Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumzwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa juma la Januari 4 hadi Aprili 19, 1999. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu kwa maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.
[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]
Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:
1. Sikuzote Yehova hakuongoza kiimla yale yaliyorekodiwa katika Biblia. (2 Tim. 3:16) [w97-SW 6/15 uku. 5 fu. 3]
2. Upatano wa familia na usitawi wa kiroho wa watoto wategemea wazazi kabisa. (Mit. 22:6) [fy-SW uku. 85 fu. 19]
3. Kwa kuwa dhambi ‘ilikuwa inaotea mlangoni,’ Kaini hangeweza kwa vyovyote kuepuka kufanya kosa zito. (Mwa. 4:7) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w94-SW 6/15 uku. 14 fu. 11.]
4. Tineja anapoendelea kukua, anapaswa kuruhusiwa moja kwa moja awe na uhuru zaidi katika uchaguzi wake wa tafrija. [fy-SW uku. 73 fu. 20]
5. Tamaa ya kumpendeza Muumba wetu huandaa kichocheo kizuri zaidi cha kusema kweli nyakati zote. (Mit. 6:17) [g97-SW 2/22 uku. 19 fu. 4]
6. Ili ‘maneno ya kinywa chetu na mawazo ya moyo wetu yapate kibali mbele za BWANA’ katika sala, twapaswa kujitahidi kuwa wenye ufasaha iwezekanavyo. (Zab. 19:14) [w97-SW 7/1 uku. 29 fu. 3-4]
7. Amri, hukumu, na sheria za Yehova zinazotajwa kwenye Mwanzo 26:5 hurejezea zile za agano la Sheria. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w92-SW 7/1 uku. 10 fu. 8.]
8. Yesu aliposema “imani yako imekufanya upone,” kama ilivyorekodiwa kwenye Luka 8:48, alimaanisha kwamba mwanamke aliyekuwa mgonjwa alihitaji kutangaza imani yake kwake akiwa Mesiya kabla ya kuponywa. [w97-SW 7/1 uku. 4 fu. 2-4]
9. Mwanzo 11:1 ni mojawapo ya maandiko ya Biblia ambayo hutumia usemi “nchi [“dunia,” NW]” kurejezea wanadamu kwa ujumla, au jamii ya binadamu. [g97-SW 1/8 uku. 27 fu. 3]
10. Hata ikiwa hakukuwa na mwelekeo wa kukubali upande wa Dina, bado alihusika kwa kupoteza ubikira wake. (Mwa. 34:1, 2) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w85-E 6/15 uku. 31 fu. 4.]
Jibu maswali yafuatayo:
11. Shetani alidokeza nini kupitia kule kusababu kunakopatikana kwenye Mwanzo 3:1-5? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 7/15 uku. 5 fu. 2.]
12. Kwenye Ufunuo 19:15, ni nini kinachowakilishwa na “upanga mrefu mkali” unaotoka kinywani mwa Yesu? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 5/15 uku. 4 fu. 4.]
13. Ni nini kinachokaziwa na uhakika wa kwamba Musa huandaa tarehe hususa kuhusiana na Furiko la siku ya Noa? [g97-SW 2/8 uku. 26 fu. 4]
14. Abrahamu ‘aliliitiaje jina la BWANA [“Yehova,” NW]’? (Mwa. 12:8) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 7/1 uku. 20 fu. 9.]
15. Katika muktadha, Yehova alimaanisha nini alipomwambia Paulo: “Fadhili yangu isiyostahiliwa yakutosha wewe”? (2 Kor. 12:9) [w97-SW 6/1 uku. 25 fu. 3]
16. Ni nini ambacho kwa wazi kilimchochea mke wa Loti aangalie nyuma, kikasababisha awe nguzo ya chumvi? (Mwa. 19:26) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w90-SW 4/15 uku. 18 fu. 10.]
17. Wakristo huonaje kununua bidhaa zilizoibwa? (Kut. 22:1; Yer. 17:11) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w92-SW 6/15 uku. 30 fu. 3, 9; uku. 31 fu. 5-6.]
18. Kulingana na Mwanzo 33:18, Yakobo alionyeshaje kwamba hakupendezwa na kushirikiana na Wakanaani? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w95-SW 9/15 uku. 21 fu. 5.]
19. Vitendo vya Yosefu vinavyofafanuliwa kwenye Mwanzo 37:13 vililinganaje na vya Yesu? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w87-SW 5/1 uku. 12 fu. 12.]
20. Tofauti kati ya Mungu na wanadamu ni nini, inapohusu kuonyesha hasira? [g97-SW 6/8 uku. 19 fu. 1-2]
Toa neno au fungu la maneno yanayohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:
21. Kuhesabia wengine nia _________________________ bila sababu _________________________ ni sawa na kuwahukumu. [w97-SW 5/15 uku. 26 fu. 5]
22. Uasilia wa kitabu cha Mwanzo waonyeshwa kwa _________________________ wake wa ndani, na pia _________________________ wake kamili pamoja na Maandiko yale mengine yaliyopuliziwa na Mungu. [si-SW uku. 14 fu. 8]
23. Kielelezo cha Rehoboamu na cha Eli chaweza kusaidia wazazi watambue matokeo ya kuwa _____________________ sana au _____________________ sana katika kulea mtoto. [fy-SW uku. 80-82 fu. 9-13]
24. Kutwaa _________________________ ni hatua ya maana katika kusitawisha _________________________ ya kimungu. [w97-SW 8/1 uku. 4 fu. 5]
25. Kuripoti kosa ni tendo la upendo wenye kanuni wa Kikristo unaoonyeshwa kuelekea _________________________ , kuelekea _________________________ , na kuelekea _________________________ . [w97-SW 8/15 uku. 30 fu. 2]
Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:
26. Nidhamu (kali, pole; ifaayo) ni uthibitisho wa upendo wa mzazi kwa mtoto wake. (Ebr. 12:6, 11) [fy-SW uku. 72 fu. 18]
27. Mwanzo 7:6, 11 hurejezea mwaka (2970; 2370; 2020) K.W.K., “gharika ya maji ilipokuwa juu ya nchi.” [Usomaji wa Biblia kila juma; ona si-SW uku. 294 chati.]
28. Kwenye Yohana 8:32, uhuru ambao Yesu alikuwa akisema ulikuwa uhuru kutoka (utawala wa Kiroma; ushirikina; dhambi na kifo). [w97-SW 2/1 uku. 5 fu. 1]
29. Katika utimizo wa mwisho wa Mwanzo 22:18, mbegu hurejezea (Isaka; Waisraeli; Yesu na wale 144,000). [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w98-SW 2/1 uku. 14 fu. 8.]
30. Ilikuwa ni (kutii Sheria ya Kimusa; kuona Mungu kuwa halisi na hofu inayofaa ya kutompendeza yeye; kuhofu adhabu) kulikomsaidia Yosefu akinze vishawishi vya ukosefu wa adili kwa mafanikio. (Mwa. 39:9) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w81-E 2/15 uku. 7 fu. 2.]
Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:
Mit. 5:3, 4; 15:22; 20:11; Efe. 5:19; 2 Tim. 3:16
31. Ni muhimu kwa wazazi kuhakikisha kwamba watoto wao wanaamini kwa moyo wote umaana wa kuishi maisha ya adili na yaliyo safi. [fy-SW uku. 67 fu. 8]
32. Mazungumzo ya siri kati ya wazazi na watoto wao matineja ni muhimu ili kuendeleza njia za mawasiliano. [fy-SW uku. 65 fu. 4]
33. Ufunguo wa kuboresha kuimba kwenye mikutano ya kutaniko ni kuwa na mtazamo wa moyo unaofaa. [w97-SW 2/1 uku. 27 fu. 3]
34. Kuwa na uelewevu wa mafundisho ya Neno la Mungu, Biblia, ni takwa la uhai udumuo milele. [w97-SW 8/15 uku. 6 fu. 5]
35. Ili kuepuka kishawishi cha ukosefu wa adili, lazima tutambue kwamba ni kosa na kwamba una matokeo yenye kuleta msiba na mabaya zaidi. [fy-SW uku. 93 fu. 9]