Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 11/96 uku. 3
  • Mahali pa Kulala pa Mwangalizi wa Mzunguko

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mahali pa Kulala pa Mwangalizi wa Mzunguko
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1996
Huduma Yetu ya Ufalme—1996
km 11/96 uku. 3

Mahali pa Kulala pa Mwangalizi wa Mzunguko

Twathamini sana kazi za ndugu zetu wanaotumika katika utumishi wa wakati wote wakiwa waangalizi wasafirio, sivyo? Kadiri hali zetu zinavyoruhusu, twaweza kuwapa moja kwa moja msaada wa kimwili. Kwa mfano, mwangalizi wa mzunguko azurupo kutaniko lako, huenda ukaweza kumwandalia makao yanayofaa, milo, au msaada kwa gharama zake za usafiri. Ukarimu kama huo haukosi kuonwa na Baba yetu wa kimbingu, anayetaka watumishi wake watunzwe. (Zab. 37:25) Miaka kadhaa iliyopita ndugu mmoja aliyeweza kuandaa vyakula vyepesi pekee alialika mwangalizi asafiriye pamoja na mkeye nyumbani mwake. Wenzi hao walipotoka waende katika huduma ya utumishi ya jioni, ndugu huyo akawapa wageni wake bahasha. Ndani mlikuwa na noti (iliyotoshana na dola moja ya Marekani) iliyokuwa pamoja na taarifa hii iliyoandikwa kwa mkono: ‘Kwa kikombe cha chai, au galani ya petroli.’ Ni uthamini mzuri kama nini ulioonyeshwa katika njia hii sahili! Tungependa kuwaandalia mahali pa kulala waangalizi wetu wasafirio. Inaonekana haijawa rahisi katika maeneo mengine na hii ni sehemu tunayotaka kuangalia.—Ona Mnara wa Mlinzi, Desemba 1, 1994, kurasa 17-18, fungu la 19.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki