Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • yb16 uku. 82-uku. 85 fu. 5
  • Maelezo Mafupi Kuhusu Indonesia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maelezo Mafupi Kuhusu Indonesia
  • 2016 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
2016 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
yb16 uku. 82-uku. 85 fu. 5

INDONESIA

Maelezo Mafupi Kuhusu Indonesia

Nchi Indonesia ni kisiwa kikubwa zaidi duniani kilicho katikati ya bara la Asia na Australia na kinapitiwa na mstari wa ikweta. Zaidi ya visiwa 17,500 vinavyofanyiza kisiwa hiki vimezungukwa na milima na misitu ya kitropiki. Indonesia ina milima zaidi ya 100 yenye volkano hai, na ndilo eneo lenye milipuko mingi ya volkano duniani.

Mwanamke wa Mwindonesia pambo la asili la kichwani

Watu Indonesia ni nchi ya nne yenye idadi kubwa ya watu duniani (baada ya China, India na Marekani) na kuna makabila zaidi ya 300. Kabila la Wajava na Wasunda hufanyiza zaidi ya nusu ya idadi ya watu nchini humo.

Dini Asilimia 90 hivi ya Waindonesia ni Waislamu. Asilimia zinazobaki ni Wahindi, Wabudha, na Wakristo wachache. Pia, watu wengi hufuata desturi za dini za kienyeji.

Lugha Kuna zaidi ya lugha 700 ambazo huzungumzwa katika kisiwa hicho. Lugha ya taifa ni Kiindonesia ambacho kinatokana na Kimalay. Watu wengi pia huzungumza lugha za kienyeji nyumbani.

Mishikaki

Kazi Watu wengi ni wakulima wadogo-wadogo au wachuuzi. Nchi hii pia ina migodi mingi, mbao, mafuta, na gesi na huuza kwa wingi mpira na mafuta ya mawese.

Chakula Chakula kikuu ni wali. Vyakula vya kawaida ni nasi goréng (wali wa kukaangwa na mayai yaliyochanganywa na mboga), satay (mishikaki), na gado-gado (kachumbari na mchuzi wa njugu-karanga).

Hali ya hewa Joto kali na unyevu. Kuna misimu ya mvua na kiangazi. Ni kawaida pia kusikia ngurumo za mvua.

UKUBWA WA NCHI (Kilometa za mraba)

737,815

IDADI YA WATU

256,000,000

IDADI YA WAHUBIRI MWAKA 2015

26,246

UWIANO, MHUBIRI MMOJA KWA

9,754

HUDHURIO LA UKUMBUSHO MWAKA 2015

55,864

Ramani ya Indonesia
    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki