Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 9/8 kur. 25-27
  • “Njoo Nasi Kwenye Mashamba ya Mizabibu ya Hungaria!”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Njoo Nasi Kwenye Mashamba ya Mizabibu ya Hungaria!”
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Divai Itokanayo na Zabibu Kavu?
  • Kuteremka Kuingia Vyumba vya Kuhifadhia Divai
  • Kileo Ni Nini Yaliyo Maoni ya Mkristo Juu Yacho?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
  • Zabibu Zilizoganda Zinazotokeza “Divai ya Dhahabu”
    Amkeni!—2002
  • Je, Ni Kosa Kunywa Kupita Kiasi?
    Amkeni!—2004
  • Je, Ni Vibaya Kunywa Kileo?
    Amkeni!—2006
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 9/8 kur. 25-27

“Njoo Nasi Kwenye Mashamba ya Mizabibu ya Hungaria!”

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA HUNGARIA

Milima ya Zemplén yajulikana kwa vilima vyayo vyenye umbo la pia vyenye asili ya kivolkeno. Kwenye miteremko ya milima hii hukaa eneo likuzalo divai la Hungaria, Tokaj-Hegyalja lenye kuvutia mno.

KATIKA kaskazini-mashariki mwa Hungaria, lililofichika chini ya Mlima Tokaj wenye kimo cha juu mno, lipo jiji la Tokaj. Lililoenea kutoka hapo, ambapo mito miwili yaungana, hadi kilometa 55 kaskazini-magharibi ni eneo likuzalo zabibu. Katikati kabisa mwa sehemu hii yenye rutuba, twapata kijiji kidogo kiitwacho Tolcsva, ambapo kikundi cha watunda-zabibu wanatunda kwa uangalifu zile zinazoonekana kuwa zabibu kavu kutoka vichala vya mizabibu aina ya Furmint ya Kihungaria.

Njoo, uonje divai tamu ijulikanayo sana ya Tokay Aszu ya Tokaj-Hegyalja! Hapa wakuzaji huona mazao yao yakiwa yasiyolinganika na hubandika divai zao majina ya Kilatini, kama vile Vinum Regum, Rex vinorum, yakimaanisha “Mfalme wa Divai, Divai Inayowafaa Wafalme.”

Divai Itokanayo na Zabibu Kavu?

“Je, unapanga kutengeneza divai kutokana na zabibu kavu?” twauliza kwa udadisi. Swali letu lavuta maelezo yenye idili. Hizi si zabibu kavu hasa bali ni zabibu za kipekee zilizoachwa zikunjamane kwenye mzabibu, twaelezwa. “Ni nini kinachozifanya ziwe za kipekee mno?” Kwa kushangaza twajulishwa Botrytis cinerea, ambayo ni aina ya kipekee ya ukungu inayopatikana kwenye sehemu ya juu ya zabibu katika eneo hili.a Twaelezwa kwamba kuvukiza kwa maji kutoka mitoni chini yetu hufanya mazingira yafae kwa ukungu huu wa kipekee.

Ili huo ukungu utimize kazi yao kwenye zabibu, halianga itakikanayo ni ya lazima. Wakuzaji wanahitaji majira ya kiangazi yenye siku nyingi zenye jua pamoja na mvua ya kutosha ili kuwezesha ukuzi wa mapema wa vichala vya zabibu. Kisha, zabibu zikiiva kabisa mapema mwa Septemba na vuli yenye ukavu na jua yafuata, matunda yatakuwa katika hali bora zaidi kwa ajili ya utengezaji-divai.

Lakini ukungu husaidiaje katika utengezaji-divai? Jibu ni gumu kueleweka kidogo; hata hivyo, hili ndilo tunaloelezwa. Utendanaji wa kikemikali huanzishwa wakati ganda la zabibu iliyoiva linapopasuka kwenye mzabibu, ikiruhusu ukungu kujilisha sukari ya matunda katika zabibu, hilo likifanya asidi zitokezwe.

Je, hizo asidi hufanya divai iwe na ladha ya chachu? Twahakikishiwa kwamba hiyo sukari na alkoholi huficha uchungu wa asidi maliki na asidi tatariki. Asidi nyinginezo, kama vile asidi sitriki na asidi glukoniki, ni za muhimu kwa ladha ya divai. Uasidi wa divai hutegemea muundo wa mchanga, nayo ladha ya divai pia huathiriwa na kikao cha mizabibu kuhusiana na jua.

Maelezo yaendeleapo, twapata kujua kwamba baada ya kushinikizwa, fofota kutoka zabibu zilizokauka huchanganywa na divai ya mwaka uliopita, ambayo ilitengenezwa kutokana na zabibu za kawaida. Matokeo ya uziduaji wa muda wa saa 72 na kushinikizwa kwa mwisho, ni umaji-maji mzito wenye kiwango cha juu cha sukari ambao utachachishwa kwa muda fulani katika mapipa ya mbao. Kiwango cha alkoholi kifikapo kati ya asilimia 13 na 15, uchachishaji unasimamishwa kikemikali. Mwishoni mwa miezi sita, lazima hiyo divai ichujwe na kuachwa itulie ili iive zaidi. Divai ya Aszu iliyo bora huhitaji kuanzia miaka mitatu hadi tano kabla ya kuwa tayari kutumiwa.

Kuteremka Kuingia Vyumba vya Kuhifadhia Divai

Tukiwa twarudi kijijini, twaingia jumba la kuhifadhia divai, ambapo kiolezo kimoja chavuta uangalifu wetu—jembe zee lenye uma. Kufanya kazi na kifaa hiki katika mchanga mgumu kulikuwa kwenye kuchosha sana hivi kwamba hicho kifaa kiliitwa kiua-mwanadamu.

Mfanyakazi mwenye furaha wa chumba cha kuhifadhia divai atusalimu na kwa furaha atuongoza kupitia chumba cha kuhifadhia divai cha hilo jumba la hifadhi. Kwa fahari yeye aeleza uangalifu unaotolewa ili kudumisha halijoto na unyevu utakikanao kwa mapipa ya divai. Kwa kuwa halijoto yapasa kuwa digrii 12 Sentigredi, vyumba hivyo vinachimbwa ndani ya mwamba wa chokaamawe. Unyevu wiani unadumishwa kwenye asilimia 85 hadi 90.

Mara nyingine tena twashangazwa, wakati huu twashangazwa kujua kwamba uivaji zaidi wa divai utategemea kuwapo kwa ule ukungu wa kipekee, ambao hutua juu ya karibu kila kitu katika chumba cha kuhifadhia divai—mbao, vioo, hata kuta za matofali—kila kitu isipokuwa sakafu ya saruji. Ili ukungu usisumbuliwe na hewa safi ya nje, watengeza-divai hujaribu kutembea kupitia hivyo vyumba mara chache mno wawezavyo.

Mwongozi wetu anukuu methali moja ya Kihungaria ya mtengeza-divai: “Palipo ukungu bora, pana divai bora, na palipo divai bora, pana ukungu bora.” Ili kutusadikisha ukweli wa taarifa hii, mfanyakazi wa chumba cha kuhifadhia divai aliye mkarimu atupatia aina tofauti za divai ya Tokay Aszu ili tuonje. Kwa nuru ya mshumaa, huku divai katika glasi zetu ikimetameta kwa rangi ipenyekayo nuru, yeye ataja jinsi hiyo divai huacha mstari wa kimviringo upande wa ndani wa glasi, kawaida ya divai ya Tokay Aszu.

Yeye atuambia kwamba mwonja-divai hupendelea divai chungu, kwa kuwa hiyo hutokeza utamu na harufu yenye kutofautisha ya divai, ambayo huenda isitambuliwe katika divai tamu. Inasemekana kwamba divai tamu ya Tokay Aszu ni ya kifumbo—hiyo huhitaji mtaalamu ili kuvumbua siri zayo.

Kwa kumalizia, yeye atuuliza hivi: “Je, mlijua kwamba divai ya Tokay Aszu ilifikiriwa kuwa dawa na ilikuwa ikipatikana katika kila duka la dawa?” Hili latukumbusha shauri la Paulo kwa Timotheo: “Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.” (1 Timotheo 5:23) Mwishowe, baada ya kuona kuwekwa kwa divai katika chupa na uuaji wa vijidudu vya maradhi, twarudi nyumbani tukiwazia jinsi, wakati divai itumiwapo kwa kiasi, maneno ya Zaburi 104:15 huwa ya kweli: “Na divai imfurahishe mtu moyo wake.”

[Maelezo ya Chini]

a Huo ukungu “hukoleza sukari za zabibu na kukolea kuwa utamu ulio kama wa asali,” yasema The New Encyclopædia Britannica.

[Picha katika ukurasa wa 26]

Juu: Divai huiva katika mapipa haya

Kulia: Ule ukungu wa kipekee hukua hata juu ya chupa

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki