Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 7/8 kur. 14-15
  • Umajimaji Ulio wa Thamani Kubwa Zaidi Ulimwenguni

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Umajimaji Ulio wa Thamani Kubwa Zaidi Ulimwenguni
  • Amkeni!—1991
  • Habari Zinazolingana
  • Thamani Halisi ya Damu
    Amkeni!—2006
  • Chembe Nyekundu za Damu Zenye Kustaajabisha
    Amkeni!—2006
  • “Lori” Ndogo za Mwili Wako
    Amkeni!—2001
  • Kuokoa Uhai kwa Damu—Jinsi Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 7/8 kur. 14-15

Umajimaji Ulio wa Thamani Kubwa Zaidi Ulimwenguni

TONE moja la damu ni rahisi sana kuchukuliwa hivi hivi. Hilo hukusanyana kutokana na mkwaruzo au mdungo wa pini, likiwa kiviringo kidogo sana cha wekundu unaometameta, nasi huliosha au kulipangusa bila kufikiri.

Lakini kama tungeweza kujifinya tuwe wadogo sana mpaka kiviringo hicho kiwe kikubwa sana juu yetu kama mlima, tungepata katika vina vyacho vyekundu ulimwengu wenye utatanishi na utaratibu wa ajabu. Ndani ya tone moja hilo, yapita majeshi makubwa ya chembe yakiwa na pirikapirika nyingi: chembe nyekundu 250,000,000, chembe nyeupe 400,000 za damu, na visahani 15,000,000, ambavyo ni sehemu tu ya wanajeshi wa kawaida waliomo. Lianzishwapo likafanye kitendo katika mkondo wa damu, kila jeshi huanza kazi yalo tofauti.

Chembe nyekundu hupita mbio katika ule mtataniko wa mfumo wa mishipa, zikibeba oksijeni kutoka kwenye mapafu kuipeleka kwenye kila chembe mwilini na kuondoa kaboni dayoksaidi. Chembe hizo ni ndogo sana hivi kwamba fungu moja la 500 la hizo lingekuwa na urefu wa kwenda juu wa sentimeta 0.1 tu. Hata hivyo, fungu moja la chembe nyekundu zote katika mwili wako zingepanda juu kufikia kilometa 50,000! Baada ya karibu siku 120 za kufunga safari ya kupita mwilini mara 1,440 kwa siku, ile chembe nyekundu huachishwa kazi. Kiini chayo chenye chuma kingi hurekebishwa upya vya kutosha, na sehemu nyinginezo kuharibiwa. Kila nukta, chembe nyekundu milioni tatu huondolewa, huku idadi hiyo hiyo ya zilizo mpya zikifanyizwa katika uloto (mafuta mekundu ya mifupa). Mwili hujuaje kwamba chembe nyekundu imefikia umri ufaao wa kuacha kazi? Wanasayansi wanapigwa fumbo. Lakini bila mfumo huu wa kuweka chembe nyinginezo mahali pa chembe nyekundu zilizozeeka, kulingana na mwanakemia mmoja, “damu yetu ingekuwa nzito kama zege katika muda wa majuma kadhaa.”

Kwa sasa, chembe nyeupe hunyemelea-nyemelea katika ule mfumo, zikitafuta na kuharibu wavamizi wasiotakwa. Visahani hukusanyika mara hiyo mahali penye mkato na kuanza utaratibu wa kugandamanisha na kufunika palipopasuka. Chembe zote hizo huning’inizwa katika umajimaji mwangavu, wenye rangi ya pembe uitwao plasma, huo wenyewe ukiwa ni mjumliko wa mamia ya vijumlishio mbalimbali, vingi vyavyo vikitimiza sehemu za muhimu katika kutekeleza kazi nyingi sana za damu.

Wanasayansi wakiwa na ujumla wa uwezo wa mabongo yao hushindwa kuelewa kila jambo ambalo damu hufanya, achia mbali kuinakili. Je! umajimaji huu wa kimwujiza uliotatanika ungeweza kuwa chochote kile ila kazi ya Mbuni Stadi? Na je, yafaa kusababu kwamba Muumba huyu mwenye nguvu kuliko binadamu ana kila haki ya kuamrisha jinsi vitu vyake alivyoviumba vyapasa kutumiwa?

Mashahidi wa Yehova wamefikiri hivyo sikuzote. Wao huiona Biblia kuwa barua kutoka kwa Muumba wetu ambayo ina miongozo juu ya jinsi ya kuishi maisha bora yawezekanayo; ni kitabu kisichonyamaza juu ya jambo hili la damu. Walawi 17:14, NW, husema hivi: “Nafsi ya kila aina ya mwili ni damu yake”—bila shaka, si kwa uhalisi, kwa kuwa Biblia husema pia kwamba kiumbe hai chenyewe ni nafsi. Bali, uhai wa nafsi zote umeunganika sana na damu na kuendelezwa nayo hivi kwamba kwa kufaa damu huonwa kuwa umajimaji mtakatifu unaowakilisha uhai.

Kwa watu fulani, hilo ni jambo gumu kueleweka. Twaishi katika ulimwengu ambao huona vitu vichache sana kuwa vitakatifu. Ni mara haba ambapo uhai wenyewe huthaminiwa jinsi upasavyo. Basi, si ajabu sana kwamba damu hununuliwa na kuuzwa kama bidhaa nyingine yoyote. Lakini wale waheshimuo matakwa ya Muumba hawauchukui jinsi hiyo. ‘Msile damu’ ilikuwa ndiyo amri ya Mungu kwa Noa na wazao wake—ainabinadamu yote. (Mwanzo 9:4) Karne nane baadaye Yeye alitia amri hiyo katika Sheria yake kwa Waisraeli. Karne kumi na tano baadaye aliikazia tena kwa kundi la Kikristo: ‘Jiepusheni na damu.’—Matendo 15:20.

Mashahidi wa Yehova hushikilia sheria hiyo kwa sababu hasa wao wataka kutii Muumba wao. Kwa njia ya kifo cha dhabihu cha Mwana wake mwenyewe mpendwa, tayari Muumba ameandalia ainabinadamu damu yenye kuokoa uhai. Yaweza kurefusha maisha si kwa miezi au miaka michache tu bali milele.—Yohana 3:16; Waefeso 1:7.

Zaidi ya hilo, kujiepusha na kutiwa damu mishipani kumelinda Mashahidi na maelfu ya hatari. Watu wengi zaidi na zaidi mbali ya Mashahidi wa Yehova wanakataa kutiwa damu mishipani leo. Pole kwa pole jumuiya ya kitiba inaitikia na kupunguza utumizi wayo wa damu. Kama vile Surgery Annual lilivyoweka wazo hilo: “Kwa wazi, mtio wa damu mishipani ulio salama kabisa ni ule ambao haujatiwa.” Jarida Pathologist lilisema kwamba Mashahidi wa Yehova wamesisitiza kwa muda mrefu kwamba kutiwa damu mishipani si matibabu yenye kushaurika. Liliongezea hivi: “Kuna ushuhuda mwingi wa kuunga mkono ushindani wao, kujapokuwa na mateto kutoka wanabenki wa damu kwamba sivyo ilivyo.”

Wewe ungeona ni afadhali kutumaini nani? Yule Mwenye hekima aliyebuni damu? Au watu wale ambao wamefanya kuuza damu kukawa biashara kubwa?

(Blurb katika ukurasa wa 14)

Hata ikiwa kutia damu mishipani kungeweza kuachiliwa mbali kuwa ni bidhaa hatari zisizo za lazima za biashara ambayo mara nyingi ni yenye pupa, bado hiyo haingeeleza kwa nini Mashahidi wa Yehova hukukataa. Sababu zao ni tofauti kabisa na za maana zaidi. Hizo ni nini?

[Picha katika ukurasa wa 15]

Mfumo wa mishipa ya kibinadamu, ukiwa na kapilari (katika mchoro wa ndani) zilizo nyembamba sana hivi kwamba chembe za damu hulazimishwa kusafiri kupita ndani yazo kwa mfuatano wa moja moja

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki