Matangazo
● Toleo la fasihi la Oktoba: Andikisho la ama Amkeni! au Mnara wa Mlinzi au yote mawili. Novemba: New World Translation of the Holy Scriptures na Should You Believe in the Trinity? au “Tazama! Mimi Ninafanya Vitu Vyote Kuwa Vipya.” Desemba: Kitabu Hadithi za Biblia au Kuishi Milele. Januari na Februari: Kitabu chochote cha zamani zaidi cha kurasa 192 kilichochapwa kabla ya 1980.
● Makundi yapaswa kuanza kuagiza Kuyachunguza Maandiko Kila Siku—1991 pamoja na agizo lao la vitabu la Oktoba. Vijitabu hivyo vitapatikana katika Kiarabu, Kiingereza, Kifaransa na Kiswahili.
● Kadi za beji za Mkusanyiko wa Wilaya wa mwaka wa 1990 katika Kiingereza na Kiswahili zitapelekwa na kutiwa pamoja na upakizi ujao wa fasihi. Hazihitaji kuagizwa. Kulingana na ukubwa wa kila kundi, bidhaa zitapangwa katika vifungu vya 25. Hesabu ya fasihi itatozwa kwa kulingana na kiasi. Ikiwa kadi za beji zaidi zahitajiwa na kundi, hizo zapasa kuagizwa katika fomu ya Agizo la Vitabu (S-14). Mwahitaji kuagiza vishikilizo vya plastiki vya kadi za beji kwa wowote kundini wanaovihitaji.
● Ratiba ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa 1991 imepangwa hivi kwamba kitabu Ujana Wako chaweza kutumiwa kuwa chimbuko la habari kwa ajili ya hotuba Na. 4 badala ya kitabu Young People Ask kwa kuwa hicho cha pili bado hakipatikani katika Kiswahili.
● Kama ilivyoonyeshwa katika Huduma ya Ufalme Yetu ya Septemba, kitabu “All Scripture Is Inspired of God and Beneficial,” chapa iliyosahihishwa katika Kiingereza kitapatikana karibuni. Makundi yaombwa yaagize upesi iwezekanavyo.
●“Lugha Iliyo Safi” Mkusanyiko wa Wilaya
Tarehe: Mahali:
Novemba 1-4, 1990
Mbeya, Tanzania
Novemba 29–Desemba 2, 1990
Mombasa, Kenya
Mbale, Uganda
Desemba 6-9, 1990
Eldoret, Kenya
Kampala, Uganda
Desemba 13-16, 1990
Dar es Salaam, Tanzania
Moshi, Tanzania
Desemba 20-23, 1990
Nairobi, Kenya
Desemba 27-30, 1990
Kisumu, Kenya
Mwanza, Tanzania