Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 7/22 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Chakula cha Kutosha, Lakini Utapiamlo Wazidi
  • Tamathali ya Msaada wa Somalia
  • Akina Baba Pia ni wa Kulaumiwa
  • Kupendezwa Kunakokua kwa Roho Zenye Nguvu Zaidi
  • Uuwaji wa Waandishi Habari
  • Ni Homa Nyingine Yenye Kuenea Kote?
  • Waume Wenye Kupigwa
  • Kusaka Wachawi Bado Kupo
  • Kulaumu Kafeini
  • Tauni Mbaya Zaidi Katika Historia
    Amkeni!—2005
  • Mambo Tunayojua Sasa Kuhusu Homa
    Amkeni!—2005
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Kulinda Familia Yako Dhidi ya Homa
    Amkeni!—2010
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 7/22 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Chakula cha Kutosha, Lakini Utapiamlo Wazidi

Hata ingawa idadi ya watu ulimwenguni pote imeongezeka ajabu, utapiamlo umepunguka kwa watu zaidi ya milioni 150 katika nchi maskini kuliko ulivyokuwako miaka 20 iliyopita. “Utokezaji wa chakula na wakulima wameongeza mazao ya chakula kwa kadiri sawa hata kupita idadi ya watu,” asema John Lupien, mkurugenzi wa Shirika la UM linaloshughulika na Chakula na Kilimo. “Kwa sasa, kuna chakula cha kutosha kulisha kila mtu, ikiwa kwa kweli kingewafikia watu wanaokihitaji.” Kwa kuhuzunisha, The Economist laripoti, “karibu watu [milioni] 780 katika nchi maskini, moja kati ya tano ya idadi ya watu katika nchi maskini, hawapati chakula cha kutosha. Watu wapatao bilioni 2 ambao wanapata chakula cha kutosha kumaliza njaa lakini wanakosa vitamini na madini wanazohitaji. . . . Watoto wapatao 40,000 hufa kila siku, sababu moja ikiwa ni utapiamlo unaowafanya wapatwe kwa urahisi na aina zote za ugonjwa.” Kwa upande mwingine, mlo wa kupita kiasi unasababisha matokeo yenye kuumiza pia, kutia ndani magonjwa kama vile ugonjwa wa moyo na kansa za aina fulani miongoni mwa jamii ya watu matajiri.

Tamathali ya Msaada wa Somalia

Kuingizwa kwa chakula cha bure katika Somalia yenye kupatwa na njaa kumetokeza tamathali yenye kushangaza. Huku msaada wa chakula ukiwa wenye matokeo katika kukomesha njaa, unatisha pia kuharibu uchumi wa ukulima wa wenyeji. Chakula kilipokuwa kidogo hivi kwamba watu milioni 1.5 walikabiliwa na njaa kali na kifo, bei za chakula zilipanda ajabu. Lakini baada ya mtiririko wenye kuendelea wa msaada wa chakula, bei zilishuka zaidi. “Bei ya mchele inasemekana kuwa ya chini zaidi ulimwenguni, bei ya gunia la mchele la kilo 50 ilishuka hadi dola 5 za U.S. kwa miezi michache iliyopita,” ikasema ripoti ya New York Times. “Kwa kulinganisha, kiwango hichohicho cha aina hiyo ya mchele kingeuzwa karibu dola 11.70 katika United States na dola 120 katika Japani.” Kama tokeo, chakula kinachotolewa na wenyeji kimekosa thamani hivi kwamba wakulima hawawezi kuuza mazao yao. Programu sasa inaendelea ya kuuza badala ya kupeana msaada wa chakula na kujaribu kusawazisha gharama.

Akina Baba Pia ni wa Kulaumiwa

Kwa muda fulani sasa, kina mama wanaotazamia watoto wameonywa kuepuka mambo ambayo yatasababisha kasoro za kuzaa, kama vile kileo na kuvuta sigara, na kula mlo unaofaa. “Sasa, maonyo kama hayo yamepewa wale wanaotazamiwa kuwa kina baba,” likasema U.S.News & World Report. “Uchunguzi mpya unadokeza kwamba mwanamume akijihatarisha kwa kemikali hataathiri tu uwezo wake wa kutokeza mtoto bali pia afya ya wakati ujao ya watoto wake.” Ushuhuda unaonyesha kwamba wanaume “wanachangia kuliko ilivyojulikana mbeleni kwa kuharibika kwa mimba katika wake zao na kasoro nyinginezo, kansa na kuchelewa kukua kwa watoto wao.” Inaonekana sasa kwamba dawa na kemikali nyingine (kutia ndani masalio ya uvutaji sigara), pamoja na mlo unaokosa mboga na matunda ya kutosha yenye vitamini C, zinaharibu shahawa. Mtaalamu wa sumu Devra Lee Davis asema: “Kwa muda mrefu tumekuwa tukikaza fikira kwa kina mama. Umuhimu wa kina baba katika kufanyiza watoto wenye afya umekuwa haujulikani.”

Kupendezwa Kunakokua kwa Roho Zenye Nguvu Zaidi

Ongezeko la ulimwenguni la kupendezwa na roho zenye nguvu zaidi linaonekana sana katika Afrika Kusini. Waganga wa kienyeji, dini inayodai kuwa na uwezo wa kuponya, unajimu, na ibada ya Shetani zimeongezeka kwa wingi hivi karibuni tangu miaka ya katikati ya 1980. Kwa nini? “Wakati wa shida, watu huacha kutumia busara na kugeukia mafumbo yasiyofahamika.” Likasema The Weekly Mail la Johannesburg. “Mwisho wa mileani ya pili, kumekuwa na ongezeko la kupendezwa na mambo ya roho.” Mchunguzi wa elimu ya binadamu Robert Thornton aelezea hivi: “Nafikiri itikadi hizi zinaonyesha aina ya woga ambao watu wanao. Ni uchunguzi wa watu ambao wanahisi hawawezi kudhibiti maisha yao.” Mfunzi wa fizikia isiyo ya akili Rod Suskind asema: “Sababu moja ya kupendezwa huko kunakoongezeka ni kwamba wakati ujao unaonekana kukosa matazamio, na watu wanatafuta vyanzo visivyo vya kawaida ili kuelewa jambo linalotukia.” Na kulingana na The Weekly Mail, mchunguzi wa elimu ya binadamu Isak Niehaus “analaumu ukosefu wa sayansi na dini za kawaida kujibu masuala ya maana yanayokabili watu.”

Uuwaji wa Waandishi Habari

Angalau waandishi habari 60 waliuawa walipokuwa wakiripoti habari za mapambano ya ulimwengu katika 1992. Ripoti hiyo, iliyochapishwa na Shirika la Kimataifa la Waandishi Habari katika Brussels, Ubelgiji, na kuandikwa kwenye Manchester Guardian Weekly, ilitaja Uturuki na Bosnia kuwa mahali hatari zaidi. Angalau waandishi habari kumi walisemwa kuwa wameuawa katika nchi hizo mbili mwaka uliopita. Waandishi habari pia wamekuwa wakitishwa wanapoandika juu ya habari ya vita vya ukoo na njaa katika Somalia. Shirika hilo linauliza Umoja wa Mataifa na serikali za Jumuiya ya Ulaya kutangaza kwamba kukagua habari ni “kuvunja kabisa haki za kibinadamu.”

Ni Homa Nyingine Yenye Kuenea Kote?

“Bila shaka, homa yenye kuenea itakuwa tauni kubwa itakapoibuka, labda katika miaka kadhaa inayokuja,” laeleza The New York Times Magazine. “Kulingana na wanasayansi, wakati umefika wa kutokea kwa homa yenye kuenea inayofanana na ile ya 1918 iliyoua watu kati ya milioni 20 hadi milioni 40. “Kuna matarajio makubwa kwamba ikiwa ilitokea wakati moja, inaweza kutokea tena,” asema John R. La Montagne, mkuu wa magonjwa ya kuambukizwa katika Taasisi ya Kitaifa ya Mizio na Magonjwa ya Kuambukizwa katika Bethesda, Maryland. Hata hivyo, kubadilika kwa virasi ambayo hutokeza ugonjwa wenye kudhoofisha wa homa hiyo haupatikani kwa urahisi. Zimepatikana mara tatu tu katika karne hii: ile inayoitwa homa ya Hispania ya 1918, homa ya Asia ya 1957, na homa ya Hong Kong ya 1968; na hizo mbili za mwisho zilikuwa za kadiri. Kwa sababu virasi vya homa hujibadili mara nyingi na pasipo kutazamiwa, mweneo wenye kufisha waweza kutokea kabla ya chanjo sahihi kutengenezwa. Makala hiyo ilimalizia: “Ikiwa historia inategemeka labda tunaweza kutazamia mabadiliko makubwa ya antijeni hizo—badiliko moja kubwa likiweza kutoa homa kali ulimwengu pote—kabla ya karne hii kwisha.”

Waume Wenye Kupigwa

“Karibu asilimia 40 ya wanawake waliohojiwa katika uchunguzi uliodhaminiwa na serikali ulisema kwamba walikuwa wametisha au kuwaumiza kimwili waume zao, sana kuliko asilimia ya wanaume waliotoa lalamiko kama hilo,” lasema The Toronto Star. “Uchunguzi huo wabadilisha imani inayojulikana sana kuhusu jeuri ya familia . . . Hata watafiti walishangazwa na matokeo ya uchunguzi huo.” Huko kutenda vibaya kulitia ndani kutisha, kurusha kitu fulani, au kupiga kwa kutumia chombo. Katika visa vilivyo vingi wanawake walisema kusudi la jeuri yao halikuwa kujikinga wenyewe. “Utafiti huu unapaswa kufanya watu wafikirie tena chanzo chote cha kutenda vibaya mwenzi wa ndoa kwa uhalifu,” akasema Rena Summer, mwanafunzi wa udaktari katika idara ya masomo ya familia ya Chuo Kikuu cha Manitoba na ambaye pia ni mmoja wa waandishi wa uchunguzi huo. Hata hivyo, kwa sababu wanaume mara nyingi wana nguvu kuliko wanawake, wanawake mara nyingi hupata majeraha makubwa ikiwa wanatendwa vibaya na waume, akasema.

Kusaka Wachawi Bado Kupo

Wakitajwa kuwa wachawi, wanawake zaidi ya 12 katika makabila ya bara la India waliuawa na umati wenye ghadhabu kali kwa kipindi cha miezi miwili, laripoti India Today. “Wanawake wengine wengi wamepigwa, kuteswa, wakatembezwa wakiwa uchi, wakadhiliwa kinyama na kufukuzwa vijijini mwao.” Visa hivyo vya kinyama vilianza na maandamano ya kidini yaliyoenda kijiji hadi kijiji. Zoea hilo liliongoza kwenye mabadiliko na upungufu wa uhalifu katika jamii. Lakini baadhi ya wanawake wenye kushiriki katika maandamano hayo “wakapagawa” na kuanza kuwatambua wanawake kadhaa katika kijiji kuwa wenye kuhusika kwa matatizo ya wenyeji. Kushindwa kupita “mtihani” wa kutokuwa na hatia, kama vile mchawi kufufua mtu mfu ikiwa alishtakiwa kuua, kulimaanisha adhabu ya mara hiyo. Kuamini uchawi ndiko kunasemekana kuwa sababisho kuu la hali hiyo, na kulingana na mchunguzi mmoja wa elimu ya binadamu, “kunatokana na tamaa katika jamii za kikabila kudhibiti na kutumia roho zenye nguvu zaidi, kuwa na uwezo dhidi ya kijicho, uwezo wa kufikia miradi yao na uwezo wa kuwalazimisha wengine wafanye kama watakavyo.”

Kulaumu Kafeini

Wanywaji kahawa kupita kiasi wanaoacha tabia yao kwa ghafula wanalalamika kuumwa kichwa, mshuko wa moyo, ulegevu, hangaiko, na hata maumivu ya misuli, ugagazi, na kutapika. Sasa, watafiti katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins wamepata kuwa dalili hizo zapatikana kwa watu wanaokunywa kikombe kimoja tu au viwili vya kahawa au chai kila siku, au soda nyingi ambayo ina kafeini, na ambao wanakosa kunywa kwa siku mbili. Matokeo ya kuacha kunywa yanaweza kuwa mabaya sana hivi kwamba wahisi kumwona daktari. Waathiriwa wanaweza kuwa wale ambao wanakosa kunywa kahawa ya kutengenezwa kazini wakati wa mwisho juma, watu wanaogeukia soda zisizo na kafeini, au wagonjwa ambao wanapaswa kujiepusha na chakula au kinywaji kabla ya upasuaji. Madaktari wanashauriwa kuandika kiwango cha matumizi ya kafeini ya wagonjwa wanaolalamika kuumwa vichwa na dalili nyingine ambazo zinaonwa na mtu anayeacha kafeini. Wale wanaotamani kupunguza kunywa kafeini wanashauriwa kufanya hivyo polepole. Uchunguzi huo ulitokeza swali ikiwa kafeini, na hivyo basi kahawa, inapaswa kuorodheshwa upande wa dawa halisi ya kulevya.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki