Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 6/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1991
  • Habari Zinazolingana
  • Glakoma Ugonjwa Unaosababisha Upofu
    Amkeni!—2004
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2004
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2000
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 6/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Mikusanyiko ya Poland Familia yangu nami tulipata pendeleo la kuhudhuria mikusanyiko hiyo [ya Mashahidi wa Yehova]. (Juni 8, 1990) Kuchangamana bila kizuizi na ndugu kutoka Soviet Union na Chekoslovakia, ambao wengi wao walikuwa wamesafiri kwa kujidhabihu sana, kulisisimua. Kuona ndugu Warusi na Waamerika wakikumbatiana kulikuwa ni ushuhuda ulio kimya juu ya mahali ambapo roho ya Mungu inatenda kazi leo.

I.L., Jamhuri ya Muungano wa Ujerumani

Bunduki Nimeudhiwa na maelezo yaliyopotoka juu ya bunduki katika toleo la Mei, 8, 1991. Maelezo hayo ya kuangalia upande mmoja, yanayoeleza upande mbaya wa vitu visivyo na uhai si ya akili. Bunduki kwa asili si nzuri au mbaya; wala kule kuzifanyiza, kuziuza, au kuwa nazo.

J.P., United States

Mjomba wangu alipoteza mke wake katika msiba wa motokaa na akatumia miezi mitatu akinywa kupindukia. Hatimaye alijifungia katika bafu na kujipiga risasi. Natumaini kwamba watu wanaosoma makala hii watatua na kufikiri juu ya kama inastahili kuwa na bunduki.

M.C.A., Brazil

Ingawa lazima nikiri kwamba sikuzote nimekuwa nikitaka bunduki, niliposoma kurasa zile, zilinifanya niulize kama bado nastahili kuendelea kuweka akiba ili ninunue moja.

D.M., Uingereza

Utafiti wa Kutumia Wanyama Twakaribisha uhakika wa kwamba Mashahidi wa Yehova hutoa maelezo juu ya habari ya utafiti wa wanyama. (Amkeni! Aprili 8, 1991; Awake! Julai 8, 1990) Twaonelea ni jambo la lazima kusahihisha taarifa hii: “Mwelekeo duniani pote ni kuunga mkono vile vyama vyenye kutumia nguvu kutetea haki za wanyama.” Wanaotumia nguvu ni wachache na hupata umaarufu tu kupitia vyombo vya habari.

I.L., Shirika la Muungano wa Haki za Wanyama,

Jamhuri ya Muungano wa Ujerumani

Tulisema kwamba “baadhi”—wala si wote—ya wateteaji wa haki za wanyama “wako tayari kutumia jeuri.” Taarifa hiyo ilitolewa na Mkanada aliye mteteaji wa wanyama ambaye ni mashuhuri. Sisi tuliiripoti tu.—MHARIRI.

Nilista kusoma toleo juu ya utafiti wa wanyama (Aprili 8, 1990) kwa sababu mimi nilijua hiyo ni habari yenye kutokeza mchanganyiko wa maono ya moyoni. Lakini nyinyi mliishughulikia kwa njia ya busara na ya usawaziko.

N.V., United States

Kwa kuwa utafiti ndiyo kazi yangu ya maisha, nilikuwa na hamu nyingi kusoma ambayo Amkeni! lingesema. Ni wazi kwamba Biblia hailaani utafiti wa wanyama, hata hivyo haitetei ukatili unaotendwa wanyama. Ikiwa kazi yangu itataka utumizi wa wanyama wakati ujao, nitakuwa mwangalifu nisiwatumie vibaya wala kuwa mkatili kwao.

O.O., United States

Makala yenu ilionekana ni kama ilipendelea utafiti wa wanyama iwapo hauhusishi mteseko mwingi. Ni lenye thamani gani wakati jambo linatimizwa kupitia mteseko na kifo cha wanyama wasio na hatia?

M.B., United States

Utafiti wa wanyama ni suala lenye kujawa na mchanganyiko wa maono ya moyoni, na makala zetu zilitokeza kutoka kwa wasomaji majibu mengi isivyo kawaida. Biblia hailaani kwa ujumla matumizi ya wanyama ili kufaidi wanadamu. Lakini, yaeleweka, wengi huchukizwa na mteseko wa aina yoyote kwa wanyama, na hakika sisi twastahi hisia zao katika hilo.—MHARIRI.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki