Habari za Kitheokrasi
Uwekaji-wakfu wa Majumba ya Ufalme: Tuna furaha kuona makutaniko mengi yanayojitahidi kuwa na Majumba ya Ufalme yao yenyewe. Hivi majuzi Majumba ya Ufalme ya Thika na Sotik katika Kenya yaliwekwa wakfu.
Mambo Makuu Kutoka Ripoti ya Mwaka: Nchi zote zilizoko chini ya ofisi ya tawi ya Kenya zilikuwa na mwaka mzuri sana wa utendaji. Kila nchi ilikuwa na ongezeko la zaidi ya asilimia 10 katika idadi ya watangazaji: Kenya asilimia 12, Rwanda asilimia 61, Sudan asilimia 10, Tanzania asilimia 17, na Uganda asimilia 11. Kama mwezavyo kuona kwenye ripoti ya utumishi ya Agosti, tulifunga mwaka wa utumishi wa 1996 kwa vilele vipya katika idadi ya watangazaji. Utendaji wa magazeti ulionyesha maendeleo mazuri. Sehemu moja tunayotaka kuboresha ni utendaji wa painia-msaidizi. Ikiwa huwezi kutumika ukiwa painia wa kawaida, je, hali zako zakuruhusu ushiriki utendaji wa painia-msaidizi wakati wa mwaka wa utumishi wa 1997? Kwa nini usipange kimbele ufurahie utendaji huu kwa mwezi mmoja au zaidi mwaka huu wa utumishi. Twamshukuru Yehova kwa ongezeko zuri tunaloona katika shamba letu.—1 Kor. 3:5-9.
Hudhurio la Ukumbusho la 1996: Kenya: 29,000; Rwanda: 11,496; Sudan: 4,242; Tanzania: 16,978; Uganda: 5,292.