Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w13 11/1 uku. 3
  • Kwa Nini Watu Wanashindwa Kumpenda Mungu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kwa Nini Watu Wanashindwa Kumpenda Mungu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Habari Zinazolingana
  • Ukweli Unaweza Kukuweka Huru
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Uwongo Unaomfanya Mungu Asieleweke
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Uwongo Unaomfanya Mungu Aonekane Kuwa Mkatili
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Mpende Mungu Anayekupenda
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
w13 11/1 uku. 3

HABARI KUU | UWONGO UNAOFANYA WATU WASIMPENDE MUNGU

Kwa Nini Watu Wanashindwa Kumpenda Mungu?

“‘Lazima umpende Yehova Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote na kwa akili yako yote.’ Hii ndiyo amri iliyo kuu na ya kwanza.”​—Yesu Kristo, 33 W.K.a

Baadhi ya watu huhisi ni vigumu kumpenda Mungu. Wao hufikiri Mungu haeleweki, hajali, au hata ni mkatili. Fikiria maneno yafuatayo:

  • “Nilisali kwa Mungu ili anisaidie lakini wakati huo huo nilihisi yuko mbali sana na haiwezekani kumkaribia. Nilifikiri kwamba Mungu hana utu wala hisia.”​—Marco, Italia.

  • “Ingawa nilitamani sana kumtumikia Mungu, nilihisi yuko mbali sana. Nilifikiri kwamba yeye ni Mungu mkatili ambaye hupenda kutuadhibu tu. Sikuamini kwamba ana hisia nyororo.”​—Rosa, Guatemala.

  • “Nilipokuwa mtoto, niliamini kwamba Mungu hutafuta makosa yetu na yuko tayari kutuadhibu tunapomkosea. Baadaye, nilihisi Mungu hajali. Nilimwona Mungu kama waziri mkuu anayeongoza mambo ya watu lakini hapendezwi nao.”​—Raymonde, Kanada.

Wewe una maoni gani? Je, inawezekana kumpenda Mungu? Wakristo wamejiuliza swali hilo kwa karne nyingi. Isitoshe, katika Enzi za Kati, Wakristo wengi hawakusali kwa Mungu Mweza-Yote. Kwa nini? Watu wengi walimwogopa Mungu kupita kiasi. Mwanahistoria Will Durant anafafanua hivi hali hiyo: “Mtenda dhambi anawezaje kusali kwa Mungu mkatili na asiyejali?”

Ni nini kilichofanya watu waanze kumwona Mungu kuwa “mkatili na asiyejali”? Biblia inafundisha nini hasa? Je, kujifunza ukweli kumhusu Mungu kunaweza kukufanya umpende?

a Mathayo 22:37, 38.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki