Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 2/8 kur. 14-15
  • Mchanganyiko Hatari

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mchanganyiko Hatari
  • Amkeni!—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Majaribio ya Kuzuia Mwendo Huo
  • Idadi ya Vifo Yaendelea Kupanda
  • Aksidenti za Magari Je, U Salama?
    Amkeni!—2002
  • Makosa ni ya Nani?
    Amkeni!—1992
  • Jinsi ya Kuzuia Aksidenti za Barabarani
    Amkeni!—2011
  • Jinsi ya Kupambana na Msongamano wa Magari
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 2/8 kur. 14-15

Mchanganyiko Hatari

“TATIZO kubwa,” akatangaza rais Bush wa U.S. “Hali mbaya mno ya mambo,” likasema gazeti The Star la Afrika Kusini. “Ugonjwa wa kipuku,” likasema gazeti U.S. News & World Report. “Pigo kwa jamii,” akasema mwananchi mmoja mwenye kuhangaikia hali.

Je! hawa wanazungumzia vairasi hatari yenye kuogopwa sana ya UKIMWI? La, lakini ni juu ya aina nyingine ya pigo ambalo kwa sasa linaua watu wengi kuliko UKIMWI katika nchi nyingi. Ni nini hilo? Matokeo ya mchanganyiko hatari: unywaji na uendeshaji gari.

Ulimwenguni pote, karibu watu 300,000 huuawa kila mwaka katika aksidenti za magari. Kati ya mamilioni ambao hujeruhiwa, makumi ya maelfu hulemazwa maisha yote. Gharama ya fedha ni maelfu ya mamilioni mengi ya dola kila mwaka. Aksidenti zinazosababishwa na kileo huchukua sehemu kubwa ya kadirio hilo.

Katika mwongo ulioishia mwaka wa 1990, watu wapatao 100,000 walikufa kutokana na UKIMWI katika United States. Lakini katika miaka hiyo hiyo kumi, watu karibu 250,000 wameuawa katika aksidenti zinazosababishwa na kileo. Mara nyingi UKIMWI huathiri kwa njia ya moja kwa moja wale wapotovu kingono na watumiaji wa dawa za kulevya kwa kujidunga sindano. Lakini dereva mlevi aweza kuua si mwenye kuitumia vibaya tu bali pia mpita njia asiye na hatia.

Kuchanganya unywaji na uendeshaji gari mara nyingi husababisha kifo cha jeuri sana kwa wale wasiokitazamia, na hutenganisha familia nyingi. Wazazi hufiwa na watoto wao, watoto na wazazi wao, na waume na wake wenzi wao.

Majaribio ya Kuzuia Mwendo Huo

Jitihada nyingi zinafanywa ili kuzuia mwendo huo wa uharibifu. Katika United States, kampeni za kuelewesha umma zimekwisha anzishwa na mashirika madogo kama vile RID (“Remove Intoxicated Drivers” au Ondoa Madereva Wapumbaa-Pombe) na MADD (“Mothers Against Drunk Drivers” au Akina Mama Wanaopinga Madereva Waliolewa). Kuna programu kama vile “Stop-DWI” (“Driving While Intoxicated” au Koma-Kuendesha Gari Ukiwa Umepumbaa kwa Pombe). Mashirika kama hayo yamo katika nchi nyinginezo nyingi. Mashirika hayo husaidia wenye kupatwa na msiba na haki zao na kuendeleza marekebisho ya sheria.

Mashirika ya kulinda sheria yanaongeza jitihada za kukamata madereva waliodhoofishwa, yakitumia njia mbalimbali kama vile vituo vya barabarani vya kutambua kama dereva amepumbaa akili. Sheria kadhaa zimepitishwa ili kufanya wale wanaouza vileo waweze kushtakiwa. Na hata vibao huwekwa kando za njia kukumbusha madereva sheria zilizopo.

Idadi ya Vifo Yaendelea Kupanda

Kujapokuwa jitihada zote hizo, vifo vinavyosababishwa na uendeshaji wa waliolewa vyaendelea kupanda ulimwenguni pote. Katika Brazili mtu mmoja huuawa kila dakika 21—vifo 25,000 kila mwaka—katika aksidenti zinazosababishwa na kileo. Hiyo ni karibu asilimia 50 ya vifo vyote vya barabarani huko. Katika Uingereza na Ujerumani, karibu sehemu moja kwa tano ya vifo vyote vya barabarani husemwa kuwa vimesababishwa na kileo. Katika Meksiko, kulingana na vyanzo vingi vya habari, asilimia 80 ya vifo vya barabarani 50,000 husababishwa na ‘makosa ya kibinadamu, yaletwayo sana sana na waendeshaji gari waliopumbazwa akili kwa pombe,’ laripoti El Universal la Jiji la Meksiko.

Inakadiriwa kwamba zaidi ya asilimia 25 ya vifo vya barabarani katika Afrika Kusini huhusisha kileo. Katika United States kwa mwaka wa wastani, aksidenti zinazosababishwa na kileo hutokeza kujeruhiwa kwa watu 650,000, huku 40,000 kati yao wakiwa mahututi; watu zaidi ya 23,000 wanauawa—hiyo ikiwa ni karibu nusu ya vifo vyote vya barabarani.

Kwa sababu ya mahangaiko ya kujaribu kukomesha dereva anayeendesha akiwa amedhoofishwa na pombe, Halmashauri ya Wenye Kupatwa na Msiba na Madereva Wapumbaa-Pombe [DWI] ilianzishwa katika Jimbo la Washington, U.S.A. Halmashauri hiyo imekuwa sehemu ya kuhukumu kisheria wale wanaoshtakiwa kuendesha wakiwa wamepumbaa kwa pombe. Programu hiyo sasa inatumiwa katika sehemu nyingi za nchi hiyo. Kusudi la programu hiyo ni kuleta wenye makosa uso kwa uso na matokeo ya msiba ya unywaji wao usioangaliwa. Wenye hatia huamuriwa na mahakama kusikiliza waliopatwa na msiba pamoja na washiriki wa familia yao na kujulishwa msiba mkubwa ambao umesababishwa. Amkeni! lilialikwa litazame kwa ukaribu zaidi jinsi jambo hilo hufanywa.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 15]

Dominic D. Massita, Sr./Accident Legal Photo Service of New York

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki