Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yb14 uku. 120
  • Beji Zilikuwa “Pasipoti” Zao

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Beji Zilikuwa “Pasipoti” Zao
  • 2014 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
2014 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehovah
yb14 uku. 120

SIERRA LEONE NA GUINEA

Beji Zilikuwa “Pasipoti” Zao

“MNAMO 1987, zaidi ya wajumbe 1,000 walihudhuria Kusanyiko la Wilaya lenye kichwa ‘Tumaini Katika Yehova’ lililofanywa mjini Guéké­dou, nchini Guinea. Kwa kuwa mahali pa kufanyia kusanyiko palikuwa karibu na mpaka wa Sierra Leone na Liberia, wajumbe wengi kutoka nchi hizo waliamua kusafiri kila siku wakitokea nyumbani kwenda kusanyikoni. Hata hivyo, hawakuwa na hati za kusafiria zilizohitajiwa. Kwa hiyo, ndugu waliosimamia safari hiyo walijadiliana na wenye mamlaka waliokuwa mpakani na kukubaliana jambo moja. Wajumbe wangehitaji hati moja tu​—beji zao za kusanyiko! Polisi wa mpakani walipoona beji za rangi ya machungwa, mara moja waliwapungia mkono wajumbe ili kuashiria kwamba wanaweza kuvuka mpaka.”​—Anaeleza Everett Berry, aliyetumikia akiwa mmishonari.

Picha katika ukurasa wa 120

Ndugu wakifurahia mlo katika kusanyiko la wilaya

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki