Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 5/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mahakama Kuu Yafanya Uamuzi wa Kuunga Mkono Mmoja wa Mashahidi wa Yehova
  • Lugha Inayokua
  • Wapenzi wa Pilipili Kali
  • Watoto Wafanya-Ngono
  • Vijana Wenye Tatizo la Unywaji
  • Mahali pa Kuzoezea Wahalifu
  • Majeruhi wa Ushindi
  • Kutojali Sana Afya
  • Tatizo la Kuwa na Mafuta Mengi Mno Mwilini
  • Watoto Wenye Kutendwa Vibaya
  • Uhalifu wa Kupangwa Kitengenezo
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1997
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2003
  • Kiungo Kilichotoka Sehemu za Mbali Sana za Dunia
    Amkeni!—2000
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 5/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Mahakama Kuu Yafanya Uamuzi wa Kuunga Mkono Mmoja wa Mashahidi wa Yehova

Miaka minne iliyopita mmoja wa Mashahidi wa Yehova katika Florida, U.S.A., alipoteza kiasi kikubwa cha damu akizaa mtoto kwa kupasuliwa uvungu wa tumbo. Madaktari wake walihisi kwamba ilikuwa lazima watie damu mishipani ili kuokoa uhai wake. Mgonjwa alikataa kuidhinisha utumizi wa damu kwa msingi wa kanuni zake na masadikisho ya kidini. Katika usikizi wa kesi ya dharura, mahakama ya mahali hapo iliamua kwamba huyo mwanamke mgonjwa angeweza kutiwa damu mishipani dhidi ya mapenzi yake kama ilivyoonwa kuwa lazima na matabibu wenye kumhudumia. Hoja kuu ilikuwa kwamba kama kifo cha mgonjwa kingetokea, watoto wake wangekoseshwa utunzaji na ulinzi wake. Uamuzi huo uliungwa mkono na Mahakama ya Rufani ya Wilaya ya Florida. Mwishowe, kesi ikafikia Mahakama Kubwa Zaidi ya Florida. Mahakama hiyo ilifanya uamuzi wa kumuunga Shahidi mkono, ikiyaondoa yale maamuzi yaliyofanywa na mahakama mbili zilizotangulia, ingawa ilikuwa ni kwa kuchelewa mno isiwezekane kuzuia mitio-damu isiyotakwa. Mahakama kuu ya Florida ilitaarifu kwamba kuwa mzazi “hivyo tu na basi, hakunyang’anyi mtu haki ya kuishi kulingana na imani zake mwenyewe.” Hivyo, mahakama ilikubali kwa uthabiti kwamba mgonjwa ana haki ya kujiamulia litakalofanywa na mwili wake na ana uhuru wa kidini.

Lugha Inayokua

Zaidi ya watu milioni 330 husema Kihispania leo. Kufikia mwaka 2000, idadi ya wasema-Kihispania katika United States pekee itafika milioni 35. Kufikia mwaka huo Kihispania kitapita Kiingereza na kuwa lugha yenye kusemwa zaidi katika ulimwengu wa Magharibi. Ndivyo lisemavyo gazeti la Kihispania Cambio16 América. Instituto Cervantes, tengenezo la kueneza lugha ya Kihispania, liliripoti ongezeko la asilimia 70 katika idadi ya watu wenye kujifunza Kihispania katika United States kati ya 1986 na 1990, na ongezeko la asilimia 80 katika Japani. Kwa nini kuna upendezi mwingi sana katika lugha hiyo? Mkurugenzi wa Instituto Cervantes asema kwamba watu wanang’amua kwamba Kihispania kinazidi kuwa cha maana katika ulimwengu wa Magharibi. Kihispania kina faida ya ziada: Hicho husemwa katika nchi nyingi zilizo tofauti.

Wapenzi wa Pilipili Kali

Watu zaidi na zaidi wanakula pilipili kali. Wengi wasiozipenda huamini kwamba pilipili kali humaliza tu ladha za kiasili za chakula. Lakini wapenzi wa pilipili kali hudai kwamba hiyo si kweli hata kidogo. Kulingana na gazeti Reader’s Digest, kitabu cha hivi majuzi juu ya aina za pilipili chaeleza kwamba pilipili kali zina kitu fulani cha kikemikali kisicho na harufu ambayo huchanganyika na chembe za hisia katika kinywa na kuwasaidia wahisi ladha ya chakula. Watu fulani hudai kwamba pilipili kali ni nzuri pia kwa afya yako. Pilipili mbichi ina kiasi kingi cha vitamini C kuliko chungwa. Pilipili ijulikanayo kuwa kali zaidi ni habanero kutoka Yucatán, Meksiko. Imesemwa kwamba kula habaneros hukufanya uhisi kama kichwa chako kimetenganishwa na sehemu nyingine ya mwili wako. Lakini watu fulani hawawezi kukubali kuacha kuila.

Watoto Wafanya-Ngono

Uchunguzi wa hivi majuzi miongoni mwa wanafunzi wa shule ya msingi katika Connecticut, U.S.A., ulifunua kwamba asilimia 28 ya wanafunzi wa darasa la sita ni wafanya-ngono. Kadiri ya wenye kufanya ngono iliongezeka kufikia asilimia 49 miongoni mwa wanafunzi wa darasa la nane, na zaidi ya asilimia 60 miongoni mwa wanafunzi wa darasa la kumi. Wastadi fulani huamini kwamba idadi ya kadiri kubwa ya hata watoto wachanga zaidi wanafanya ngono. Ili kuzuia mimba miongoni mwa wasichana matineja mweneo wa UKIMWI, Mpasuaji Mkuu wa U.S. apendekeza kwamba “shule zapasa kugawa mipira ya kuzuia uzazi” kwa wanafunzi, kulingana na gazeti USA Weekend. Wilaya za shule zipatazo 50 katika United States zimefuata pendekezo hilo. Wilaya moja ya shule katika New Haven, Connecticut, inawatolea mipira ya kuzuia uzazi watoto walio wachanga hata kufikia umri wa miaka kumi. Wenye kupinga programu hiyo hushikilia kwamba ugawaji huo wa mipira ya kuzuia uzazi kwa watoto huwatia moyo wafanye ngono.

Vijana Wenye Tatizo la Unywaji

Katika uchunguzi mmoja uliofanywa kwa wanafunzi wapatao 14,000 wa shule ya sekondari katika Japani, asilimia 17.3 walionwa kuwa wenye tatizo la unywaji, laripoti gazeti Asahi Evening News. Miongoni mwa wavulana kadiri ya wenye kufanya hivyo ilikuwa juu zaidi, kukiwa na asilimia 24.8 wenye tabia za unywaji ambazo husababisha matatizo ya kimawazo, ya kimwili, na ya kijamii. Zaidi ya nusu ya vijana hao walio na tatizo la unywaji walisema wao hunywa kwa sababu wao huipenda ladha. Mmoja kati ya 4 alisema yeye hunywa kwa sababu ni mwenye huzuni au mpweke. “Wakati umefika wa wale washughulikao na wanafunzi hao waanze kukabiliana kwa uzito na tatizo hilo,” asema Dakt. Kenji Suzuki, aliyeendesha uchunguzi huo. “Ni lazima wanafunzi hao wafundishwe ifaavyo shuleni na nyumbani,” akaongezea. Katika Japani sheria huwakataza wenye umri ulio chini ya miaka 20 kunywa.

Mahali pa Kuzoezea Wahalifu

Wale wafikirio kwamba wafungwa walio wengi huanza wakiwa “majambazi hatari kabisa” wanajidanganya, asema mwanasheria Mbrazili Noely Manfredini D’Almeida. Badala ya hivyo, mwanamke huyo ashikilia dai la kwamba katika Brazili “mfungwa wa kawaida huwa ni mtu maskini sana tena kijana sana aliyeingilia uhalifu bila nafasi ya kujianzia maisha yake mwenyewe.” Wakosaji vijana hao hutupwa gerezani kuishi pamoja na wahalifu sugu. Kulingana na gazeti Veja, magereza hayo kwa kweli ni “mashine za kutengeneza maharamia wa sheria. Wafungwa wenye makosa madogo hugeuzwa kuwa wahalifu wataalamu.”

Majeruhi wa Ushindi

Hivi majuzi Kolombia ilisherehekea ushindi wa timu yao ya mpira wa miguu ilipostahili kuingia wanio la mpira wa miguu wa Kombe la Dunia la 1994. Mara tu baada ya ule mchezo wa ushindi ambamo timu ya taifa ya Kolombia ilishinda timu ya Arjentina kwa ‘mabao 5 kwa 0,’ Wakolombia walivama barabarani kwa nderemo za taharuki kuu. Muda si muda shangwe ikageuka kuwa msiba. Zaidi ya watu 70 waliuawa wakati wa sherehe za barabarani, kulingana na ripoti moja. Pia, karibu watu 900 walijeruhiwa kwa sababu ya aksidenti za magari, ulevi, au mapigano. Hata hivyo, ofisa mmoja alitaarifu kwamba ingawa idadi ya majeruhi ni ya kadiri kubwa kutosha, bado ni “ya kawaida tu katika hali kama hiyo.”

Kutojali Sana Afya

“Zaidi ya theluthi moja ya wafanyakazi wote wa ofisi katika Ujerumani hawaonyeshi kupendezwa na afya yao wenyewe,” laripoti Süddeutsche Zeitung. Huo ndio mkataa uliofikiwa na Claudia Pohle wa Chuo Kikuu cha Ruhr katika Bochum baada ya kuuliza wafanyakazi 343 wa ofisi wao hufanya nini kwa ajili ya afya yao ya kimwili, ya kihisia-moyo, na ya kijamii. Zaidi ya asilimia 36 ya walioshiriki walionyesha kutojali sana afya yao; chini ya asilimia 20 walionyesha upendezi wenye idili lakini wa muda mfupi katika lile elekeo la karibuni zaidi la kufanya mazoezi. Ni asilimia 20 tu waliojua jambo ambalo wahitaji kufanya ili kubaki wakiwa na afya, nao wakajiendesha kulingana na uhitaji huo.

Tatizo la Kuwa na Mafuta Mengi Mno Mwilini

“Amerika ndiyo nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu wenye mafuta mengi mwilini,” adai Dakt. Robert Kushner, mkurugenzi wa Kliniki ya Chuo Kikuu cha Chicago ya Kudhibiti Lishe na Uzito wa Mwili. “Idadi ya Waamerika wenye mafuta mengi mno mwilini walio na miaka zaidi ya 17 waliongezeka haraka kuwa asilimia 28 ya idadi ya watu katika 1990 kutoka asilimia 24 katika 1985,” laripoti The Toronto Star. Kisababishi ni nini? Utafiti mpya wadokeza kwamba kula mno, kukosa mazoezi, na hali za urithi ndizo sababu kubwa. “Watu wanazidi kuwa wazito, na hilo ni jambo la kuhangaisha sana,” asema Charlotte Schoenborn wa Kitovu cha Taifa cha Takwimu za Afya. Kuwa na mafuta mengi mno mwilini kwaweza kuanzisha msukumo mwingi wa damu, ugonjwa wa sukari, na matatizo mengine mazito ya afya. Kupata majibu si rahisi. Madaktari hudokeza badiliko katika mtindo-maisha. “Kula kidogo zaidi na ufanye mazoezi zaidi. Uzito wa mwili ukiisha kupotezwa, jambo la pekee ambalo husaidia kikweli kuuzuia usirudi ni utendaji wa kimwili,” laongezea Star.

Watoto Wenye Kutendwa Vibaya

“Jeuri dhidi ya watoto inafikia kadiri kubwa ajabu,” laripoti gazeti la Kibrazili O Estado de S. Paulo. Kwa habari ya uchokozi usio wa ngono, asilimia ya wavulana wenye kutendwa vibaya ni karibu ileile ya wasichana wenye kutendwa vibaya. Lakini sivyo ilivyo kwa habari ya kutendwa vibaya kingono. Miongoni mwa vijana watendwao jeuri ya ngono, karibu asilimia 23 ni wa kiume hali asilimia 77 ni wa kike. Wala hata watoto wadogo hawaponyoki kutendwa jeuri ya kinyumbani. Kulingana na Miriam Mesquita, profesa kwenye Chuo Kikuu cha São Paulo, “zaidi ya asilimia 30 ya watoto wa chini ya miaka 10 wenye kuuawa huuawa na washirika wa familia.” Karibu asilimia 29 ya watoto waliouawa na baba, mjomba (au ami), ndugu, au baba wa kambo walilalwa kwa nguvu kabla ya kufa. O Estado de S. Paulo laripoti kwamba katika Brazili karibu asilimia 90 ya visa vyote vya jeuri ya kinyumbani itendwayo dhidi ya watoto hupita bila kuripotiwa.

Uhalifu wa Kupangwa Kitengenezo

“Uhalifu wa kupangwa kitengenezo umepanuka kwa kadiri ya kushtusha sana hivi kwamba mfumo ulioenea kote wa matengenezo ya uhalifu uko kotekote ulimwenguni,” adai Gianni De Gennaro, mkurugenzi anayewakilisha serikali ya Kiitalia katika shughuli za kupinga utendaji mbalimbali wa Mafia. Mpanuko wa vikundi vya uhalifu kama Mafia ya Kiitalia, miungano-utatu ya Kichina, magenge ya waendesha-pikipiki ya Amerika Kaskazini, na tabaka la wahalifu wa yale yaliyokuwa mabara ya Kikomunisti hapo kwanza ni jambo la kuhangaisha sana jamii ya watu. Faida zipatikanazo kwa haramu huwawezesha wahalifu kupata vifaa vya tekinolojia bora kabisa na ustadi mwingi, ikifanya iwe vigumu kwa mawakili wa kutekeleza sheria kukabiliana na tatizo hilo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki