Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w01 12/15 uku. 28
  • Wazazi Timizeni Mahitaji ya Watoto Wenu!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wazazi Timizeni Mahitaji ya Watoto Wenu!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
w01 12/15 uku. 28

Wazazi Timizeni Mahitaji ya Watoto Wenu!

WATOTO wanahitaji mwongozo na nidhamu yenye upendo, hasa kutoka kwa wazazi wao. Kuhusiana na habari hiyo, mwalimu mmoja wa Brazili, Tania Zagury, asema: “Kila mtoto huwa na mwelekeo wa kujifurahisha. Ni muhimu kuwawekea mipaka. Wazazi ndio wanaopaswa kufanya hivyo. Wazazi wasipoweka mipaka, watoto huwa watukutu.”

Katika nchi nyingi, ni vigumu kufuata shauri lililo juu kwa sababu ya uvutano wa jamii yenye uendekevu ambayo huthamini sana uhuru wa kibinafsi. Basi, wazazi wanaweza kupata wapi msaada? Wazazi wanaomwogopa Mungu wanatambua kwamba watoto wao ni “urithi wa BWANA.” (Zaburi 127:3) Kwa hiyo, wao hutegemea Neno la Mungu, Biblia, ili iwaongoze kulea watoto wao. Kwa mfano, andiko la Mithali 13:24 husema: “Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; bali yeye ampendaye humrudi mapema.”

Biblia inapotumia neno “fimbo” haimaanishi kuadhibu kimwili tu; fimbo yarejezea njia yoyote ile inayotumiwa kusahihisha. Kwa kweli, huenda mara nyingi maneno tu yakatosha kusahihisha mwenendo uliopotoka wa mtoto. Andiko la Mithali 29:17 husema: “Mrudi mwanao naye atakustarehesha; naam, atakufurahisha nafsi yako.”

Watoto wanahitaji nidhamu yenye upendo ili kuondoa tabia zisizofaa. Sahihisho hilo thabiti na la fadhili huthibitisha kwamba mzazi anajali mtoto wake. (Mithali 22:6) Kwa hiyo wazazi msife moyo! Kwa kufuata shauri la Biblia linalofaa na la busara, mtampendeza Yehova Mungu na kuheshimiwa na watoto wenu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki