Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 1/8 kur. 24-25
  • Wanasayansi Wahadaa Umma

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wanasayansi Wahadaa Umma
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • “Mtu wa Orce” Atangazwa na Vyombo vya Habari
  • Kasoro Juu ya Utambulisho
  • Kwa Nini Walihadaiwa?
  • “Sayansi Huhangaikia Kuvumbua Kweli”
  • Je, Uhai Wote Umetokana na Chanzo Kimoja?
    Maswali Matano Muhimu Kuhusu Chanzo cha Uhai
  • Majitu Yalipokuwa Yamejaa Ulaya
    Amkeni!—2009
  • Mageuzi
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
  • Sayansi: Je! Imethibitisha Biblia Kuwa Yenye Makosa?
    Biblia—Neno la Mungu au la Binadamu?
Amkeni!—1994
g94 1/8 kur. 24-25

Wanasayansi Wahadaa Umma

Na mleta habari za Amkeni! katika Uhispania

TOMÁS SERRANO, mkulima Mhispania aliye mzee-mzee, mwenye ngozi iliyochomwa na jua, alikuwa ameamini kwa miaka mingi kwamba shamba lake dogo la Andalusia lilikuwa na jambo fulani la kipekee. Mara nyingi jembe lake la kulimia lilifukua mifupa na meno yasiyo ya kawaida ambayo kwa hakika hayakuwa ya ng’ombe wowote wa hapo. Lakini aliposema kijijini juu ya vitu alivyopata, hakuna mtu aliyetoa uangalifu—angalau haikuwa hivyo hadi 1980.

Mwaka huo timu ya watafiti wa mabaki ya vitu vya kale waliwasili ili kutafiti sehemu hiyo. Kabla ya muda mrefu walipata hazina kubwa ya mabaki ya kale: mifupa ya dubu, ndovu, viboko, na wanyama wengineo—wote wakiwa wamewekwa katika eneo dogo ambalo ilionekana lilikuwa bwawa lililokauka. Hata hivyo, ilikuwa katika 1983, eneo hilo maarufu lilipotokea ghafula katika vichwa vikuu vya habari vya kimataifa.

Kipande kidogo lakini cha kipekee cha fuvu kilikuwa kimepatikana hivi karibuni. Kilitangazwa kuwa “mabaki ya kibinadamu ya kale zaidi kuvumbuliwa katika Ulaya na Asia.” Kwa kukikadiria kuwa chenye umri wa miaka kati ya 900,000 na 1,600,000, wanasayansi fulani walitazamia kuanzisha “mvuvumko katika uchunguzi wa jamii ya kibinadamu.”

Baki lililochochea msisimuko huo wote liliitwa “Mtu wa Orce”—kwa kuitwa jina la kijiji hicho kilicho katika mkoa wa Granada, Uhispania, ambako lilipatikana.

“Mtu wa Orce” Atangazwa na Vyombo vya Habari

Mnamo Juni 11, 1983, baki hilo lilionyeshwa kwa umma katika Uhispania. Wanasayansi mashuhuri wa Uhispania, Ufaransa, na Uingereza walikuwa tayari wametia uhakikishio wa uasilia walo, na utegemezo wa kisiasa ulikuwa ukija upesi. Gazeti la kila mwezi la Uhispania liliripoti hivi kwa msisimuko: “Uhispania, na hasa Granada, sasa iko katika mstari wa mbele wa asili ya [binadamu] wa kale katika kontinenti kubwa ya Ulaya na Asia.”

“Mtu wa Orce” alikuwaje hasa? Wanasayansi wamfafanua kuwa mhamiaji wa hivi karibuni kutoka Afrika. Ilisemwa kwamba baki hilo hususa lilikuwa la kijana aliyekuwa mwenye umri wa miaka 17 na kimo cha meta moja unusu. Labda alikuwa mwindaji na mkusanyaji ambaye huenda hakuwa bado amejifunza kutumia moto. Yaelekea tayari alikuwa amesitawisha lugha na dini ya msingi. Alikula matunda, nafaka, beri, na wadudu, kutia na mabaki ya wanyama ambayo fisi walikuwa wameua mara kwa mara.

Kasoro Juu ya Utambulisho

Katika Mei 12, 1984, majuma mawili tu kabla ya mkutano wa kimataifa wa kisayansi juu ya jambo hilo, shaka nzito zilitokea juu ya asili ya baki hilo. Baada ya kuondoa kwa uangalifu mabaki ya chokaa kutoka sehemu ya ndani ya fuvu hilo, wachunguzi hao wa mabaki ya kale walipata “kigongo” chenye kukatisha tamaa. Mafuvu ya kibinadamu hayana kigongo kama hicho. Mkutano huo uliahirishwa.

Gazeti la Madrid la kila siku El País lilikuwa na kichwa kikuu, “Dalili Kubwa Kwamba Fuvu la ‘Mtu wa Orce’ ni la Punda.”[11a] Hatimaye, katika 1987, gazeti la kisayansi lililoandikwa na Jordi Agustí na Salvador Moyà, wawili kati ya wachunguzi wa vitu vya kale waliohusika katika uvumbuzi wa pale mwanzoni, walijulisha kwamba uchanganuzi wa eksi-rei kwa kweli ulikuwa umethibitisha kwamba baki hilo lilikuwa la aina fulani ya farasi.

Kwa Nini Walihadaiwa?

Kushindwa huko kulitokea kwa sababu kadhaa, ambazo hakuna zozote kati yazo zinazohusu njia ya sayansi. Katika uwanja wa wanasayansi, ni nadra kwa uvumbuzi wenye kutazamisha wa wazazi wa kale wa kibinadamu kudumu muda mrefu. Wanasiasa walifanya upesi kuunga mkono, na usahihi wa kisayansi ulifunikwa kwa harara ya kitaifa.

Waziri mmoja wa utamaduni wa eneo alijulisha kwamba ilikuwa pindi yenye fahari kwa Andalusia “kuwa mahali pa uvumbuzi mkubwa jinsi hiyo.” Shaka juu ya uvumbuzi huo zilipotolewa na wataalamu fulani, serikali ya mkoa wa Andalusia ilishikilia kwa dhati kwamba “mabaki hayo yalikuwa asilia.”

Sababu moja inayofanya baki dogo kama hilo (lenye kipenyo cha karibu sentimeta 8) kupata maana kubwa ni ukosefu wa ithibati inayounga mkono eti mageuzi ya mwanadamu. Ijapokuwa kipimo kidogo cha baki hilo, “Mtu wa Orce” alisifiwa kuwa “uvumbuzi mkubwa zaidi wa watafiti wa vitu vya kale, kutia na kuwa kile kiungo kinachokosekana kati ya mwanadamu wa kawaida wa Afrika (Homo habilis) na mwanadamu wa kale zaidi wa kontinenti ya Ulaya na Asia (Homo erectus).” Mawazio mengi na kukisia kusiko kwa kisayansi kulitosha kujazia mambo madogo-madogo juu ya sura na njia ya maisha ya “Mtu wa Orce.”

Mwaka mmoja hivi kabla ya uvumbuzi wa “Mtu wa Orce,” kiongozi wa ile timu ya wanasayansi, Dakt. Josep Gibert, alikuwa amekisia juu ya mambo ya kushtua ambayo eneo hilo lingefunua. “Ni mojawapo sehemu maarufu zaidi ambazo Wakwotenari wadogo walio wengi walipatikana katika Ulaya,” yeye akakazia. Na hata baada ya utambulisho wa kweli wa baki hilo kufunuliwa, Dakt. Gibert alisisitiza: “Jumuiya ya kisayansi ya kimataifa yaamini kwa dhati kwamba katika eneo la Guadix-Baza [ambako baki hili lilipatikana], baki la kibinadamu lenye umri zaidi ya milioni moja halina budi kupatikana, na huo kwa kweli utakuwa uvumbuzi mkubwa.” Kwa kweli, huko ni kutamani mambo yasiyowezekana!

“Sayansi Huhangaikia Kuvumbua Kweli”

Mvumbuzi mwenzi wa “Mtu wa Orce,” Dakt. Salvador Moyà, alikiri hivi kwa unyoofu kwa Amkeni!: “Dakt. Jordi Agustí nami tulipata kuwa vigumu sana kukubali kwamba baki hilo halikuwa la kibinadamu. Hata hivyo, sayansi huhangaikia kuvumbua kweli, hata ingawa huenda isiwe kwa upendeleo wetu.”

Kibishanio ambacho kimehusu yule “Mtu wa Orce” chatoa kielezi jinsi ilivyo kazi ngumu kwa wachunguza vitu vya kale kufukua kweli juu ya yale yaitwayo eti mageuzi ya mwanadamu. Kujapokuwa miongo ya uchimbaji, mabaki ya kweli ya yule anayedhaniwa kuwa mzazi wa kale aliye kama nyani hayajapatikana. Ingawa huenda isipendelee wanasayansi fulani, je, yaweza kuwa kwamba ukosefu wa uthibitisho imara waelekeza kwenye uhakika wa kwamba mwanadamu si tokeo la mageuzi?

Mchunguzi asiyependelea upande wowote aweza kujiuliza kwa kufaa kama “wanadamu-nyani” wengine wenye kusifiwa ni halisi zaidi ya vile yule “Mtu wa Orce” amethibitika kuwa.a Kama vile historia imeonyesha waziwazi, sayansi yaweza kuongoza watu kwenye kweli, lakini si kwamba wanasayansi hawawezi kukosea. Ni hivyo hasa wakati upendeleo wa kisiasa, kifalsafa, na kibinafsi unapofanya suala lisiwe wazi—na wakati kitu kidogo sana chatumiwa kujaribu kueleza mambo mengi sana.

[Maelezo ya Chini]

a Kwa uchanganuzi wenye mambo mengi juu ya wale waitwao eti wanadamu-nyani, ona sura ya 9 ya kitabu Life—How Did It Get Here? By Evolution or by Creation? kilichotangazwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

[Picha katika ukurasa wa 24, 25]

Juu: Nakili ya kipande cha sentimeta saba unusu cha yule aliyesemwa kuwa “Mtu wa Orce”

Kulia: Mchoro wa “mwanadamu wa kale” wa kudhaniwa kama vile wanamageuzi wanavyowaza

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki