Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Katika Kaseti
1 Mnara wa Mlinzi na Amkeni! katika Kiingereza sasa yanapatikana katika kaseti kwa msingi wa uandikisho wa kila mwaka. Ingawa zinapatikana kwa kila mtu, maandalizi hayo yatakuwa yenye msaada hasa kwa wale wenye vizuizi vya kimwili ambao huwazuia kusoma magazeti yetu yaliyochapishwa. Mirekodi hiyo itasaidia watoto na wengine pia wanaojitahidi kufanyia maendeleo ustadi wao wa kusoma.
2 Makala nyingi katika kila toleo la magazeti hayo zitatiwa ndani katika kaseti moja ambayo itapelekwa moja kwa moja kwa mwandikishaji mara mbili kwa mwezi. Tafadhali fahamu yafuatayo. Maandikisho hayo yakishatolewa, hasara yoyote inayotokea wakati wa kuyasafirisha itakuwa juu ya mpokeaji. Sosaiti haitakubali daraka kwa bidhaa zisizopokewa au bidhaa zinazopotea katika mfumo wa upelekaji. Mara Sosaiti ikishapeleka kaseti hizo kwa njia ya posta Sosaiti haitakubali daraka la kuzikabidhi kwa wenyewe. Mwandishi pamoja na ndugu anayeshughulikia maandikisho katika kundi apasa kuhakikisha kwamba mwongozo ulioonyeshwa hapo juu umeelezwa waziwazi kwa kila mwandikishaji wa magazeti katika kaseti.
3 Bei ya uandikisho kwa magazeti katika kaseti itakuwa kama ifuatavyo:
Kwa Njia ya Posta Kwa Ndege
Wahubiri
na Wote: Kshs. 1,400/- 2,350/-
Painia: Kshs. 1,250/- 2,190/-
Kwa mengine yote tafadhali uliza. Maandikisho yote ni ya mwaka mmoja tu; hakutakuwa na bei ya uandikisho wa miezi sita.
4 Fomu za pekee za uandikisho wa kaseti zinapelekwa kwa makundi, na hizo zaweza kupatikana kutoka kwa ndugu anayeshughulikia maandikisho. Fomu iliyokamilishwa yapaswa irudishwe kwake ili aipeleke kwa Sosaiti pamoja na maandikisho yale mengine ya kawaida. Kwa maandikisho ya kaseti msitumie fomu za kawaida za maandikisho ya magazeti.
5 Kwa faida ya vipofu na wale wasioweza kimwili kutumia au kusoma maandishi madogomadogo yaliyochapishwa, Sosaiti inafanya kaseti za Mnara wa Mlinzi na Amkeni! zipatikane kwa bei iliyopunguzwa ambayo iko chini ya gharama za ufanyizaji. Wale wanaostahili kwa bei hiyo iliyopunguzwa watapokea kaseti zao bila malipo ya posta zikiwa “Bidhaa za Bure kwa Vipofu na Walemavu.” Ili kustahili, itakuwa lazima kutoa kithibitisho cha kuwa na kizuizi cha kimwili kwa kila uandikisho uliopunguzwa bei. Hilo laweza kuwa kwa namna ya hati ya uthibitisho, ambayo hutolewa na mashirika ya kusaidia vipofu, itolewayo na madaktari, wastadi wanaotibu walemavu, na kadhalika. Au kwa msingi wa kufahamiana kibinafsi na mwandikishaji, mwandishi wa kundi aweza kutia sahihi taarifa ya uhakikisho katika upande wa nyuma wa kikaratasi cha uandikishaji wa pekee. Tafadhali mfahamu kwamba kutojua kusoma pekee hakustahilishi yeyote kulipa bei iliyopunguzwa.
6 Ingawa Mnara wa Mlinzi na Amkeni! kwenye kaseti yatathaminiwa zaidi na wale walio na vizuizi vya kuona, Sosaiti ina furaha kufanya mirekodi hiyo ya kaseti ipatikane kwa wowote ambao huenda wakataka kufaidika kutokana na Mnara wa Mlinzi na Amkeni! kwenye utepe, kuongezea kurasa zilizochapishwa.