Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 11/8 kur. 24-26
  • Je! Wewe Unachukia Kupokea Uchambuzi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Wewe Unachukia Kupokea Uchambuzi?
  • Amkeni!—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • 1. Kubali Uchambuzi
  • 2. Dhibiti Mchambuzi Wako Aliye Mkali Zaidi
  • 3. Uliza Mambo Madogo-madogo
  • 4. Umtulize Mchambuzi Wako
  • 5. Kazia Yaliyomo Katika Uchambuzi, Si Jinsi Yanavyotolewa
  • 6. Punguza Ukali wa Uchambuzi
  • Waweza Kukabiliana
  • Kutoa Uchambuzi
  • Nifanyeje Ninapopewa Ushauri Unaoumiza Hisia?
    Vijana Huuliza
  • Nifanye Nini Ninapolaumiwa?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
  • “Hekima Huonyeshwa Kuwa Yenye Uadilifu kwa Matendo Yake”
    Huduma Yetu ya Ufalme—2010
  • Jinsi ya Kuwa Mstahimilivu
    Amkeni!—2019
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 11/8 kur. 24-26

Je! Wewe Unachukia Kupokea Uchambuzi?

JE! UNAWEZA kukumbuka wakati ulipochambuliwa mara ya mwisho? Jambo hilo humtokea kila mtu mara kwa mara na kwa sababu tofauti-tofauti.

Labda mtu alikuchambua ili ajitukuze. Hata hivyo, uchambuzi mara nyingi hutoka kwa mtu ambaye anajali mapendezi yako moyoni mwake: Mume wako aliona kasoro fulani kwa upishi wako; mke wako alisema kwamba tai yako haikulingana na suti yako; rafiki fulani alikuchambua kwa kutojitunza kiafya. Au huenda uchambuzi ulikuwa wa nidhamu, kama vile kutoka kwa mwajiri au mzazi (ikiwa wewe ni mchanga), ili kusahihisha jambo ulilosema au ulilofanya.

Iwe ni nini ilitokea, je, ulipokea uchambuzi huo kwa uchangamshi? Au ulikasirika, labda hata ukimwambia mtu huyo ajali shauri lake?

Kwa wengi, kupokea uchambuzi ni ono lenye uchungu. Wanakasirika, na kuwa na chuki. Wengine hupoteza uhakika wao, wakikata kauli kwamba ‘siwezi kufanya jambo lolote sawa’ na kisha wanapatwa na mkazo wa akili.

Je! wewe u miongoni mwa wale wanaochukia kuchambuliwa? Basi wewe ni mtu wa kawaida; wengi huhisi hivyo. Je! waweza kujifunza kupokea uchambuzi bila uchungu mno, na bila kuwa mwepesi wa kukasirika? Makala hii itachunguza njia sita ambazo kwazo uchambuzi waweza kupokewa vyema zaidi. Zinaweza kukusaidia uondoe, au angalau upunguze, mwasho wa uchambuzi.

1. Kubali Uchambuzi

Je! waonekana kuwa jambo lisilo la kawaida kwako kwa watu wengine kutaka uchambuzi, au hata kuutafuta? Gazeti Bits and Pieces lilionelea hivi: “Viongozi wenye akili. . . wanajua kwamba watakuwa na makosa kadiri fulani ya wakati. Ndiyo sababu wanataka hoja hizo zenye kuwapinga—ili kupunguza makosa kabla hayajafanywa, na kusahihisha makosa yaliyofanywa haraka iwezekanavyo.”

Kama vile wengine wawezavyo kuona mambo fulani ya sura yetu ambayo sisi hatuwezi kuona—shingo ya nguo iliyokunjika vibaya, tai iliyokaa vibaya— hivyo pia waweza kuona mambo fulani katika utu wetu ambayo sisi hatuwezi kuona. Ona maoni yao kuwa ya kusaidia badala ya kuwa tisho. Karibisha uchambuzi wao kuwa nafasi ya kujifunza jambo fulani. Uitumie kama jambo linalokutia nguvu.

2. Dhibiti Mchambuzi Wako Aliye Mkali Zaidi

Je! wewe hujichambua kupita kiasi? Je! wewe huwazia juu ya mapungufu yako? Au iwapo mtu anakutajia kosa lako fulani, je, wewe huliongezea kwa akili yako kwenye orodha ndefu ya udhaifu mbalimbali ambao hauhusiani na upungufu huo?

Dkt. Harold Bloomfield ataja hivi: “Ikiwa tayari tumekuwa na udhaifu wa kujichambua, basi hasa tutafadhaishwa tunapopokea uchambuzi kutoka kwa wengine. Hata mtu akitusifu na ana kajambo kadogo tu ka kuchambua, mara nyingi sisi hukazia kosa hilo kushinda mambo tuliofanya vyema.”

Uwe mwenye kusababu unapojichunguza mwenyewe. Wawezaje kujua jambo lililo la akili kufanya? Hebu wazia kwamba rafiki yako wa karibu anapokea uchambuzi kama huo. Ungetaka kupata itikio la namna gani kutoka kwake? Kujisikitikia? Kuwa na hasira? Kukataa kwa kiburi shauri nzuri? La, yaelekea ungetumaini kwamba angesikiliza uchambuzi huo bila kuona uchungu sana, auchunguze kwa unyofu, na kuutumia kwa maendeleo yake ya kibinafsi.

Basi, mbona usijifanyie mwenyewe ivyo hivyo?

3. Uliza Mambo Madogo-madogo

“Mimi sipendi tabia yako!” Je! ungetaka mtu akuambie hivyo? La, maneno kama hayo huumiza, au sivyo?

Jambo bora zaidi kwako kufanya katika kisa hicho ni kuuliza mambo madogo-madogo hususa. Katika kitabu chake Conversationally Speaking,” Alan Garner aeleza hivi: “Mara nyingi uchambuzi hutolewa bila kutaja mambo hususa. . . Kuuliza mambo hususa kutakusaidia upate kujua anachomaanisha mtu huyo. . .Na kama vile ripota afanyavyo, unachofanya tu ni kuuliza maswali yenye lengo la kujua ni nani, nini, lini, wapi, kwa nini, na jinsi gani.”

Kwa mfano, kwa yale maneno ambayo yametajwa hapo juu, ungeweza kujibu hivi: ‘Ni tabia ipi hasa unayomaanisha?’ Kama yeye bado hawi wazi vya kutosha, waweza pia kumwuliza: ‘Ni kwa sababu gani tabia hiyo inakasirisha? Je! waweza kunipa mfano wa siku nilipoonyesha tabia hiyo?’ Akitiwa moyo na tamaa yako ya kuwasiliana badala ya kubishana, maswali kama hayo yanaweza kusaidia mchambuzi wako na pia wewe kukazia akili mambo hususa. Maswali hayo yanaweza kufunua kama uchambuzi ni wa haki au tu unaonyesha wepesi wa kuona mabaya. Na pia yanakupa wakati zaidi wa kufikiria mambo hayo yote.

4. Umtulize Mchambuzi Wako

Vipi ikiwa anayekuchambua ameudhika? Dkt. David Burns apendekeza hivi: “Iwe mchambuzi wako yu sahihi au si sahihi, mwanzoni tafuta njia fulani ya kukubaliana naye.” kufanya hivyo kunakusaidiaje? Kufanya hivyo kuna mwelekeo wa kupunguza udhia wa mchambuzi wako, kumtuliza, na kumfanya awasiliane zaidi.

Kwa upande mwingine, ukijikinga moja kwa moja—kama inayoelekea ikiwa shtaka hilo si la haki—basi ni kama unaongezea nguvu mchambuzi wako. Kama aelezavyo Dkt. Burns: “Utapata kwamba uchambuzi wa mpinzani wako unazidi!” Basi, jambo bora kabisa la kufanya ni kutafuta mambo ya kukubaliana kabla ya kuzungumzia mambo yoyote ya kubishaniwa.

5. Kazia Yaliyomo Katika Uchambuzi, Si Jinsi Yanavyotolewa

Mama mmoja alipata lalamiko kuhusu tabia ya mtoto wake katika ujirani. Lalamiko hilo lilitolewa kwa ukali na kwa roho ya ushindani. Mama huyo kwa urahisi angetupilia mbali lalamiko la jirani huyo kuwa lisilo la haki na linakosa unyofu, na kwa kweli alishawishwa afanye hivyo.

Badala ya hivyo, baada ya kusababu kwamba kulikuwa na ukweli fulani kwa uchambuzi huo, alimwambia mtoto wake hivi: “Nyakati zote si watu watupendao ndio hutuonyesha makosa yetu, hata iwapo ni sisi tunafaidika nayo. Tutumie lalamiko hilo kuwa nafasi ya kufanya maendeleo.”

Je! mtu fulani amekukaripia vikali? Labda mtu huyo ana tatizo la kuchokozeka haraka au hata wivu. Wewe au mwingine waweza kuwa na fursa ya kumsaidia kwa wakati unaofaa. Lakini usikatae wazo lake kwa sababu tu ya kwamba alilitoa kwa ukali mno. Kazia fikira juu ya yaliyomo katika uchambuzi. Je! oni lake ni kweli? Ikiwa ndivyo, usijinyime nafasi hii ya kufanya maendeleo.

6. Punguza Ukali wa Uchambuzi

Hilo huenda likakushangaza, lakini wewe una uwezo wa kadiri fulani wa kudhibiti mara ambazo wewe hupokea uchambuzi na pia ukali ambao wewe waupokea. Kanuni hii ni ya kweli hasa katika hali ya uchambuzi wa kukosolewa kutoka kwa watu walioko mamlakani. Jinsi gani hivyo?

Zamani sana, mmea wa mkunde mweusi ulipendwa sana katika Palestina. Lakini kwa kutofautiana na mimea mingine, haukupurwa kwa vitu vizito au vizungushio vya kupura. Badala ya hivyo, mmea huu ulipurwa kwa fimbo au ufito. Mbona kazi hiyo ya ustadi na ya uanana kwa mmea huo? Kwa sababu mbegu ndogo ndogo na nyororo za mmea huo hazikuhitaji kupurwa kwa uzito kwa vile kwa hakika zingeharibiwa.

Kitabu cha Biblia cha Isaya chatumia mmea wa mkunde mweusi kutoa kielelezo cha hali tofauti-tofauti za nidhamu. Mtu anapoitikia masahihisho madogo-madogo, hatahitaji sahihisho kali kwa kosa lile lile.—Isaya 28:26, 27.

Hivyo, waweza kuzuia sahihisho nzito kwa kuitikia kwa haraka kwa uchambuzi wa mambo madogo-madogo. Kwa mfano, je, wajua kwamba wewe huchelewa mara nyingi kazini? Basi sahihisha tabia hiyo sasa, kabla mwajiri wako hajazungumza nawe kulihusu. Je! tayari amekutajia jambo hilo? Basi itikia upesi kwa kufika kwa wakati, kabla hajaona kwamba inafaa achukue hatua zaidi.

Waweza Kukabiliana

Kupokea uchambuzi kwaweza kuumiza. Huenda ukatamani watu wakuache, waache kukuhukumu, na kuacha kutoa ‘madokezo yanayosaidia.’

Lakini kutamani watu wasikusumbue na kukataa kupokea uchambuzi hakutakomesha uchambuzi. Kuwa mchambuzi ni sehemu ya utu wa kibinadamu sasa. Zaidi ya hilo, wewe huna udhibiti juu ya kiwango cha busara ambacho wengine hutumia wanapotoa ushauri ambao haukuombwa.

Badala ya kukasirika, tumia kwa faida kile uwezacho kudhibiti: itikio lako. Tumia baadhi ya madokezo yaliyo hapo juu ili kukabiliana na uchambuzi na kupunguza uchungu wayo. Utafurahi kuwa ulifanya hivyo.

Kutoa Uchambuzi

Ikiwa wewe ni mwepesi wa kukasirika unapopokea uchambuzi, huenda ukawa na matatizo kuutoa pia. Hapa pana miongozo kadhaa ya kukumbuka unapotoa uchambuzi:

Tumia maneno machache. Jitihada zisizoongozwa vyema za kuepuka kuumiza hisia za yule unayemchambua hutokana mara nyingi na maneno mengi ya bure, ambayo yanaweza kutoa ujumbe usio wazi.

Epuka kuchambua kila kakosa kadogo unakoona kwa mtu. Hiyo hukasirisha, na hatimaye watu watatupilia mbali maoni yako kuwa hayafai. Huenda hata wakaanza kukuepa. Kila mmoja hajakamilika na ana mapungufu. Hawawezi kuyafanyia kazi mapungufu yao yote pamoja kwa wakati ule ule mmoja. Ikiwa kosa unaloona si nzito, acha lipite. Ni kama vile Biblia inavyoonelea: “Upendano husitiri wingi wa dhambi.”—1 Petro 4:8.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki