Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 10/8 kur. 16-18
  • Milima—Usanii Bora wa Uumbaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Milima—Usanii Bora wa Uumbaji
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kanda za Uhai Zisizo na Kifani
  • Athari Juu ya Mwanadamu
  • Je, Ni Mazingira Yaliyotishwa?
  • “Una Utukufu Kuliko Milima”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Tunahitaji Milima
    Amkeni!—2005
  • Milima Imo Hatarini
    Amkeni!—2005
  • Ni Nani Atakayeiokoa Milima?
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 10/8 kur. 16-18

Milima—Usanii Bora wa Uumbaji

MILIMA Andes, Viporomoko vya Maji, milima Himalaya, milima Rocky, milima Alp, na milima Ural—ni baadhi tu ya milima ya sayari Dunia. Ukubwa wa ajabu wa milima hii waweza kukufanya uvute pumzi kwa mshangao.

Wazia kusimama mbele ya Mlima Everest. Huu ndio kipambo cha dunia kwa kimo, meta 8,848—nguzo ya ukumbusho yenye kimo cha kilometa 8.8! Na kilele kimoja hiki ni sehemu ndogo tu ya milima Himalaya yenye uzuri wa ajabu. Kukiwa na vilele zaidi ya 70 ambavyo kila kimoja huinuka sana hadi meta 6,400, safu hii ya milima ina ukubwa ulio mara mbili za milima Alp katika Ulaya!

Kanda za Uhai Zisizo na Kifani

Milima iliyo mingi ina kanda, au mazingira, mbalimbali za uhai, sana-sana kwa sababu halijoto hushuka karibu digrii 1.8 kipimo cha Selsiasi kwa kila meta 300 za mwinuko. Hali mbalimbali za mvua, udongo, na upepo hufanya pia kila ukanda uwe bila kifani.

Kielelezo cha namna mbalimbali za mazingira hayo ni Vilele vya San Francisco katika Arizona, Marekani. Hiyo ndiyo milima yenye kimo cha juu zaidi katika jimbo hilo. Ukianza kwenye msingi wa milima hiyo kwenye Uwanda wa Juu wa Coconino na kupanda hadi kileleta cha kimojapo Vilele vya San Francisco, kwanza utaona jumuiya ya kimazingira ambayo ni kutia ndani mijusi na mikakati katika mazingira ya jangwa. Hatua kwa hatua utaingia katika kanda za uhai zenye baridi zaidi, zilizo makao ya mbuzi wa milimani na miti ya sprusi. Hatimaye utafikia mazingira ya kileleta yaliyo na ubarafu mwingi wa milimani. Katika mpando huu mmoja tu, ungeweza kukuta namna zilezile mbalimbali za uhai na mazingira ambazo ungeweza kuzipata ukisafiri barani tu karibu na usawa wa bahari kutoka Mexico hadi Kanada!

Je, umepata kuhisi burudisho la kuvuta hewa safi kabisa ya mlimani? Halijoto ya chini ya hewa ni kisababishi kimoja cha hisi hiyo. Lakini mahali ambako hakuna majiji karibu, hewa ya milimani yaweza pia kutakata zaidi na kuwa safi zaidi. Katika kila sentimeta ya mrabasawa (kyubu) ya hewa kwenye mwinuko wa meta 2,000, huenda kukawa na vijipande 2,500 tu vya vumbi, chavuo, na kadhalika. Linganisha kiasi hicho na hewa iliyo katika majiji makubwa, ambako vijipande hivyo vyaweza kufikia wingi wa 150,000 katika kiasi hichohicho cha nafasi ya hewa! Ndiyo sababu majengo ya ki-siku-hizi ya kuchunguza halianga hujengwa mara nyingi juu ya milima ambako hewa kavu iliyotakata huandaa hali safi kabisa za kuchunguza anga za juu.

Bila shaka, milima si makao ya kupendeza kwenye miinuko ya juu zaidi ambako kani ya angahewa na oksijeni hupungua, mnururisho wa jua huongezeka, na pepo za kidhoruba husababisha halijoto ishuke kasi sana. Ajabu ni kwamba, hata chini ya hali hizo, uhai fulani bado husitawi tu vyovyote vile. Kwa kielelezo, fikiria kibuibui kiitwacho saltisidi, au buibui mrukaji. Mkaaji huyu wa milimani hustarehe sana kwa kukaa katika milima Himalaya kwenye mwinuko wa meta 6,000! Haieleweki kabisa ni jinsi gani kiumbe huyo hubaki hai katika hali hizo.

Athari Juu ya Mwanadamu

Milima ina matokeo makubwa juu ya wanadamu wote. Kwa kielelezo, ebu tazama ramani ya ulimwengu. Angalia jinsi milima Pyrenee, yenye vilele vifikavyo zaidi ya meta 3,000 hutenganisha Hispania na Ufaransa na sehemu nyingineyo ya Ulaya. Vilevile utaona kwamba mipaka mingine ya kisiasa hufanywa kati ya milolongo ya milima mikubwa. Vizuizi hivyo visivyoondoleka vimezuia usafiri na biashara kati ya vikundi vya watu wa lugha na desturi tofauti. Hivyo, yaelekea kuwapo kwa milima kumerekebisha umbo na ukubwa wa nchi uishimo, lugha usemayo, na desturi za bara lako.

Pia milima ya kimo kirefu huvunja ulaini wa kuvuma kwa upepo. Hili laweza kuwa na matokeo mazito juu ya mvua, theluji, upepo, na halijoto. Hili, nalo, huathiri namna mbalimbali za chakula ulacho, namna ya mavazi uvaayo, labda hata muundo wa nyumba ukaamo.

Kwa kielelezo, milima ya Kunlun, ya Tien Shan, ya Hindu Kush, ya Himalaya, na safu nyingine za milima katika Asia ya Kati hufuliza kusonga kuanzia mashariki hadi magharibi. Matungamo haya ya milima iliyokaa kwa utulivu huzuia zile pepo baridi na kavu zenye kuvuma zikiteremka chini kutoka Siberia na huzuia zile pepo zenye ujotojoto na uchepechepe zipitazo kutoka Bahari Kuu ya Hindi. Hivyo, kaskazini mwa milima hii mna tabia-nchi iliyo tofauti kabisa na ile ya kusini, nayo huathiri maisha za mamilioni ya watu.

Je, Ni Mazingira Yaliyotishwa?

Kwa kushangaza, wanadamu wanaumbua uzuri na fahari ya milima. Linksi (mapaka-shume) na dubu waliokuwa wakizurura milima Alp walikwisha kutokomea kwa sababu ya uwindaji usiodhibitiwa. Udongo wa juu wenye thamani kubwa huoshewa mbali kutoka miinamo mingi ya milima kutokana na ufyekaji-misitu. Pia uchafuzi wa viwandani na utalii mwingi sana una matokeo mazito sana juu ya ule usawaziko wa mazingira wa majimbo fulani ya milimani ulio rahisi sana kuharibika.

Ufurahisho ni kwamba, milima ni sehemu ya kudumu ya mandhari ya ardhi. (Linganisha Mwanzo 49:26.) Yastahili kuangaliwa kwamba Biblia huifananisha na mlima serikali mpya ya ulimwengu inayokuja. Ikiijaza dunia, serikali hii iliyo kama mlima itarekebisha dosari yoyote iliyotendewa sayari hii. (Danieli 2:35, 44, 45) Hivyo sisi tuna uhakikishio wa kufurahia milele usanii huu bora wa uumbaji.

[Picha katika ukurasa wa 16, 17]

Mont Blanc, katika Ufaransa, meta 4,807

[Hisani]

M. Thonig/H. Armstrong Roberts

[Picha katika ukurasa wa 18]

Mlima Fuji, katika Japani, meta 3,776

[Credit line]

A. Tovy/H. Armstrong Roberts

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki