Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w06 11/1 uku. 32
  • Daniel na Beji Yake ya Kusanyiko

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Daniel na Beji Yake ya Kusanyiko
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
w06 11/1 uku. 32

Daniel na Beji Yake ya Kusanyiko

YESU aliwakemea viongozi wa kidini waliojiona kuwa waadilifu ambao walikasirika walipowaona wavulana wadogo wakimsifu Mungu hadharani. Kwa kufaa, Yesu aliwauliza hivi: “Je, ninyi hamkusoma hili kamwe, ‘Kutoka katika kinywa cha watoto na wanaonyonya umetoa sifa’?”—Mathayo 21:15, 16.

Daniel mwenye umri wa miaka sita, anayeshirikiana na kutaniko la lugha ya Kirusi huko Ujerumani, anathibitisha kwamba bado vijana wanamsifu Yehova. Akiwa pamoja na mama yake na dada yake, alihudhuria kusanyiko la wilaya la Mashahidi wa Yehova huko Duisburg. Hiyo ilikuwa mara yao ya kwanza kuhudhuria kusanyiko kubwa kama hilo. Mambo yote yalikuwa mapya: hoteli, umati mkubwa, kuketi kwa utulivu kwa siku tatu, ubatizo, na hata drama. Naye Daniel alijiendeshaje? Mwenendo wake ulikuwa mzuri sana.

Siku ya Jumatatu (Siku ya Kwanza) baada ya kusanyiko, wakiwa wamerudi nyumbani, Daniel aliamka mapema ili kwenda shuleni. Lakini bado alikuwa na nini kwenye koti lake? Beji iliyomtambulisha kuwa mjumbe wa kusanyiko! Mama yake alimwambia hivi: “Kusanyiko limekwisha. Leo unaweza kuvua beji yako.” Lakini Daniel akasema: “Ninataka kila mtu ajue mahali nilipokuwa na mambo niliyojifunza.” Hivyo, siku yote hiyo shuleni, alifurahi sana kuvaa beji yake. Mwalimu wake alipomuuliza kuhusu beji hiyo, alimweleza kuhusu programu ya kusanyiko.

Kwa kufanya hivyo, Daniel alikuwa akifuata mfano wa maelfu ya wavulana na wasichana ambao wamemsifu Yehova hadharani kwa karne nyingi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki