Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w05 5/15 uku. 32
  • Unajenga Juu ya Msingi Gani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Unajenga Juu ya Msingi Gani?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
w05 5/15 uku. 32

Unajenga Juu ya Msingi Gani?

NYUMBA inahitaji hasa kuwa na msingi thabiti ili iweze kudumu. Nyakati nyingine Biblia hutumia kanuni hiyo katika maana ya mfano.

Kwa mfano, nabii Isaya anasema kwamba Yehova Mungu ndiye ‘anayeweka msingi wa dunia.’ (Isaya 51:13) Msingi huo unamaanisha sheria za Mungu zisizoweza kubadilika, ambazo hudhibiti jinsi dunia inavyosonga na kuifanya idumu mahali pake. (Zaburi 104:5) Pia, Neno la Mungu, Biblia, hutaja “misingi” inayotegemeza wanadamu ambayo ni haki, sheria, na utulivu. Misingi hiyo ‘ikibomolewa,’ au kudhoofishwa, kupitia ukosefu wa haki, ufisadi, na jeuri, mvurugo hutokea.—Zaburi 11:2-6; Methali 29:4.

Kanuni hiyo pia inaweza kutumika kuhusu mtu mmoja-mmoja. Yesu Kristo alimalizia Mahubiri yake ya Mlimani kwa kusema: “Kila mtu anayesikia maneno yangu haya na kuyatenda atafananishwa na mtu mwenye busara, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. Na mvua ikanyesha na mafuriko yakaja na pepo zikavuma na kuipiga nyumba hiyo, lakini haikuporomoka, kwa maana msingi wake ulikuwa umejengwa juu ya mwamba. Zaidi ya hayo, kila mtu anayesikia maneno yangu haya na hayatendi atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga. Na mvua ikanyesha na mafuriko yakaja na pepo zikavuma na kuigonga nyumba hiyo, nayo ikaporomoka, na anguko lake lilikuwa kubwa.”—Mathayo 7:24-27.

Unajenga maisha yako juu ya msingi gani? Je, unayajenga juu ya mchanga wa falsafa za wanadamu wasiomwogopa Mungu, ambazo zitaporomoka? Au unajenga juu ya mwamba kwa kutii maneno ya Yesu Kristo, ambayo yatakusaidia kuokoka dhoruba za mfano maishani?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki