Enyi Wazazi Msipuuze Uvutano wa Televisheni kwa Watoto Wenu
1 Tunaweza kujiachilia tuwe na mtazamo wa kutazama vipindi vya televisheni visivyo na adili. Televisheni imekuwa mtunza-mtoto kwa wengi. Lakini mara nyingi wazazi hawachunguzi vipindi ambavyo watoto wao wanatazama, na jambo hilo huleta matatizo mengi. Watu fulani wamejiruhusu kutazama sana vipindi vya televisheni vya mfululizo vinavyoonyesha mambo ya kijamii au vipindi visivyoisha. Na wafanya-biashara wamefanya iwe rahisi kuwa na setilaiti za televisheni au kanda nyingi za video. Huenda hizo zikawa na matumizi muhimu, lakini watu wengi huzinunua ili waweze kujionea nyumbani mwao wenyewe vitumbuizo vyenye kushusha adili ambavyo ulimwengu huu hutamani. Naam, twaweza kufisidi akili na moyo wetu tukiwa tu nyumbani mwetu maadamu tuna vitu hivyo. Ijapokuwa “vitumbuizo” hivyo vimekuwa vya kawaida kwa watu wengi, inawabidi Wakristo wakumbuke shauri la Paulo la kufikiria ‘mambo yoyote ya uadilifu, yaliyo safi kiadili na ya kustahili sifa.’—Flp. 4:8; Ona Mnara wa Mlinzi, Januari 15, 1984, ukurasa wa 22, fungu la 17.
2 Maandiko yafuatayo yaliyozungumziwa kwenye kusanyiko la mzunguko lililopita yanahusianaje na habari hii?—Isa. 5:20; Zab. 97:10; Efe. 5:3-7; Gal. 5:19-21; 1 Kor. 15:33; Gal. 6:7, 8; na Mit. 27:12.