Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 10/95 uku. 11
  • Matangazo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Matangazo
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1995
Huduma Yetu ya Ufalme—1995
km 10/95 uku. 11

Matangazo

◼ Fasihi ya kutumiwa wakati wa Oktoba: Maandikisho ya Amkeni! na Mnara wa Mlinzi. Fanya jitihada ya pekee kuangusha nakala za magazeti hayo. Novemba: Toa New World Translation pamoja na kitabu Biblia—Neno la Mungu au la Binadamu? Desemba: Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi. Januari: Kitabu chochote chenye kurasa 192 kilichotangazwa kabla ya 1982 ambacho kutaniko laweza kuwa navyo akibani. Makutaniko ambayo hayana ugavi wa vitabu hivyo yaweza kutoa Kuokolewa Kuingia Katika Dunia Mpya. TAARIFA: Makutaniko ambayo bado hayajaagiza vifaa vya kampeni vilivyotajwa juu yapaswa kufanya hivyo katika Fomu ya Kuomba Fasihi yao ya kila mwezi itakayofuata (S-14-SW).

◼ Moja ya nyongeza katika toleo hili la Huduma ya Ufalme Yetu ni “Ratiba ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi ya 1996” na yapasa kuwekwa kwa ajili ya marejezo katika mwaka 1996. Waangalizi wasimamizi wanapaswa kuhakikisha wanachukua ugavi wao kutoka kwenye idara ya fasihi kwenye mkusanyiko wa wilaya.

◼ Kama ilivyotangazwa katika Huduma ya Ufalme Yetu ya Septemba 1995, ziara za matembezi za jengo jipya la Betheli katika Nairobi zawezekana kuanzia Jumatano hadi Jumamosi, saa 2:00 asubuhi hadi saa 5:30 asubuhi na kuanzia 7:00 alasiri hadi saa 10:00 alasiri. Tafadhali hakikisha kuja na kadi yako ya Mwelekezo wa Mapema Kuhusu Tiba/Ondoleo la Hatia.

◼ Mahali pa mkusanyiko wa wilaya wa Nanyuki pamebadilishwa kuwa ASK Show Grounds, Nyeri. Tarehe zabaki zikiwa zilezile, Desemba 22-24, 1995.

◼ Makutaniko yapaswa kuanza kuagiza Kuyachunguza Maandiko Kila Siku—1996 pamoja na agizo lao la fasihi la Oktoba. Vijitabu hivyo vitapatikana katika Kiarabu, Kifaransa, Kiingereza, Kinyarwanda na Kiswahili. Vijitabu Kuyachunguza Maandiko ni bidhaa za agizo la pekee.

◼ Vichapo Vipya vya Braille Vipatikanavyo:

Kuyachunguza Maandiko Kila Siku—1996 (mabuku manne) —Kiingereza gredi ya pili

Ratiba ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi ya 1996 (buku moja) —Kiingereza gredi ya pili

Tafadhali tieni jina na anwani ya mtu ambaye atatumia hicho kichapo cha Braille.

◼ Kaseti Mpya za Video Zinazopatikana:

The New World Society in Action (Pitio la filamu ya kihistoria 1954 yenye kichwa hicho hicho) —Kiingereza

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki