendo ya aina hiyo kwa kweli ni alama za kutambulisha Ukristo wa kweli. “Sisi hatuendi tu nyumba hadi nyumba tukisema juu ya upendo,” yeye akasema. “Bali tunajaribu kutenda yale tunayohubiri.”—Yohana 13:34, 35.

[Picha katika ukurasa wa 32]

Olive Bartholomew akiwa pamoja na mume wake

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki