Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w08 4/1 uku. 32
  • Ni Nani Anayestahili Kuwatawala Wanadamu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Nani Anayestahili Kuwatawala Wanadamu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
w08 4/1 uku. 32

Hotuba ya Pekee ya Watu Wote

Ni Nani Anayestahili Kuwatawala Wanadamu?

Ni mtawala gani anayeweza

• kutatua matatizo ya kiuchumi na kuhakikisha kwamba kila mtu anapata chakula kingi na nyumba nzuri sana?

• kuzuia misiba ya asili na hivyo kuwalinda wanadamu dhidi ya uharibifu unaosababishwa na tsunami, vimbunga, au matetemeko ya nchi?

• kumaliza magonjwa yote, hata kuwarudishia wazee nguvu zao za ujana?

• kukomesha vita vyote na hivyo kufanya raia wake waishi kwa amani na usalama?

• kuboresha mazingira ya dunia na kuigeuza kuwa paradiso?

Kuna Mtawala mmoja tu anayeweza kufanya mambo hayo yote mazuri. Ni nani huyo? Swali hilo litajibiwa katika hotuba ya watu wote yenye kichwa “Ni Nani Anayestahili Kuwatawala Wanadamu?” Hotuba hiyo ya Biblia itatolewa ulimwenguni pote katika zaidi ya nchi 230. Katika sehemu nyingi, itatolewa kwenye Jumba la Ufalme la Mashahidi wa Yehova Jumapili (Siku ya Yenga), Aprili 6, 2008 (6/4/2008). Mashahidi katika eneo lenu watafurahi kukueleza saa na mahali wanapokutana. Unakaribishwa kwa uchangamfu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki