Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w11 3/1 uku. 23
  • Je, Wajua?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wajua?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Habari Zinazolingana
  • Ndoa ya Ndugu Mkwe
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
  • Ukristo wa Mapema na Serikali
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Kitabu Cha Biblia Namba 50—Wafilipi
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
  • Ile Serikali Kubwa ya Sita ya Ulimwengu Roma!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
w11 3/1 uku. 23

Je, Wajua?

“Wale wa nyumbani mwa Kaisari” waliotuma salamu za Kikristo kwa Wafilipi kupitia Paulo, ni akina nani?

▪ Mtume Paulo aliliandikia kutaniko la Filipi akiwa Roma yapata mwaka wa 60 hadi 61 W.K., na Kaisari aliyemtaja alikuwa Maliki Nero. Lakini ni nani katika nyumba ya Nero angetuma salamu kwa Wakristo waliokuwa Filipi?—Wafilipi 4:22.

Itakuwa kosa kufikiri kuwa maneno “nyumbani mwa Kaisari” lazima yawe yalimaanisha watu wa ukoo wa karibu wa maliki huyo. Badala yake, yalirejelea watu wote kutia ndani watumwa na watu waliowekwa huru huko Roma na pia mikoani, ambao walimtumikia maliki. Kwa hiyo, maneno “wale wa nyumbani mwa Kaisari” huenda yalitia ndani maelfu ya watumishi ambao walishughulikia majukumu mbalimbali ya usimamizi wa mali zake na kazi ndogondogo katika majumba ya maliki na katika mashamba yake. Wengine hata walifanya kazi serikalini.

Inaonekana kuwa baadhi ya watumishi wa maliki wa Roma walipata kuwa Wakristo. Haijulikani kama hilo lilitokana na ushahidi ambao Paulo alitoa jijini Roma. Vyovyote vile, inaonekana kwamba walipendezwa kwa njia ya pekee na kutaniko la Filipi. Kwa kuwa, Filipi lilikuwa koloni la Roma na watu wengi walioishi huko walikuwa wanajeshi na wafanyakazi wa serikali waliostaafu, inawezekana kuwa wale waliomtuma Paulo salamu walikuwa rafiki za baadhi ya Wakristo wa Filipi.

Ndoa ya ndugu-mkwe inayotajwa katika Sheria ya Musa ni nini?

▪ Katika Israeli la kale, ikiwa mtu angekufa bila kupata mtoto wa kiume, ilitazamiwa kuwa ndugu yake angemwoa mjane aliyeachwa ili kuzaa watoto watakaoendeleza uzao wa ndugu yake aliyekufa. (Mwanzo 38:8) Mpango huo ambao baadaye ulikuja kuwa sehemu ya Sheria ya Musa, uliitwa ndoa ya ndugu-mkwe. (Kumbukumbu la Torati 25:5, 6) Tendo la Boazi linaloelezwa katika kitabu cha Ruthu, linaonyesha kuwa jukumu hili lingeweza kutekelezwa hata na wanaume wengine wa ukoo ikiwa mtu aliyekufa hakuwa na ndugu walio hai.—Ruthu 1:3, 4; 2:19, 20; 4:1-6.

Uhakika wa kwamba Masadukayo walirejelea ndoa ya ndugu-mkwe katika Marko 12:20-22, ni uthibitisho kuwa mpango wa ndoa ya ndugu-mkwe ulikuwapo katika siku za Yesu. Mwanahistoria Myahudi Flavio Yosefo anasema kuwa mpango huo uliendeleza jina la familia na pia kusaidia kutunza mali ya familia na kuhakikisha kuwa mjane ametunzwa. Wakati huo, mke hakuwa na haki ya kurithi mali ya mume wake. Hata hivyo, mtoto aliyezaliwa katika ndoa ya ndugu-mkwe, angerithi mali ya baba aliyekufa.

Sheria iliwaruhusu watu wa ukoo kukataa kutekeleza ndoa ya ndugu-mkwe. Lakini mwanamume ambaye angekataa“kujenga nyumba ya ndugu yake” angeonekana kuwa amekosa heshima.—Kumbukumbu la Torati 25:7-10; Ruthu 4:7, 8.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki