Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g01 9/8 uku. 31
  • Msichana Mdogo Mwenye Tumaini Thabiti

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Msichana Mdogo Mwenye Tumaini Thabiti
  • Amkeni!—2001
  • Habari Zinazolingana
  • Vijana Wanaomsifu Yehova Huboresha Maisha Yao
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Walijitoa Wenyewe kwa Hiari Nchini Ghana
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2016
  • Nilitoroka Mauaji na Kupata Uzima
    Amkeni!—2009
  • Tunatiwa Nguvu Ili Kushinda Vishawishi na Kutovunjika Moyo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2001
g01 9/8 uku. 31

Msichana Mdogo Mwenye Tumaini Thabiti

WACHAPISHAJI wa gazeti la Amkeni! walipokea barua kutoka kwa msichana mwenye umri wa miaka 12 anayeitwa Stephanie. Aliandika hivi: “Ninataka kuwaambia jinsi ambavyo vichapo vyenu vimenisaidia sana shuleni. Hivi majuzi tulipewa mradi wenye kichwa ‘Tamaduni Mbalimbali.’ Familia yetu ilichunguza vichapo vyenu na kukata maandishi na picha zilizofaa kichwa hicho. Kisha nikabandika maandishi na picha hizo kwenye ubao.” Mwalimu wa Stephanie aliwaagiza watoto darasani wateue miradi mitano iliyo bora sana. Stephanie anaandika hivi: “Siku iliyofuata nilijua kwamba mradi wangu ulikuwa kati ya miradi mitano bora.”

Stephanie alitoa habari kadhaa kutoka katika toleo la Amkeni! la Oktoba 22, 1998, lenye kichwa hiki kwenye jalada: “Je, Watu Wote Watapata Kupendana?” Stephanie, ambaye ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova, anaamini kabisa kwamba watu wa tamaduni mbalimbali wanaweza kuishi pamoja kwa amani. Yeye ni mshiriki wa udugu wa kimataifa, na washiriki wenzake wengine waliokuwa maadui awali—kama vile Watutsi na Wahutu, Wajerumani na Warusi, Waarmenia na Waturuki, Wajapani na Wamarekani—wameungana kwa kufuata kweli ya Biblia. Wanajaribu kumwiga Muumba wao pamoja. Kwa njia gani? Andiko moja ambalo Stephanie alitumia katika mradi wake linajibu hivi: “Mungu si mwenye ubaguzi, bali katika kila taifa mtu ambaye humhofu na kutenda uadilifu akubalika kwake.” (Matendo 10:34, 35) Mashahidi wa Yehova wanajitahidi sana kuwatendea wengine bila ubaguzi.

Stephanie anatazamia utimizo wa ahadi ya Biblia ya kwamba hivi karibuni Ufalme wa Mungu utaleta hali za uadilifu duniani. (Ufunuo 21:3, 4) Vijana wengi katika ulimwengu huu wana hofu na wasiwasi kuhusu wakati ujao, lakini Stephanie ana tumaini thabiti.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki