Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w03 1/15 uku. 32
  • Mashahidi wa Yehova Waliouawa Wakumbukwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mashahidi wa Yehova Waliouawa Wakumbukwa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
w03 1/15 uku. 32

Mashahidi wa Yehova Waliouawa Wakumbukwa

KATIKA Machi 7, 2002, bamba la ukumbusho lilifunguliwa katika mji wa Körmend, magharibi mwa Hungaria. Bamba hilo lilitengenezwa ili kuwakumbuka Mashahidi watatu wa Yehova waliouawa na Wanazi mwaka wa 1945.

Bamba hilo limebandikwa kwenye ukuta wa makao makuu ya sasa ya idara ya zima moto kwenye Barabara ya Hunyadi, ambapo mauaji hayo yalifanywa hadharani. Bamba hilo lilitengenezwa ili kuwakumbuka ‘Wakristo waliouawa mnamo Machi 1945 kwa kukataa kushiriki vita kwa sababu ya dhamiri. Antal Hőnisch (1911-1945), Bertalan Szabó (1921-1945), János Zsondor (1923-1945).’

Wakristo hao waliuawa miezi miwili tu kabla Vita ya Pili ya Ulimwengu kukoma. Kwa nini Wakristo hao waliuawa? Gazeti la Hungaria Vas Népe linaeleza: “Baada ya Hitler kuanza kutawala nchi ya Ujerumani, alianza kuwanyanyasa, kuwatesa, na kuwapeleka kwenye kambi za mateso, na hata kuwaua Wayahudi na pia Mashahidi wa Yehova ambao hawakukana imani yao ya kidini. . . . Mnamo Machi 1945, kulikuwa na hofu kuu magharibi mwa Hungaria. . . . Kati ya mambo yaliyosababisha hofu hiyo ni kufukuzwa na kuuawa kwa Mashahidi wa Yehova.”

Programu ya ufunguzi wa bamba hilo ilikuwa na sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ilifanywa kwenye jumba la maonyesho la Kasri ya Batthyány. Wasemaji walikuwa Profesa Szabolcs Szita, mkuu wa shirika la Holocaust Documentation Center huko Budapest; László Donáth, mshiriki wa halmashauri ya bunge iitwayo Parliament’s Committee for Human Rights, Minority and Religious Affairs; na Kálmán Komjáthy, shahidi aliyejionea mauaji hayo ambaye sasa ni mwanahistoria wa mji huo. Wahudhuriaji zaidi ya 500 walitembea kutoka sehemu moja ya mji hadi nyingine wakati wa sehemu ya pili ya programu hiyo—kufunguliwa kwa bamba hilo na Meya József Honfi wa Körmend.

Katika barua ya kuwaaga wenzake, Ján Žondor (János Zsondor) aliwahimiza ndugu na dada zake Wakristo wasihuzunike. Aliandika hivi: “Ningali nakumbuka maneno ya Yohana yanayopatikana katika andiko la Ufunuo 2:10: ‘Jithibitishe mwenyewe kuwa mwaminifu hata kufikia kifo.’ . . . Waambieni wale walio nyumbani wasihuzunike, kwa sababu nimekufa kwa ajili ya kweli si kwa sababu ya kuwa mhalifu.”

[Picha katika ukurasa wa 32]

Bertalan Szabó

[Picha katika ukurasa wa 32]

Antal Hőnisch

[Picha katika ukurasa wa 32]

Ján Žondor

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki