Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w74 7/15 kur. 324-333
  • Haraka Inayokupasa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Haraka Inayokupasa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
  • Vichwa vidogo
  • Ukubali Msaada Sasa
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1974
w74 7/15 kur. 324-333

Haraka Inayokupasa

JE! TUMAINI la usimamizi mpya wa mambo ya dunia linakuvuta? Je! unaona ni faraja kuiona dunia isiyo na vita, dini ya uongo, ufisadi, magonjwa na kifo? Au yote yaonekana kama ndoto?

Kwa kweli, ujumbe juu ya kusudi la Mungu la taratibu mpya yenye haki si ndoto. Yehova Mungu hasemi uongo wala kudanganya. (Ebr. 6:18) Yeye haahidi kitu ambacho hatakileta. Naye anapowafanya watumishi wake waeneze onyo sasa ulimwenguni pote, zaidi katika yanayoitwa mataifa ya “Kikristo,” twaweza kuhakikisha anamaanisha anachosema.

Vile vile twaweza kuhakikisha kwamba Mungu asemapo ataiangamiza dini ya ulimwengu na kuiacha dini yake ya kweli, vile vile anamaanisha anachokisema. Si shauri la kama hilo litatukia. Litatukia, bila ya kushindwa. Ulizo ni, Wewe utafanya nini juu yake?

Kwanza, unapoona kwamba dini ya ulimwengu ina hatia ya kumwakilisha Mungu vibaya na kuwapotosha watu, je! imekupasa ufanye nini? Imekupasa ufanye neno la Mungu linavyosema ufanye. Nini? Utoke ndani yake mbele ya kuja kwa kuanguka kwake kwa ghafula! Yesu alipowaita wanadini wataalamu wa siku zake “viongozi vipofu,” aliwaambia watu wa vivi hivi: “Waacheni.”​—Mt. 15:14.

Ndiyo, achana nao! Jiepushe nao! Dini ya ulimwengu ni chafu na yenye hatia ya damu machoni pa Mungu. Kwa hiyo onyo kali la mtume lazima litiiwe na wale wanaotaka kuendelea kuishi:

“Pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? . . . Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? . . . Kwa hiyo, tokeni kati yao, mkatengwe nao, asema [Yehova], msiguse kitu kilicho kichafu, nami nitawakaribisha. Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike, asema [Yehova] Mwenyezi.”​—2 Kor. 6:14-18.

Ikiwa kanisa lako ni sehemu ya dini ya ulimwengu, kimbia sasa! Ikiwa unamjua kiongozi wa dini unayeona ni mtu mzuri, hata naye amepaswa akimbie!

Haya ni maneno mazito, lakini ni ya kweli. Ndivyo Mungu alivyokusudia. Bila shaka, wakati wa dini ya ulimwengu unakwisha kwa kasi. Mwisho wake hauko mbali sana. Kwa hiyo imekupasa ufanye tendo la haraka sasa.

Ukubali Msaada Sasa

Ijapokuwa kuikimbia dini ya ulimwengu ni hatua ya kwanza ya lazima, hata hivyo hakutoshi. Hata wasioamini kuwako kwa Mungu wamefanya hivyo. Kunayo vile vile hatua nyingine ya lazima. Ni lazima kila mtu anayetaka uzima katika taratibu mpya ya Mungu amjue Mungu kusudi aupate ulinzi na kuuokoka mwisho wa hii taratibu.​—Yohana 17:3.

Wawezaje kumjua Mungu kwa kweli na anayokutaka ufanye? Ni kwa kujifunza Neno lake wewe mwenyewe, Biblia. Ili ufanye hivyo unahitaji msaada.

Nini njia kubwa ambayo wanafunzi wa kwanza waliitumia kuwaongoza watu kwenye kweli juu ya Mungu? Waliwafundisha watu kwa faragha, mara nyingi wakienda nyumbani kwa watu wenye kupendezwa. Humo, katika nyumba zao wenyewe, watu walijifunza ambayo Biblia iliyasema kwa kweli. Ndivyo ilivyo na leo. Mashahidi wa Yehova wanaendesha mpango wa miezi sita wa bure wa kuzitembelea nyumba kwa ajili ya wanaotaka kumjua Mungu kweli kweli. Kwa njia hii mamilioni ya watu yamepokea mafundisho ya Biblia.​—Matendo 20:20.

Ni kweli, nyakati nyingine watu hawa wanapingwa. Huenda wakafanyiwa hivyo na watu wasiojua sawasawa, marafiki au jamaa. Lakini mara nyingi, kwa kuwa wenye busara na wavumilivu, wanaweza kuwasaidia wale wanaotaka kabisa kujifunza njia inayoongoza kwenye uzima katika taratibu mpya ya Mungu.

Je! wewe umejipatia elimu ya bure ya Biblia inayotolewa na mashahidi wa Yehova? Kama sivyo, twakusihi ufanye hivyo sasa. Usiwe kati ya wale walio kama wakwe za Lutu. Wakati mji usiomheshimu Mungu wa Sodoma ulipokuwa karibu ya kuharibiwa na tendo la Mungu, Lutu aliwaonya. Lakini Biblia inasema, “Akawa kama achezaye machoni pa wakweze.” (Mwa. 19:14) Lakini haukuwa mchezo. Asubuhi yake Sodoma uliharibiwa kabisa. Ndivyo na wakwe za Lutu.

Je! wewe waupenda uzima? Je! wataka kuendelea kuishi? Basi fanya haraka ufanye linavyosema Neno la Mungu: “Mtafuteni [Yehova], enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, . . . Itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya [Yehova].”​—Sef. 2:3.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki