Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 8/02 kur. 5-6
  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2002
Huduma Yetu ya Ufalme—2002
km 8/02 kur. 5-6

Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Pitio la vitabu vikiwa vimefungwa kuhusu habari iliyozungumziwa katika migawo ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi kwa juma la Mei 6 hadi Agosti 19, 2002. Tumia karatasi tofauti ya kuandika majibu ya maswali mengi kadiri uwezavyo kwa wakati uliogawiwa.

[Taarifa: Wakati wa pitio la kuandika, ni Biblia pekee inayoweza kutumiwa kujibu swali lolote. Marejezo yanayofuata maswali ni kwa ajili ya utafiti wako wa kibinafsi. Nambari za ukurasa na fungu huenda zisipatikane katika marejezo yote kwenye Mnara wa Mlinzi.]

Jibu kila ya taarifa zifuatazo Kweli au Si Kweli:

1. Yeremia 18:1-6 huonyesha kwamba Yehova huwalazimisha watu wafanye mambo kinyume cha mapenzi yao. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w99-SW 4/1 uku. 22 fu. 3-4.]

2. Manabii wa uwongo waliiba matokeo ya kusikiliza maneno ya Mungu kwa kuwatia watu moyo wasikilize uwongo badala ya onyo la kweli kutoka kwa Mungu. (Yer. 23:30) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w92-SW 2/1 uku. 4 fu. 3.]

3. Kulingana na Yeremia 25:15, 16, “kikombe cha divai ya ghadhabu” ambacho chafanya “mataifa yote . . . kufanya wazimu” charejezea matokeo yenye kupumbaza akili ya dini ya uwongo. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w94-SW 3/1 uku. 20 fu. 13.]

4. Kulingana na vile unabii wa Yeremia ulivyotumiwa na Mathayo, “nchi ya adui” humaanisha nchi ya kifo, ambako watoto wachanga waliouawa na Herode Mkuu wangerudishwa kupitia ufufuo. (Yer. 31:15, 16; Mt. 2:17, 18) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w80-SW 1/1 uku. 6 fu. 13 au w79-E 6/15 uku. 19 fu. 13.]

5. Yeremia 37:21 hutuhakikishia kwamba Yehova anaweza kutegemeza watumishi wake waaminifu wakati wa hali ngumu za kiuchumi. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w97-SW 9/15 uku. 3 fu. 4–uku. 4 fu. 2.]

6. Kitabu cha Maombolezo chaonyesha huzuni kubwa juu ya uharibifu wa Yerusalemu mwaka wa 607 K.W.K., uliofanywa na Nebukadneza mfalme wa Babiloni. [si-SW uku. 130 fu. 1]

7. Maombolezo 5:7 huonyesha wazi kwamba Yehova huadhibu watoto moja kwa moja kwa sababu ya dhambi za wazazi wao. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 9/1 uku. 27 sanduku.]

8. Alama katika kipaji cha uso inayotajwa kwenye Ezekieli 9:4 humaanisha kwamba ujuzi peke yake utamwokoa mtu. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 9/15 uku. 14 fu. 18.]

9. “Zawadi [zikiwa] wanadamu” zinazotajwa kwenye Waefeso 4:8 ni wazee Wakristo, ambao wanawekwa na roho takatifu na kupewa mamlaka ya kushughulikia masilahi ya kiroho ya waamini wenzao. (Mdo. 20:28) [w00-SW 8/1 uku. 6 fu. 3]

10. Katika matumizi ya siku ya kisasa ya Ezekieli sura ya 23, Uprotestanti waweza kulinganishwa na Oholiba nao Ukatoliki kulinganishwa na dada yake mkubwa Ohola. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 9/15 uku. 21 fu. 22.]

Jibu maswali yafuatayo:

11. Ni manabii gani watatu waliokuwa wa kutokeza wakati wa ile miaka ya hatari kuanzia 617 K.W.K. hadi 607 K.W.K., ambayo ilikwisha wakati wa uharibifu wa Yerusalemu? [si-SW uku. 133 fu. 2]

12. Twaweza kuonyeshaje kwamba tunathamini kabisa dhabihu ya fidia ya Kristo kwa kuitikia mwaliko ulio kwenye Luka 9:23? [w00-SW 3/15 uku. 8 fu. 1]

13. Yehova ‘alimhadaa’ Yeremia kwa njia gani? (Yer. 20:7) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w89-SW 5/1 uku. 31 fu. 6.]

14. Yesu alimaanisha nini aliposema kwamba roho takatifu “itawafundisha nyinyi mambo yote na kuwakumbusha mambo yote niliyowaambia”? (Yn. 14:26) [w00-SW 4/1 uku. 8 fu. 7-8]

15. Kulingana na Yeremia 35:18, 19, kuna tumaini gani kwa jamii ya siku ya kisasa ya Warekabi? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona su-SW uku. 131 fu. 7.]

16. Wanefili walikuwa “watu hodari” na “watu wenye sifa” kwa njia gani? (Mwa. 6:4) [w00-SW 4/15 uku. 28 fu. 1]

17. Baruku alipotezaje usawaziko wake wa kiroho, na ni somo gani tunaloweza kujifunza kutokana na jambo hilo? (Yer. 45:1-5) [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w97-SW 8/15 uku. 21 fu. 14-16.]

18. Unabii kwenye Yeremia 50:38 ulitimia lini na jinsi gani? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona dp-SW uku. 150 fu. 2-3.]

19. Afa la Yerusalemu, “bikira binti Yuda,” lamaanisha nini kwa Jumuiya ya Wakristo kulingana na Maombolezo 1:15? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 9/1 uku. 27 sanduku.]

20. Ni nini maana ya usemi “Kiondoe kilemba, ivue taji,” kama ilivyoandikwa kwenye Ezekieli 21:26? [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 9/15 uku. 19 fu. 16.]

Andaa neno au maneno yanayohitajiwa kukamilisha kila moja ya taarifa zifuatazo:

21. Mtu mwenye kiasi havuki _________________________ ya _________________________ mzuri na hutambua kwamba kuna _________________________ ya mambo apaswayo kufanya na mambo awezayo kufanya. (Mika 6:8) [w00-SW 3/15 uku. 21 fu. 1-2]

22. Ijapokuwa huenda roho takatifu isiondoe _________________________ au _________________________ , inaweza kutusaidia _________________________. (1 Kor. 10:13; 2 Kor. 4:7) [w00-SW 4/1 uku. 11 fu. 6]

23. Kutokana na maandishi ya Yeremia, nabii Danieli alitambua kwamba ukiwa wa Yerusalemu ungechukua muda wa _________________________ ; usahihi wake wenye kustaajabisha huimarisha imani katika uwezo wa Yehova wa _________________________ . (Yer. 25:12; Dan. 9:2) [si-SW uku. 129 fu. 37]

24. Kitabu cha Maombolezo chapasa kuchochea _________________________ na _________________________ katika waabudu wa kweli na kuwa onyo la_________________________ kwa wale wasiomheshimu Yehova Mungu. [si-SW uku. 132 fu. 13]

25. Mfano wa Abrahamu wa kuachilia mambo ili kutatua kutoelewana unatuonyesha kwamba hatupaswi kuruhusu _________________________ au _________________________ kiharibu mahusiano ya amani na ndugu zetu. (Mwa. 13:5-12) [w00 8/15 uku. 24 fu. 3-4]

Chagua jibu sahihi katika kila moja ya taarifa zifuatazo:

26. Yobu alithamini (ujuzi; rehema; hukumu) ya Yehova na hivyo (akawatendea kwa ufahamu; akawarehemu; akawatendea haki) watumwa wake. (Ayu. 31:13, 14) [w00-SW 3/15 uku. 26 fu. 1]

27. Kwenye Yeremia 16:2-4, nabii huyo aliamriwa kubaki mseja (ili kutafakari kuhusu roho yake ya kujitolea; ili kufananisha kimbele kwamba Mesiya angekuwa mseja; ili kuonyesha kwamba neno la Yehova kuhusu kuangamizwa kwa Yerusalemu lingetimia bila shaka). [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w78-SW 8/1 uku. 21 fu. 4 au w78-E 4/15 uku. 31 fu. 2.]

28. Kwenye Mithali 4:7, hekima humaanisha (kufahamu mambo ya hakika; kuona jinsi mambo yanavyohusiana; kutumia ujuzi na uelewevu). [w00-SW 5/15 uku. 21 fu. 1]

29. Hakuna binadamu leo awezaye kuwa na uhakika jinsi ambavyo jina la Mungu lilivyotamkwa hapo awali katika Kiebrania kwa sababu hapo awali Kiebrania cha Kibiblia kiliandikwa kwa (vokali tu; konsonanti tu). [rs-SW uku. 424 fu. 1]

30. Gari la vita la Mungu katika Ezekieli sura ya 1 lawakilisha (Ufalme wa Mungu wa Kimesiya; tengenezo la Yehova la malaika walio roho; mawasiliano kati ya Yehova na mabaki). [Usomaji wa Biblia kila juma; ona w88-SW 9/15 uku. 11 fu. 5.]

Patanisha maandiko yafuatayo na taarifa zilizoorodheshwa chini:

Kum. 7:25, 26; Mit. 4:18; 5:21; Yer. 46:28; Rom. 15:4

31. Amri hii yaonyesha jinsi ambavyo watu wa Yehova wanapaswa kuona mifano yoyote ya ibada ambayo huenda waliiheshimu sana hapo zamani. [rs-SW uku. 199 fu. 4]

32. Njia moja hususa ambayo Yehova hutufariji ni kupitia Neno lake lililoandikwa ambalo lina tumaini zuri ajabu la wakati ujao. [w00-SW 4/15 uku. 5 fu. 4]

33. Nidhamu ya wazazi haipaswi kupita kiasi kinachofaa wala kuzidi kusudi lake la kusahihisha makosa na kufundisha. [Usomaji wa Biblia kila juma; ona kl-SW uku. 148 fu. 20.]

34. Kwa kuwa Yehova huwawezesha watumishi wake kuelewa kusudi lake hatua kwa hatua, mara nyingi mtu huhitajika kubadili kufikiri kwake kadiri ujuzi wake unavyoongezeka. [rs-SW uku. 185 fu. 2]

35. Tendo lolote lisilo safi kiadili, hata liwe la siri jinsi gani, halijafichika machoni pa Mungu. [w00-SW 7/15 uku. 31 fu. 3]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki