Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/04 uku. 5
  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2004
Huduma Yetu ya Ufalme—2004
km 12/04 uku. 5

Pitio La Shule Ya Huduma Ya Kitheokrasi

Maswali yafuatayo yatashughulikiwa kwa njia ya maswali na majibu katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi juma linaloanzia Desemba 27, 2004. Mwangalizi wa shule ataongoza pitio la dakika 30 linalotegemea habari zilizozungumziwa kwenye hotuba ambazo zilitolewa kuanzia juma la Novemba 1 hadi Desemba 27, 2004. [Taarifa: Mahali ambapo vitabu vya marejeo havijatajwa baada ya swali, utahitaji kufanya utafiti wako mwenyewe ili kupata majibu.—Ona Shule ya Huduma, uku. 36-37.]

SIFA ZA USEMI

1. Taja mojawapo ya njia bora zaidi za kuwafanya wasikilizaji wapendezwe na habari unayozungumzia. [be uku. 218 fu. 3]

2. Taja mambo matano yanayoonyesha umalizio mzuri. [be uku. 221 fu. 1-5]

3. Tunawezaje kuhakikisha kwamba mambo tunayosema ni sahihi? [be uku. 224 sanduku]

4. Tunaweza kuhakikishaje kwamba hotuba tunazotoa mikutanoni zinaonyesha tunaheshimu sana kutaniko likiwa “nguzo na tegemezo la ile kweli”? (1 Tim. 3:15) [be uku. 224 fu. 1-4]

5. Andiko la Methali 14:15 linaweza kutusaidiaje tunapotumia matukio ya hivi karibuni, mambo yaliyonukuliwa, na mambo yaliyoonwa? [be uku. 225 fu. 1]

HOTUBA NA. 1

6. Kipindi cha kutoka Furiko kurudi nyuma mpaka kuumbwa kwa Adamu kinaweza kuhesabiwaje? [si uku. 286 fu. 12]

7. Tunawezaje kujua tarehe ambayo Yesu alianza huduma yake, na kuna msingi gani wa kuamini kwamba huduma hiyo ilichukua miaka mitatu na nusu tu? [si uku. 287 fu. 16]

8. (a) “Lile neno la kurudisha na kujenga upya Yerusalemu” lilitolewa lini? (b) Ni miaka mingapi ingepita tangu kutolewa kwa tangazo hilo hadi kuja kwa Yesu akiwa Masihi? (Dan. 9:24-27) [si uku. 291 fu. 18-19]

9. Kuomba msamaha kwa unyofu ili ‘tufanye amani pamoja na ndugu yetu’ kunatia ndani nini? (Mt. 5:23, 24) [w02 11/1 uku. 6 fu. 1, 5]

10. Andiko la 2 Wafalme 13:18, 19 linatufunza nini kuhusu kutimiza kazi ambayo Mungu ametupatia? [w02 12/1 uku. 31 fu. 1-2]

USOMAJI WA BIBLIA WA KILA JUMA

11. Kwa nini Waisraeli wangeweza kumpa mkaaji mgeni au kumuuzia mgeni mnyama mfu ambaye hajatolewa damu na ambaye wao wenyewe hawangeweza kumla? (Kum. 14:21)

12. Andiko la Kumbukumbu la Torati 20:5-7 linatufunza nini?

13. Kwa nini kutwaa “kuwa rehani jiwe la kusagia la mkononi au jiwe lake la juu la kusagia” kulilinganishwa na kutwaa “nafsi”? (Kum. 24:6)

14. Kwa kuwa Waisraeli walikatazwa kula mafuta yoyote, kula “mafuta ya kondoo-dume” kunamaanisha nini? (Kum. 32:13, 14)

15. Kuna ulinganifu gani wa kisasa wa dhambi ya Akani? (Yos. 7:1-26) [w86 12/15 uku. 20 fu. 20]

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki