HAZINA ZA NENO LA MUNGU | YEREMIA 12-16
Waisraeli Walimsahau Yehova
Yeremia alipewa mgawo mgumu ambao ungeonyesha jinsi Yehova alivyoazimia kuangamiza Yuda na Yerusalemu yenye kiburi.
Yeremia alinunua mshipi wa kitani
Mshipi uliofungwa kiunoni uliwakilisha uhusiano wa karibu kati ya Yehova na taifa hilo
Yeremia aliupeleka mshipi huo kwenye Mto Efrati
Aliuficha kwenye mpasuko wa mwamba kisha akarudi Yerusalemu
Yeremia alirudi kwenye Mto Efrati kuuchukua mshipi
Mshipi ulikuwa umeharibika
Baada ya Yeremia kutekeleza mgawo wake ndipo Yehova alimweleza kilichomaanishwa na mfano huo
Utii wa Yeremia wa kutoka moyoni katika jambo ambalo lilionekana kuwa dogo ulitimiza fungu muhimu katika jitihada za Yehova za kufikia mioyo ya watu wake