Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 8/97 kur. 5-6
  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—1997
Huduma Yetu ya Ufalme—1997
km 8/97 kur. 5-6

Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa juma la Mei 5 hadi Agosti 18, 1997. Tumia karatasi tofauti ya kuandikia majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Huruma ya Yesu, inayofafanuliwa kwenye Marko 1:41, yaonyesha hangaiko lenye kugusa moyo la Yehova kwa watu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w96-SW 3/1 uku. 5.]

2. Sehemu za siku za mwisho zapatikana tu katika Mathayo 24, Marko 13, na Luka 21. [kl-SW uku. 102 sanduku]

3. Swali la Yohana Mbatizaji linalopatikana kwenye Luka 7:19 huonyesha wazi kwamba alikosa imani. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w87-SW 1/1 uku. 16.]

4. Kwenye Sikukuu ya Kupitwa ya Yesu ya mwisho pamoja na wanafunzi wake, ni Petro tu aliyemwambia: “Hakika mimi sitakukana kwa vyovyote.” [Usomaji wa Biblia kila juma]

5. Hakuna uthibitisho wa Kibiblia unaoonyesha kwamba mtume Petro alikuwa mwanamume aliyeoa. [Usomaji wa Biblia kila juma]

6. Ufalme ambao Yesu alihubiri juu yao ni wa kusaidia, au wa pili, kwa enzi kuu ya Mungu ya ulimwengu wote mzima. [kl-SW uku. 91 fu. 4]

7. Yamkini Marko aliandika Gospeli yake hasa kwa ajili ya Wayahudi. [si-SW uku. 182 fu. 8]

8. Yesu alipowaambia Mafarisayo kwamba Ufalme wa Mungu ulikuwa katikati yao, alikuwa akijirejezea kuwa ndiye Mfalme wa wakati ujao. (Luka 17:21) [kl-SW uku. 91 fu. 6]

9. Hakuna ufafanuzi ufaao kuhusu sababu kwa nini kitabu cha Luka kina msamiati mkubwa zaidi ya ule wa wale waandikaji wengine watatu wa Gospeli wakiunganishwa. [si-SW uku. 187 fu. 2]

10. Hakuna marejezo katika Biblia ya sifa ambazo umati mkubwa lazima uonyeshe ili kuokoka Har–Magedoni. [uw-SW uku. 105 fu. 5]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Ikiwa kifungu kutoka katika Biblia chaweza kutafsiriwa kisarufi kwa njia nyingi zaidi ya moja, ni kanuni gani ya uongozi ipasayo kufuatwa na mtafsiri? [rs-SW uku. 384 fu. 3]

12. Ni nini ambacho huzuia watu fulani kukubali shauri? [uw-SW uku. 127 fu. 4]

13. Ni katika hali gani itikadi ya Utatu inaweka wale wanaoing’ang’ania? [rs-SW uku. 392 fu. 4]

14. Yesu alimaanisha nini aliposema: “Iweni na chumvi ndani yenu wenyewe, na dumisheni amani nyinyi kwa nyinyi”? (Mr. 9:50) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w85-SW 12/15 uku. 28 fu. 12.]

15. Ni somo gani lenye thamani tunaloweza kujifunza kutokana na itikio la Yesu kwa mchango wa yule mjane maskini? (Mr. 12:42-44) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w87-SW 12/1 uku. 29 fu. 7–uku. 30 fu. 1.]

16. Baadhi ya sifa za Petro zaonekanaje katika mtindo wa kuandika wa Marko, na huenda sababu ikawa nini? [si-SW uku. 182 fu. 5-6]

17. Tunapolinganisha Mathayo 6:9, 10 na Luka 11:2-4, kwa nini twaweza kufikia mkataa kwamba sala ya kigezo haikukusudiwa kurudiwa-rudiwa kwa maneno yaleyale? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 5/15 uku. 16 fu. 6.]

18. Utegemeo wetu katika uhakika wa Biblia waimarishwaje tunaposoma maandishi kama vile Luka 3:1, 2? [si-SW uku. 188 fu. 7]

19. Kulingana na Ufunuo 7:14, mtu kuosha kanzu yake kwa damu ya Mwana-Kondoo hutokeza nini? [uw-SW uku. 106 fu. 6-7]

20. Kwa kuwa twajua kwamba Yesu hakukosa imani katika Mungu, kwa nini alilia: “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniachilia mbali?” (Mr. 15:34) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w87-SW 6/15 uku. 31.]

Toa neno au fungu la maneno linalohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

21. Mkate na divai inayotumiwa kwenye sherehe ya Ukumbusho ni _________________________ tu, mkate ukiwakilisha _________________________ nayo divai ikiwakilisha _________________________ yake. [uw-SW uku. 115 fu. 13]

22. Tunapofikiria kwa uangalifu yale ambayo kwa kweli yametokea, yaonekana dhahiri kwamba mwito wa kimbingu kwa ujumla ulikamilishwa wapata mwaka wa _________________________ , wakati tumaini la kidunia la _________________________ ulipofahamiwa waziwazi. [uw-SW uku. 112 fu. 6]

23. Yohana Mbatizaji alipoanza kuhubiri, gavana wa Yudea alikuwa _________________________ na mtawala wa wilaya ya Galilaya alikuwa _________________________ . [Usomaji wa Biblia kila juma; ona Luka 3:1.]

24. Roho itoayo ushahidi na kani yenye kuchochea ya akili na moyo wa wale ambao kikweli ni watoto wa Mungu ni _________________________ . [uw-SW uku. 113 fu. 9]

25. Kama inavyoonyeshwa kwenye Luka 10:16, tunapokubali kwa uthamini maandalizi ya kiroho ambayo huja kupitia _________________________ na Baraza Linaloongoza lake, twamwonyesha _________________________ staha. [uw-SW uku. 123 fu. 13]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

26. Watakatifu wanaorejezewa kwenye Mathayo 27:52 walikuwa (wamefufuliwa kwa muda tu katika mwili; kwa kweli miili iliyokufa iliyorushwa nje ya makaburi yao na tetemeko la dunia; wamefufuliwa kwenda kwenye uhai wa kimbingu kabla ya Yesu). [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 9/1 uku. 7.]

27. Kwenye Wakolosai 1:15, Yesu anaitwa “mzaliwa wa kwanza wa uumbaji wote,” jambo ambalo humaanisha kwamba yeye ni (kama Mungu na hana mwanzo; mzaliwa wa kwanza wa wana wa Mungu duniani; mkubwa zaidi katika familia ya Yehova ya wana). [rs-SW uku. 376 fu. 3]

28. Kuwekwa rasmi kwa “mtumwa mwaminifu na mwenye busara” kulithibitishwa na roho takatifu katika mwaka wa (33 W.K.; 1918; 1919). (Mt. 24:45) [uw-SW uku. 119 fu. 6]

29. Kanuni inayopasa kufuatwa na Wakristo wote, lakini hasa wale walio katika nyadhifa za usimamizi katika tengenezo la Mungu, ni hii: “Yeye ajiendeshaye mwenyewe kama (mwenye kiburi; aliye wa maana; aliye mdogo zaidi) miongoni mwenu nyote ndiye aliye mkubwa.” (Luka 9:48) [uw-SW uku. 122 fu. 12]

30. Kama ilivyorekodiwa katika (Mathayo 10; Mathayo 24; Luka 21), Yesu alitoa maagizo mahususi ya utumishi kwa wale aliowatuma kuhubiri. [si-SW uku. 180 fu. 31]

Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

Mit. 4:13; Dan. 7:9, 10, 13, 14; Mr. 7:20-23; 13:10; Luka 8:31

31. Twapaswa kuwa chonjo kutambua uvutano wowote usiomwogopa Mungu au wenye kufisidi ambao huenda ukaja akilini na moyoni mwetu nasi twapaswa kuuondoa kabla haujatia mizizi. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 11/1 uku. 14 fu. 16.]

32. Roho waovu wataungana na Shetani katika kutotenda kwa namna ya kifo wakati wa “miaka elfu.” (Ufu. 20:3) [Usomaji wa Biblia kila juma]

33. Roho ya uharaka yahitajiwa ili kazi ya ushahidi ya ulimwenguni pote itimizwe kwa wakati mchache. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 10/1 uku. 27.]

34. Kukubali shauri kwaweza kumlinda mtu dhidi ya kusema na kufanya mambo ambayo yangeweza kusababisha majuto. [uw-SW uku. 128 fu. 6]

35. Ijapokuwa sisi hatuwezi kuona viumbe wa kiroho, Neno la Yehova hutupa mitazamo mifupi ya tengenezo lake la kimbingu lisiloonekana na ya baadhi ya utendaji walo unaoathiri waabudu wake duniani. [uw-SW uku. 117 fu. 1]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki