Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 5/22 uku. 31
  • Nyuki Wangu Waliangua Vifaranga!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nyuki Wangu Waliangua Vifaranga!
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Maajabu ya Yai la Mbuni
    Amkeni!—2002
  • Wazazi Waaminifu na Wenye Ushirikiano
    Amkeni!—2009
  • Jinsi Wanyama Wanavyowalisha na Kuwatunza Watoto Wao
    Amkeni!—2005
  • Mambo Tunayojifunza Kutokana na Ndege wa Mbinguni
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 5/22 uku. 31

Nyuki Wangu Waliangua Vifaranga!

NAISHI katika shamba dogo kaskazini mwa Sweden. Hivi majuzi, wakati wawili kati ya kuku wangu walikuwa wakiatamia mayai, niliangalia matendo yao. Siku kadhaa baada ya vifaranga wa kwanza kuanguliwa, wengine walitoka kwenda kutembea-tembea, wakapitia karibu na yule kuku mwingine. Akifikiria kuwa vifaranga hao ni wake, aliamka mara moja, akaacha mayai yake, akaanza kuwakusanya chini ya mabawa yake. Vifaranga hao hawakuonekana kujali ni kuku yupi aliyewatunza.

Nilijaribu kumfanya kuku huyo arudishe vifaranga “walioibwa” na kurudia kuatamia mayai yake mwenyewe, lakini juhudi zangu ziliambulia patupu. Nilikuwa karibu kuyatupa pipani mayai yaliyoachwa nilipotua na kufikiri, ‘Huenda kungali na uhai ndani yayo!’ Ndipo nikapata wazo.

Mzinga mkubwa wa nyuki hudumisha kiwango cha joto cha digrii 34 Selsiasi katika mzinga wao. Kwa hiyo nilichukua mayai hayo na kuyaweka juu ya pamba kwenye chumba cha kuatamia ndani ya mojawapo ya mizinga yangu. Kisha nikaweka vikombe viwili vya maji karibu nayo ili kusaidia kuweka “kiota” kikiwa na unyevu. Niliyageuza mayai kila siku, kwa kufanya hivyo nikimwiga kuku mwenye kuatamia.

Baada ya siku chache, nilisikia milio ya kinda la kuku iliyo dhahiri ikitoka kwenye mayai kadhaa. Muda mfupi baadaye, kifaranga mdogo mwenye unyevu alitoka katika kaka lake! Mara moja nilimchukua na kumweka chini ya kuku aliyeyaacha mayai yake. Kwa kupendeza, alimkubali. Upesi alikuwa na makinda wadogo 12 wa kutunza wenye manyoya mororo, kwa sababu ya nyuki wenye shughuli nyingi.—Imechangwa.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

Picha zote: Foto, Roland Berggren, Västerbottens-Kuriren, Sverige

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki