Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w04 7/1 uku. 32
  • Barua kwa Noa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Barua kwa Noa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
w04 7/1 uku. 32

Barua kwa Noa

“KWA mpendwa Noa, nimesoma Biblia mara kadhaa kukuhusu na kuhusu jinsi ulivyojenga safina ambayo wewe na familia yako mliokolewa wakati wa Gharika.”

Hivyo ndivyo msichana mwenye umri wa miaka 15 aitwaye Minnamaria alivyoanza barua yake aliyopeleka kwenye mashindano ya wanafunzi wenye umri wa kati ya miaka 14 hadi 21. Mashindano hayo yalikuwa yamepangwa na ofisi ya huduma za simu za Finland, Shirikisho la Walimu wa Lugha ya Asili la Finland, na Shirika la Fasihi la Finland. Washindanaji hao walipaswa kuandika barua inayotegemea kitabu fulani. Ingeweza kuandikiwa mtungaji wa kitabu hicho au mtu fulani anayezungumziwa katika kitabu hicho. Walimu walichagua zaidi ya barua 1,400 za wanafunzi wao na kuzituma kwa waamuzi wa mashindano hayo. Waamuzi walichagua barua moja iliyokuwa bora zaidi, na kumi bora zilizochukua nafasi ya pili, na pia kumi bora zilizochukua nafasi ya tatu. Minnamaria alifurahi kwamba barua yake iliwekwa katika kundi la tatu.

Kwa nini Minnamaria, mwanafunzi tineja, alimwandikia Noa barua, mtu aliyeishi miaka 5,000 hivi iliyopita? Anaeleza: “Kwanza nilifikiria Biblia. Ninajua vizuri watu wanaozungumziwa katika Biblia. Nimesoma mambo mengi kuwahusu hivi kwamba machoni pangu ni kana kwamba wako hai. Nilichagua kumwandikia Noa kwa sababu maisha yake yalikuwa yenye kusisimua sana, nayo yalikuwa tofauti na yangu.”

Minnamaria alimalizia barua aliyomwandikia Noa kwa kusema: “Bado wewe ni kielelezo kizuri cha imani na utii. Maisha yako yanawatia moyo wote wanaosoma Biblia ili watende kupatana na imani yao.”

Barua hii ya msomaji wa Biblia aliye kijana inaonyesha vizuri kwamba Biblia ‘iko hai nayo ina nguvu’ juu ya watu, vijana kwa wazee.—Waebrania 4:12.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki