Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w06 2/1 uku. 32
  • Je, Wewe Ni Kama Mti wa Lagani Auna?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wewe Ni Kama Mti wa Lagani Auna?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
w06 2/1 uku. 32

Je, Wewe Ni Kama Mti wa Lagani Auna?

KATIKA kijiji kimoja nje ya Bandari ya Moresby, Papua New Guinea, wahudumu wawili walikuwa wakirudi nyumbani kutoka katika kazi ya kuhubiri. Walipokuwa wakitembea, waliona mti maridadi. Aliyekuwa mzee kwa umri akasema: “Ah, ona lagani auna!” Akimgeukia mhudumu kijana, aliendelea kusema hivi: “Jina hilo linamaanisha ‘mti wa kila mwaka.’ Tofauti na miti mingi ya nchi za joto, kila mwaka mti huo huangusha majani yake na huonekana kuwa umekauka. Hata hivyo, mvua inaponyesha, mti huu huchipua maua na kuwa maridadi tena.”

Tunaweza kujifunza jambo fulani kutokana na mti wa lagani auna, kama unavyojulikana. Kulingana na wataalamu fulani, mti huo ni miongoni mwa miti mitano maridadi zaidi ulimwenguni ambayo huchipua maua. Ingawa unapoteza maua na majani yake wakati wa kiangazi, mti huo huhifadhi maji. Mizizi yake ni yenye nguvu na inaweza kukua kwenye miamba iliyo chini ya ardhi. Kupitia mizizi hiyo, mti huo hustahimili upepo mkali. Kwa ufupi, mti huo unasitawi kwa kujipatanisha na hali ngumu zaidi.

Huenda tukajikuta katika hali ambazo zinajaribu ubora wa imani yetu. Ni nini kitakachotusaidia kuvumilia? Kama mti wa lagani auna, tunaweza kunywa na kuhifadhi maji ya Neno la Mungu yanayotoa uzima. Tunapaswa pia kushikamana kabisa na ‘mwamba wetu,’ Yehova, na pia tengenezo lake. (2 Samweli 22:3) Kwa kweli, mti wa lagani auna unatukumbusha vizuri kwamba hata katika hali ngumu, tunaweza kudumisha nguvu za kiroho na uzuri wetu ikiwa tutafaidika na msaada ambao Yehova anatutolea. Kwa kufanya hivyo, ‘tutarithi ahadi’ ambazo ametutolea, kutia ndani ahadi ya uzima wa milele.—Waebrania 6:12; Ufunuo 21:4.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki