Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 2/22 uku. 3
  • Kupanga Uzazi Kwawa Suala la Duniani Pote

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kupanga Uzazi Kwawa Suala la Duniani Pote
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Watoto—Ni Faida au Ni Hasara?
    Amkeni!—1993
  • Wazazi—Wafundisheni Watoto Wenu Kumpenda Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2019
  • Kwa Nini Hawana Watoto?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Idadi ya Watu, Biblia, na Wakati Ujao
    Amkeni!—2004
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 2/22 uku. 3

Kupanga Uzazi Kwawa Suala la Duniani Pote

“Kupanga uzazi kungeweza kuleta manufaa zaidi kwa watu wengi zaidi kwa gharama ndogo zaidi ya ‘tekinolojia’ nyingine yoyote moja inayopatikana kwa jamii ya kibinadamu. . . . Bado ingekuwa

hivyo hata kama hakungekuwa na jambo kama tatizo la idadi ya watu.”—The State of the World’s Children 1992.

WAKATI uliopita lilifikiriwa kuwa jambo lenye kutamanika kuwa na watoto wengi. Karibu miaka elfu nne iliyopita, wakati Rebeka alikuwa karibu kuondoka Mesopotamia akaolewe na Isaka, mama yake na ndugu yake walimbariki kwa maneno haya: “Ndugu yetu, uwe wewe mama wa kumi elfu, mara elfu nyingi.” (Mwanzo 24:60) Nyakati zimebadilika. Leo, wanawake zaidi na zaidi wanasema kwamba wanataka watoto wachache zaidi.

“Mimi nilikuwa wa tatu kati ya watoto saba,” akasema Bu, mama Mwindonesia mwenye umri wa miaka 22 ambaye ana binti mmoja. “Baba yangu alikuwa mchuuzi wa maji ya mnazi katika Klaten, Java ya Kati, na wazazi wangu walipata magumu mengi wakijaribu kulea watoto wengi hivyo. . . . Ni rahisi zaidi kulea familia ikiwa una idadi ndogo tu ya watoto.”

Hisia za Bu zafanana na za wazazi wengi ulimwenguni kote. Inazidi kuwa kwamba mume na mke wanataka kupanga wakati wa kuanza kuwa na watoto, watakuwa na wangapi, watoto wataachana umri kwa miaka mingapi, na wakati wa kuacha kuwa nao. Hiyo inaonyeshwa na takwimu za UM zinazoonyesha kwamba utumizi wa hiari wa vizuia-mimba katika nchi zinazositawi umeongezeka kwa njia yenye kutokeza, kutoka asilimia 10 ya mume na mke katika miaka ya 1960 hadi asilimia 51 leo.

Vilevile serikali zinapendezwa sana na kuendeleza kupanga uzazi. Zaidi ya nusu ya mataifa yanayositawi yanafuatilia sera za kupunguza ukuzi wa idadi ya watu. Hazina ya Idadi ya Watu ya UM yakadiria kwamba jumla ya matumizi ya programu za kudhibiti idadi ya watu sasa ni kama dola 4,500,000,000 za U.S. kila mwaka. Ili kutimiza mahitaji ya wakati ujao, wenye mamlaka watumaini kwamba tarakimu hiyo itakuwa mara mbili kufikia mwaka 2000.

Kwa nini mataifa na mtu mmoja mmoja wanapendezwa sana hivyo na kudhibiti uzazi? Na maoni ya Kikristo ni nini juu ya jambo hili la maana? Makala hizi mbili zifuatazo zitazungumzia maswali hayo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki