Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 11/22 uku. 31
  • Walitimiza Ahadi Yao!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Walitimiza Ahadi Yao!
  • Amkeni!—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Mwanamume Aliyeamua Kumtii Mungu
    Amkeni!—2003
  • Pata Faraja na Uwafariji Wengine
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Licha ya Kuwa na Haya, Ikiwa Ningepewa Nafasi Nyingine Nisingebadili Chochote!
    Masimulizi ya Maisha ya Mashahidi wa Yehova
  • Jitihada Yake Ilileta Thawabu
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 11/22 uku. 31

Walitimiza Ahadi Yao!

ANTONIO, aliyekuwa katika mwaka wake wa mwisho katika shule ya sekondari, alitaka kuwatolea wanadarasa wenzake ushahidi wa kivivi hivi. Kwa hiyo akadokeza kwamba mwalimu wake wa somo la historia aonyeshe vidio Jehovah’s Witnesses Stand Firm Against Nazi Assault. Mwalimu alikubali ajapokuwa na shaka, huku akisema kwamba angeonyesha vidio hiyo siku iliyofuata.

“Mwanzoni,” asimulia Antonio, “mwalimu aliitazama vidio hiyo huku akijisifu; lakini alipogundua kwamba wanahistoria maarufu ndio waliosimulia historia ya Mashahidi wa Yehova katika kambi za mateso, akawa makini zaidi. Mwishowe alinishukuru kwa sababu ya kudokeza onyesho la vidio hiyo.”

Wakati wa somo lililofuata, mwalimu alijaribu kueleza kazi ya Bibelforscher, kama walivyoitwa Mashahidi wa Yehova huko Ujerumani nyakati hizo; lakini aling’amua kwamba ingelikuwa heri kumwacha Antonio aieleze. Antonio alieleza fungu la Mashahidi katika jamii na baadhi ya mafundisho yao. Alimalizia kwa kusema: “Bila shaka, watu hawawezi kunufaika na ujumbe wenye thamani tunaowaletea wasipotusikiliza, wakifunga milango yao kwa vishindo tunapowazuru, au ikiwa hawasomi vichapo vyetu.”

Wanadarasa wenzi wa Antonio walikubaliana wote na maelezo yake, na mwalimu akapendekeza azimio kwa darasa hilo. Watawasikiliza Mashahidi mara ya kwanza wakutanapo nao na kukubali vichapo vyao. Darasa liliendelea kuzungumzia vidio hiyo kwa muda fulani. Unaweza kuwazia uradhi wa Antonio siku chache baadaye alipowaona wanafunzi wenzake wakija darasani na vichapo vya Watchtower na kumsikia kila mmoja wao akisema hivi kwa tabasamu: “Waona, nilitimiza ahadi yangu!”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki