Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 2/22 uku. 21
  • Tekinolojia ya Kale—Maajabu ya Kisasa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Tekinolojia ya Kale—Maajabu ya Kisasa
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Maji Halisi na ya Kiroho Ni Muhimu kwa Uhai
    Amkeni!—2001
  • “Mvua Hainyeshi Kamwe Huku Lima”
    Amkeni!—2003
  • Je, Maji Yanazidi Kupungua Ulimwenguni?
    Amkeni!—2001
  • Kito cha Mwitu
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 2/22 uku. 21

Tekinolojia ya Kale—Maajabu ya Kisasa

“MJI [wa Turfan], ulio katika mojawapo sehemu za dunia zilizo na joto jingi zaidi, zilizo kame zaidi, unabaki kuwa chemchemi ya jangwani inayositawi, kwa sababu ya tekinolojia ya miaka 2,000,” likaripoti The Globe and Mail la Toronto, Kanada.

Turfan lina sifa ya kuwa si jiji lenye joto zaidi katika Uchina bali pia mojawapo sehemu zilizo na joto jingi zaidi na zilizo kavu zaidi duniani. Idadi ya watu humo ipatayo 180,000 huishi katika upande wa kaskazini wa Bonde la Turfan, ambalo ni mweneo wa Jangwa la Takla Makan. Mvua hainyi kabisa, na kwa sababu ya joto jingi, mvua kidogo inayokunya hugeuka kuwa mvuke kabla ya kufika chini. Wakati wa miezi ya kiangazi, kwa kawaida hali-joto hufikia Sentigredi 54 kwenye kivuli.

Na bado, miti na vichaka huzunguka Turfan, ikieneza eneo la hekta 3,200. Hiyo hulinda wenyeji dhidi ya dhoruba kali za mchanga zinazopiga mji huo mara kwa mara. Dhoruba hizo huanzia Jangwa la Takla Makan na huchukua kiasi kikubwa cha mchanga unaoweza kuzika majengo kabisa na kufunika mashamba yenye rutuba. Hivyo miti na vichaka hulinda chemchemi hiyo ya jiji isiharibiwe na hatari za jangwani.

Kujapokuwa hali hiyo isiyopendeza ya dhoruba zenye msukosuko na hali-joto zenye kuchoma, Turfan linasitawi likiwa kitovu cha kilimo. Kuna aina-aina za vyakula vya kigeni, tende, zabibu, matikiti, mikomamanga, maembe ulaya, maembe dodo ulaya, matofaa, mabilingani, vitunguu, na ngano na nafaka nyinginezo, kutia ndani pamba nzuri zaidi yenye nyuzi ndefu inayokuzwa katika Uchina. Kwa muda mrefu sana, Turfan limejulikana kwa mazao ya kilimo ya hali ya juu na ya unamnanamna. Kwa maelfu ya miaka, limekuwa jumuiya yenye kusitawi katika chemchemi yenye rutuba.

Ni tekinolojia ipi ya miaka 2,000 ambayo imelifanikisha hivyo? The Globe and Mail ladai kwamba jiji hilo linawia usitawi walo kwa “mfumo wa kale wa unyunyizaji maji ambao ni mojawapo amali za ustadi na uhandisi wa muda mrefu wa mwanadamu.” Gazeti hilo laongeza hivi: “Siri ya usitawi [wa Turfan] ni ile mifereji mingi ajabu inayopitana-pitana ya kunyunyiza maji na visima—inayoitwa karez katika Kiugur cha wenyeji—inayochukua maji yanayotiririka kutoka milima yenye theluji ya Tian Shan, kilomita 80 kwenda kaskazini-magharibi.” Inaelekea kwamba maji hayo yangalikauka kabla ya kufika kwenye mitaro ya jiji ikiwa hayangaliletwa kupitia chini ya ardhi kwa mamia ya mifereji inayofanyiza mfumo tata wa unyunyizaji maji.

Muda mrefu kabla ya Wauighur kusitawisha mfumo wao wa unyunyizaji, Waajemi wa kale walitumia mifereji hiyohiyo mingi ya unyunyizaji. Encyclopœdia Britannica chasema: “Waajemi walisitawisha vyanzo vya maji vya chini ya ardhi kwa kuchimba mifereji, au kanats, katika vilima, mara nyingi mamia kadha ya futi kwenda chini ya ardhi na kama maili 12 (kilometa 19) kwa urefu.” Kwelikweli, tekinolojia hiyo ya kale ya unyunyizaji maji ni yenye kustaajabisha hata katika siku za kisasa, kwa kuwa hudumisha chemchemi ya jangwani katika mojawapo sehemu zenye joto jingi zaidi, na kame zaidi duniani.

Ingawa tekinolojia za kale na mpya zinageuza majangwa kuwa bustani zenye kupendeza, katika wakati ujao usio mbali sana, kupitia serikali yake ya Ufalme, Yehova atafanya majangwa yote ya dunia yachanue, kwa furaha ya familia ya kibinadamu. Nabii wa Yehova asema: “Nyika na mahali palipo ukiwa patafurahi; jangwa litashangilia na kuchanua maua kama waridi. Litachanua maua mengi, na kufurahi, naam, kwa shangwe na kuimba; litapewa uzuri wa Lebanoni, utukufu wa Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa BWANA [Yehova, NW], ukuu wa Mungu wetu.”—Isaya 35:1, 2.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki