Matangazo
◼ Fasihi inayotolewa Machi: Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu! Aprili na Mei: Uandikishaji wa Mnara wa Mlinzi. Juni: Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi. TAARIFA: Makundi yatakayohitaji vifaa vya kampeini vilivyotajwa juu yapaswa yaviagize kwenye Fomu ya Agizo la Vitabu (S-14-SW) la kila mwezi litakalofuata.
◼ Mwangalizi msimamizi au mtu yeyote aliyepewa mgawo naye apaswa kukagua hesabu ya kundi Machi 1 au upesi iwezekanavyo baada ya hapo. Tangazia kundi hilo lifanywapo.
◼ Barua kutoka kwa Sosaiti yenye tarehe ya Februari 14, 1992, yaliyoandikiwa makundi yote ilitangaza Mchango wa Mkusanyiko wa 1993 wa kusaidia wamishonari wazuru nchi za kwao na kuhudhuria mmojapo wa mikusanyiko ya wilaya ya mwaka huu. Machi utakuwa mwezi wa mwisho kupeleka michango kwa Sosaiti kwa ajili ya Mchango wa Mkusanyiko wa 1993. Utegemezo wenu mkarimu wa mpango huo wathaminiwa sana.
◼ Mapainia wa kawaida wanaopendezwa kushiriki katika kampeini ya mwaka huu ya maeneo ya mbali kuanzia Julai hadi Septemba wakiwa mapainia wa pekee wa muda waweza sasa kutoa maombi yao kupitia baraza la wazee (au halmashauri ya utumishi) la kundi lao, litakalotuletea maombi na mapendekezo yao kwetu kufikia Aprili 15, 1993, hiyo ikiwa ni tarehe ya mwisho.
◼ Vchapo Vipya Vinavyopatikana:
Kiamhari: Je! Kweli Mungu Anatujali?; Uzima Katika Ulimwengu Mpya Wenye Amani (Trakti Na. 15); Kuna Tumaini Gani kwa Wapendwa Waliokufa? (Trakti Na. 16) Kiingereza: Faharisi 1986-90; Will There Ever Be a World Without War? Kifaransa: Faraja kwa Walioshuka Moyo (Trakti Na. 20); Furahia Maisha ya Familia (Trakti Na. 21); Kiswahili: Faraja kwa Walioshuka Moyo (Trakti Na. 20); Furahia Maisha ya Familia (Trakti Na. 21); Ni Nani Hasa Anayeutawala Ulimwengu? (Trakti Na. 22).
◼ Vichapo Vinavyopatikana Tena:
Furahia Milele Maisha Duniani! katika lugha zifuatazo: Kiacholi, Kihaya, Kitaita, Kisomali, na Kifaransa.