Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 2/22 kur. 18-19
  • Bwana Mdogo Mwenye Kuvalia Suti Nyeusi ya Mahameli

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Bwana Mdogo Mwenye Kuvalia Suti Nyeusi ya Mahameli
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Hisi Zisizo za Kawaida
  • Chakula na Malazi
  • Safarini Huko Ghana
    Amkeni!—2001
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2003
  • Ukurasa wa Pili
    Amkeni!—2001
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2006
Amkeni!—1995
g95 2/22 kur. 18-19

Bwana Mdogo Mwenye Kuvalia Suti Nyeusi ya Mahameli

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA UINGEREZA

FUKO ni wengi mno Kaskazini mwa Uingereza, lakini nilipokuwa nikitazama konde la majani ng’ambo ya lango la shamba, nilikuwa sijapata kamwe kuviona vilima vingi hivyo vya fuko. Vilingo vidogo, vilivyofukuliwa hivi karibuni vilifunika konde la majani lote. Je, wajua fuko ni mnyama wa aina gani na anaishije?

Watu wachache mno wamepata kumwona fuko, kwani muda mwingi wa maisha yake hutumia chini ya ardhi. Ni kiumbe mdogo, karibu sentimeta 14 kwa urefu. Fuko wa kiume ana uzani upunguao gramu 113. Fuko wa Uingereza ana koti la manyoya ya kijivu yaliyo meusi-meusi, yanayokaribia kuwa meusi kabisa, koti la manyoya na kwa kawaida, na hata kwa njia ya kupendwa, huitwa bwana mdogo mwenye kuvalia suti nyeusi ya mahameli.

Nywele za manyoya hazijalala, yaani, husimama wima kutoka ngozini. Kwa hiyo hata iwe ni upande upi fuko hubeta au hugeuka kuelekea akiwa ardhini, aweza kufanya hivyo kwa urahisi. Miaka iliyopita wanasa fuko waliuza ngozi kwa ajili ya utengenezaji wa nguo, lakini “huchukua ngozi nyingi za fuko ili kufanya koti moja,” mnasa fuko mmoja akasema kwa ucheshi.

Mwili wa fuko umebuniwa kihususa kwa ajili ya kazi ya kufukua chini. Miguu ya mbele imefanywa vizuri mbele sana mwilini na viganja vikiwa vimepanuka. Viganja vitano na mfupa uliojikunja huongezea fanyizo la makoleo mawili maalumu. Miguu yake ya nyuma, ionekanayo dhaifu ikilinganishwa na ile ya mbele yenye nguvu, husaidia kumsukuma fuko mbele. Ebu jaribu kumweka fuko kwenye udongo laini, naye atatokomea mchangani kwa sekunde tano! Aweza kusafiri katika mashimo yake yenye giza na unyevu, au juu ya ardhi, kwa mwendo uliokadiriwa kufikia kilometa tano kwa saa.

Hisi Zisizo za Kawaida

Fuko si mpofu kabisa, kama baadhi ya watu wafikirivyo, lakini macho yake madogo sana, yaliyofichika ndani ya manyoya, yawezekana hutoa tu mwono unaotosha kwa ajili ya kiumbe hiki kupambanua mwangaza na giza. Fuko achimbapo kupitia udongoni, nywele ndefu huvutwa kupitia macho yake ili kuyalinda. Hata hivyo, kilicho cha thamani kupita mwono wa fuko, ni ile hisi nyepesi ya kunusa na hisi yake ya kugusa.

Fuko ya Kiulaya ana maelfu ya michomoko kwenye ncha ya pua jekundu-jeupe, kila mmoja ukiwa na unywele wao ulio mnyetivu kwa mguso. Pia anazo ndevu ndefu kwenye sehemu mbalimbali kichwani na nywele nyingi zaidi zenye seli hisishi kwenye ncha ya mkia wake. Fuko hunasa mawimbi ya kani-eneo yajifanyizayo kadiri isongavyo kwenye shimo layo. Kwa njia hiyo anaweza kuvifahamu vizuizi, kama vile mawe makubwa ama hata wanyama wanyafuaji, na kuwaepa.

Fuko ni hafifu katika kusikia, lakini mfumo wake wa kusikia ni mzuri sana. Ana uwezo wa kutambua mawimbi kupitia ardhini na kuitikia kulingana nayo. Masikio ya fuko yaweza kufungwa kwa kutumia misuli ya spensa, ambayo huonekana kutumika ili kuzuia udongo usiingie kwenye vishimo vyenye uepesi wa kuumia.

Chakula na Malazi

Kwa kutazama kote kwenye konde la majani, ningeliweza kung’amua kijia cha chini ya ardhi, kipitwacho na mafuko. Kijia hicho kilipitia karibu tu na uso wa ardhi na kilikuwa kimeinuka kidogo. Pia kwa wazi kulikuwa na vilingo vipya, vilivyofanywa fuko walipochakura udongo uliofukuliwa karibuni. Huu ugeuzaji wa ardhi ni njia ya kupalilia, ukisaidia uvujaji wa udongo na kudumisha urutuba wawo.

Chakula kikuu cha fuko ni nyungunyungu, na hii ndiyo sababu ya kufukua mashimo. Nyungunyungu, wanapotembea katika udongo, huingia katika mfumo wa mapito ya fuko. Kisha fuko, katika pitapita ya njia yake katika mafukuo yenye kiza, mara hupata chakula chake. Lakini pia hula wadudu, kutia ndani jaketi-ngozi na buu-bawakavu. Ni lazima fuko ale kila muda wa saa mbili, la sivyo atakufa.

Vilingo vidogo vya fuko ardhini havipasi kukosewa na kiota cha fuko. Hicho ni kikubwa zaidi, kikiwa na kimo cha karibu sentimeta 30 na meta moja upana. Kwa kawaida hupatikana karibu na kivuli—uvunguni mwa mti au kando-kando ya tuta la majani ya viota kama vile nyasi, vitawi, na majani yapatikanapo kwa wingi.

Mapema katika msimu wa masika, fuko wengi kufikia saba huzaliwa. Watoto wa fuko huwa wapofu na bila manyoya na huwa na uzani unaopungua gramu tatu. Baada ya majuma matano huwa na umri wa kutosha kujilisha na kutembea, labda kufikia umbali wa kilometa moja na nusu. Baada ya miezi tisa watakuwa tayari kujamiiana. Muda wa kadiri wa maisha ya fuko ni miaka mitatu. Hata hivyo, wanyama wanyafuaji huwaua wengi kabla ya wakati huo.

Kukiri wazi, fuko aweza kutokeza matatizo afukuapo kwa ajili ya chakula chake chini ya udongo uliotandazwa vizuri au kwenye uwanja wa gofu, lakini bwana wetu mdogo mwenye kuvalia suti yake nyeusi ya mahameli abaki kuwa sehemu yenye kuvutia sana ya maisha ya mashambani.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki