Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w03 12/1 uku. 32
  • Mabirika Ambayo Hayaweki Maji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mabirika Ambayo Hayaweki Maji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
w03 12/1 uku. 32

Mabirika Ambayo Hayaweki Maji

KATIKA nyakati za Biblia, mabirika yalikuwa mashimo yaliyochimbwa hasa kwa kusudi la kuweka maji. Nyakati fulani katika Nchi ya Ahadi, ndiyo pekee yaliyokuwa njia ya kuweka maji.

Alipokuwa akiandika ujumbe wa Mungu, nabii Yeremia alirejezea mabirika katika njia ya mfano akisema: “Watu wangu hawa wametenda maovu mawili; wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji ya uzima, wamejichimbia mabirika, mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji.”—Yeremia 2:13, Union Version.

Baada ya kumwacha Mungu wao Yehova—“chemchemi ya maji ya uzima”—Waisraeli waliungana na majeshi ya mataifa ya kipagani na kuabudu miungu ya uwongo, isiyo na uwezo. Kulingana na mfano wa Yeremia, makimbilio hayo yaliyotumainiwa yakawa kama mabirika yavujayo ambayo hayangeweza kutunza au kuweka chochote.—Kumbukumbu la Torati 28:20.

Je, tunaweza kujifunza chochote kutokana na mfano huo wa kihistoria? Kama ilivyokuwa katika siku za Yeremia, Mungu wa milele Yehova, ndiye Chanzo pekee cha maji ya uzima. (Zaburi 36:9; Ufunuo 4:11) Wanadamu wanaweza kupata uzima wa milele kutoka kwake tu, kupitia kwa Mwanawe, Yesu Kristo. (Yohana 4:14; 17:3) Hata hivyo, kama wale walioishi katika siku za Yeremia, watu wengi leo hulikataa na hata kulipuuza neno la Mungu lililo katika Biblia. Badala yake, wanatumaini kupata utatuzi wa haraka katika siasa, maneno matupu ya wanadamu, na mafundisho na falsafa za ubatili zinazomvunjia Mungu heshima. (1 Wakorintho 3:18-20; Wakolosai 2:8) Uamuzi ni wazi. Wewe utategemea nini? Je, utaitegemea “chemchemi ya maji ya uzima,” Yehova, au utayategemea “mabirika yavujayo, yasiyoweza kuweka maji”?

[Picha katika ukurasa wa 32]

Sanamu ya udongo ya mungu-mama iliyopatikana katika kaburi la Mwisraeli

[Hisani]

Photograph taken by courtesy of the British Museum

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki