Matangazo
◼ Fasihi inayotolewa Mei: Uandikishaji wa Mnara wa Mlinzi na Amkeni! Juni: Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi. Julai na Agosti: Yoyote ya broshua zifuatazo yaweza kutumiwa: Je! Kweli Mungu Anatujali?, Furahia Milele Maisha Duniani!, “Tazama! Mimi Ninafanya Vitu Vyote Kuwa Vipya,” Je! Uamini Utatu?, Jina la Mungu Litakaloendelela Milele, au Serikali Itakayoleta Paradiso. Septemba: Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani. ANGALIA: Makundi yatakayohitaji vifaa vya kampeni vilivyotajwa juu yapaswa yaviagize kwenye Fomu ya Agizo la Vitabu (S-14-SW) la kila mwezi litakalofuata.
◼ Sosaiti sasa inatokeza mabuku yaliyojalidiwa ya Kiingereza ya Mnara wa Mlinzi kwa miaka 1986 hadi 1991 vikiwa vifaa vya daima. Yeyote anayependezwa kupata mabuku hayo yaliyojalidiwa anapaswa kuyaagiza kupitia kundi. Miaka ijayo ya mabuku yaliyojalidiwa ya Mnara wa Mlinzi Kiingereza, pamoja na yale ya 1992, yatakuwa vifaa vya daima na vyaweza kuagizwa wakati wowote. Tafadhali kumbuka kwamba mabuku yaliyojalidiwa ni vyombo vya kuagizwa kipekee.
◼ Kitolewaji kingine cha disketi za kompyuta kinapatikana: New World Translation of the Holy Scriptures—With References/Insight on the Scriptures. Kitolewaji hiki kina New World Translation na mabuku yote mawili ya Insight. Hiki chapatikana tu kwa Kiingereza katika diski za inchi 5 1/4 megabaiti 1.2 au inchi 3 1/2 megabaiti 1.44. Kompyuta iliyo na diski ngumu inayoweza kuwa na kiwango cha nafasi ya megabaiti 18 yahitajiwa. Barua iliyopelekwa kwa makundi yote inaandaa habari ya zaidi kuhusu kifaa hiki kipya na jinsi ya kukiagiza. Diski iliyo na Biblia pekee itaendelea kupatikana.
◼ Sosaiti inafanyiza CD-ROM ya kutumia na makompyuta. Hii ni diski imara ikiwa na kumbukumbu inayokuwezesha kusoma tu. Itaruhusu mmoja aone kwenye skrini ya kompyuta na kurejezea kwenye New World Translation, yale mabuku ya Insight, Mnara wa Mlinzi, kuanzia 1950 hadi 1993, na vichapo vinginevyo vyetu. CD-ROM itatia ndani programu iliyotengenezwa na Sosaiti ambayo ina uwezo mwingi wa kutafuta-tafuta vichapo hivyo. Chombo kinachofaa cha kusoma CD-ROMs kitahitajiwa. Programu hii ya CD-ROM yatumainiwa kuwa tayari mapema mwaka ujao. Tafadhali usiandikie au kupigia Sosaiti simu ukiomba habari. Habari ya chombo hicho itakapokamilishwa, tutapelekea makundi yote barua, inayotoa habari zaidi kuhusu chombo kinachohitajiwa kutumia CD-ROM mpya.
◼ Makundi yanatiwa moyo kufikiria mahitaji ya New World Translation of the Christian Greek Scriptures katika Kiswahili na kutoa maagizo yao. Habari hii ya mapema itasaidia Sosaiti kujua ni nakala ngapi zapaswa kuchapwa.
◼ Yeyote anayependezwa na kusaidia kutafsiri Kiswahili kwa wakati wote anaweza kujulisha Sosaiti katika barua kwa ofisi ya tawi. Wale wanaopendezwa wanapaswa kuwa na ujuzi na udhibiti unaofaa wa kutumia lugha za Kiingereza na Kiswahili.
◼ Ugavi wa fomu za kutosha za kutumia wakati wa mwaka wa utumishi wa 1994 zitapelekwa kwenye kila kundi. Fomu hizo hazipasi kutumiwa vibaya. Zapaswa kutumiwa kama zilivyokusudiwa. Zikitumiwa kwa uangalifu, ugavi huo wapaswa kumaliza mwaka wote wa utumishi, hivyo ikifanya uwezekano wa kutoagiza nyingine zaidi wakati wa mwaka. Tafadhali angalieni barua ya Agosti 14, 1992 inayoonyesha fomu mtakazotazamia kupokea. Fomu zisizo kwenye orodha zapaswa kuagizwa.
◼ Vichapo Vipya Vinavyopatikana:
Kiarabu: Jehovah’s Witnesses—A Christian Community (kwa Waislamu). Kifaransa: Will There Ever Be a World Without War? (kwa Wayahudi).
◼ Kaseti Mpya Zinazopatikana:
Kifaransa: Preserving Life in Time of Famine (Drama; kaseti moja).
◼ VICHAPO VIFUATAVYO HAVICHAPWI:
Kiingereza: Life Does Have a Purpose. Kiswahili: “Habari Njema Hizi za Ufalme.”
◼ Vichapo Vipya kwa Ajili ya Vipofu Vyapatikana:
Gredi ya pili ya Kiingereza: Kuyachunguza Maandiko Kila Siku—1993 (mabuku manne); Tumefanywa Tengenezo Tutimize Huduma Yetu (mabuku matano; 1989 toleo la karibuni); Ratiba ya Shule ya Kitheokrasi ya 1993 (buku moja); Je! Ulimwengu Huu Utaokoka? (Trakti Na. 19; buku moja); Faraja kwa Walioshuka Moyo (Trakti Na. 20; buku moja); Furahia Maisha ya Familia (Trakti Na. 21; buku moja); Ni Nani Hasa Anayeutawala Ulimwengu? (Trakti Na. 22; buku moja). Andika maagizo ya vichapo vya maandishi ya vipofu hivi, ANGALIA: DAWATI YA BRAILLE. Tia ndani jina na anwani ya mtu atakayetumia maandishi ya vipofu.