Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g04 10/8 uku. 27
  • “Hatutaki Kusherehekea ‘Halloween!’”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Hatutaki Kusherehekea ‘Halloween!’”
  • Amkeni!—2004
  • Habari Zinazolingana
  • Chanzo cha Halloween Ni Nini?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Ukweli Kuhusu Halloween
    Amkeni!—2013
  • Ukweli Kuhusu Sherehe Zinazopendwa
    Amkeni!—2001
  • Je, Sherehe Zinazopendwa Zinaweza Kudhuru?
    Amkeni!—2001
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2004
g04 10/8 uku. 27

“Hatutaki Kusherehekea ‘Halloween!’”

NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI UBELGIJI

Huo ndio uliokuwa uamuzi wa wanafunzi wa darasa moja katika shule fulani huko Tienen, Ubelgiji. Kwa nini walifanya uamuzi huo? Nchini Ubelgiji, ni jambo jipya kusherehekea Halloween, ambayo ni sherehe ya mkesha wa Siku ya Watakatifu Wote. Sherehe hiyo ilipaswa kusherehekewa kwa mara ya kwanza katika shule hiyo mnamo Oktoba 31, 2002. Basi kabla ya siku hiyo, mwalimu aliwapa wanafunzi mgawo kuhusu sherehe hiyo. Mwalimu huyo aliwaambia hivi: “Tayarisheni jambo baya sana na lenye kushtua kuhusu sherehe hiyo!”

Matthias, mwenye umri wa miaka kumi, alikuwa miongoni mwa wanafunzi hao. Alikumbuka kwamba pindi moja alisoma kuhusu hatari zilizofichika za Halloween katika gazeti la Amkeni! la Oktoba 8, 2001. Alitambua kwamba sherehe hiyo inahusisha mambo yasiyompendeza Mungu. Basi, Matthias akatumia habari hizo kuandika insha. Mwalimu alipoisoma kwa makini, alikata kauli kwamba sherehe hiyo ni hatari. Kisha akamwambia Matthias awaeleze wanafunzi wenzake darasani kuhusu habari hiyo.

Matthias alipoanza kuzungumzia habari hiyo, ilionekana kwamba baadhi ya wanafunzi hawakuwa wakisikiliza. Hata hivyo, alipoendelea kuzungumza, wote wakamsikiliza kwa makini. Matthias alipomaliza, mwalimu aliwauliza wanafunzi ikiwa bado wanataka kusherehekea Halloween. Wanafunzi wote wakasema: “Hatutaki!” Mwanafunzi mmoja alisema hivi kwa sauti: “Inachukiza!” Mwingine akasema: “Sikujua kwamba Halloween haiwaheshimu wafu.”

Ingawa hapo awali Matthias alikuwa mwanafunzi mwenye haya, tukio hilo lilimwimarisha sana kuendelea kushikamana na mafundisho ya Biblia anayoamini hata anapokabili mkazo. Pia, mwalimu na wanafunzi wenzake wakamheshimu zaidi kwa kuwa Shahidi wa Yehova.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki