Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w05 1/15 uku. 32
  • “Siri Yako Ni Nini?”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Siri Yako Ni Nini?”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
w05 1/15 uku. 32

“Siri Yako Ni Nini?”

SWALI hilo lililoulizwa na mwanamume fulani mzee-mzee kwenye mkahawa wa vyakula vyepesi, lilimshangaza Muriel, mama mwenye watoto watatu. Muriel alikuwa na shughuli nyingi za kuwapeleka watoto wake kwa daktari, na alikuwa amechelewa. Hawakuwa na wakati wa kutosha kwenda nyumbani ili kula chakula cha jioni kabla ya kwenda kwenye mikutano yao ya Kikristo. Kwa hiyo, aliwapeleka watoto wake kwenye mkahawa mmoja ulio karibu ili waweze kula.

Walipokuwa wakimaliza chakula chao, mtu fulani alimkaribia Muriel na kusema: “Nimekuwa nikikutazama tangu ulipoingia hapa. Na nimeona tofauti kubwa kati ya watoto wako na wale ambao kwa kawaida mimi hukutana nao. Watoto hao hutumia vibaya meza na viti. Wao huweka miguu yao juu ya meza na kusukuma-sukuma viti. Lakini watoto wako ni watulivu sana na ni wenye adabu. Siri yako ni nini?”

Muriel alijibu: “Mimi na mume wangu hujifunza Biblia kwa ukawaida pamoja na watoto wetu, nasi hujitahidi kutumia maishani mwetu mambo tunayojifunza. Sisi ni Mashahidi wa Yehova.” Ndipo mtu huyo akasema: “Mimi niliokoka yale Maangamizi Makubwa ya Wayahudi. Nakumbuka niliwaona Mashahidi wa Yehova wakiteswa huko Ujerumani. Hata wakati huo, walionekana kuwa tofauti. Nimevutiwa sana na tabia ya watoto wako. Nitachunguza dini yako kwa makini.”

Biblia ni kitabu kinachotoa mwongozo mzuri sana wa kulea watoto. Mashahidi wa Yehova hufurahi sana kuwasaidia wengine wanufaike na mwongozo wa Biblia. Tunakualika kwa uchangamfu ukubali mwaliko ufuatao.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki