Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w00 11/15 uku. 32
  • Uzuri wa Ndani Una Thamani ya Kudumu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uzuri wa Ndani Una Thamani ya Kudumu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
w00 11/15 uku. 32

Uzuri wa Ndani Una Thamani ya Kudumu

“KIJANA MMOJA MWANAMUME ANALINGANISHA UZURI NA WEMA WA ADILI,” AKASEMA MKRISTO MMOJA MWAMINIFU ALIYE MZEE-MZEE.

Naam, kwa muda mrefu mwanadamu amekazia isivyofaa uzuri wa nje na hivyo mara nyingi kupuuza maadili ya ndani. Hata hivyo, Muumba wetu hutazama jinsi tulivyo ndani bila kujali sura yetu ya nje. Kwa njia hiyo anaweka kielelezo bora kabisa cha uamuzi wenye ukomavu. Kulingana na Biblia, Mungu mwenyewe alisema hivi: “BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.”—1 Samweli 16:7.

Mungu ndiye Chanzo cha uzuri wa kweli wa wanadamu, na Neno lake lafunua kwamba anapokadiria wema wa kweli wa mtu, sifa za kiroho ndizo huwa zenye thamani zaidi. Biblia husema: “Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.” (Mithali 31:30) Kwa kweli, sura yetu yenye kuvutia yaweza kuficha sifa za ndani zisizopendeza. (Esta 1:10-12; Mithali 11:22) Ingawa uzuri wa kimwili waweza kuisha baada ya muda, uzuri wa ndani—sifa za moyoni—waweza kusitawi na kudumu.

Kwa hiyo ni jambo la busara kama nini kusitawisha sifa kama vile upendo, shangwe, amani, ustahimilivu, fadhili, wema, imani, upole, na kujidhibiti! (Wagalatia 5:22, 23) Hivyo twaweza kupata uzuri wa ndani, ambao kwa kweli una thamani ya kudumu.—1 Petro 3:3, 4.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki