Matangazo
● Toleo la fasihi kwa Agosti: Broshua yoyote ya kurasa 32 isipokuwa broshua Shule. Septemba: Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation? Oktoba: Andikisho la ama Amkeni! au Mnara wa Mlinzi au yote mawili. Novemba: New World Translation of the Holy Scriptures na ama Should You Believe in the Trinity? au “Tazama! Mimi Ninafanya Vitu Vyote Kuwa Vipya.”
● 1991 Calendar of Jehovah’s Witnesses itaonyesha utendaji wetu mbalimbali wa kihuduma katika mabara sita ikiwa na hesabu kadhaa ya picha zenye rangi za kuvutia za matawi, Majumba ya Ufalme, na tamasha za utoaji ushahidi wa Ufalme. Makundi yapaswa kuanza kuomba 1991 Calendar pamoja na ombi lao la fasihi la Septemba. Kalenda hizo zitapatikana katika Kiingereza na Kifaransa. Kalenda ni bidhaa za kuombwa kipekee. Hadi kalenda zipatikane na kutumwa, zitakuwa “Subiri” kwenye orodha za kupakia za kundi.
● Kuanzia Agosti 29 hadi Septemba 1, Sosaiti itakuwa ikihesabu fasihi zote zilizopo Betheli. Kwa sababu ya uhesabu huo, hakuna maombi yoyote ya kundi yatakayoshughulikiwa yatumwe wala kuchukuliwa wakati wa siku hizo.
● Kila kundi litapokea fomu tatu za Orodha ya Vitabu na yapaswa kuhesabu kihalisi fasihi za kampeni. Tafadhali jazeni fomu hizo kikamili, na kupeleka ya awali kwetu, si baada ya Septemba 6, 1990. Tunzeni nakala-kaboni kwa ajili ya faili zenu. Twawapelekea nakala ya tatu iwe nakala ya kufanyia kazi.
● Wahubiri wote wapaswa kufanya upya maandikisho yao ya Mnara wa Mlinzi na Amkeni! kupitia kundi. Itasaidia pia ikiwa wahubiri wataagiza fasihi za kibinafsi na vifaa vinginevyo kupitia kundi badala ya kupeleka maagizo ya kibinafsi kwenye tawi.
● Rekebisho: Kwenye ukurasa 73 wa kitabu Kuokolewa, tafadhalini mahali pa mistari 6-15 wekeni hivi: “jipya; si Waisraeli wa kiroho. Wao ni watu wanaokusanywa ndani ya uandalizi wa Yehova wa uhai wa milele duniani kwa msingi wa imani yao katika thamani ya kidhabihu ya damu ya Yesu. Wengi wao sasa wanaingia katika ushirikia wa karibu na washiriki wa Israeli wa kiroho wakati hawa wangali duniani, na pamoja nao, wanatumainia Kristo akiwa ndiye Mchungaji Mwema. Wale wa “kondoo wengine” ambao wangali hai duniani na ambao sasa hujidhihirisha wanajumuika kuwa “mkutano mkubwa” wa Ufunuo 7:9, 10, 14, walio na tazamio la kuokoka dhiki kubwa inayokuja.”
● Rekebisho: Katika Pitio la Kuandika Na. 271, Karatasi ya Maswali (S-97) na Karatasi ya Majibu (S-98). Swali 32, mstari 4 lapasa kubadilishwa kutoka uku. 22 kuwa uku. 24. Swali 34, mstari 3 wapasa kubadilishwa kutoka uku. 21 kuwa uku. 23.