Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 3/06 uku. 3
  • Tamaa ya Kupendwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Tamaa ya Kupendwa
  • Amkeni!—2006
  • Habari Zinazolingana
  • Dada Waliotaabika Ambao ‘Waliijenga Nyumba ya Israeli’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Ninaweza Kuzungumzaje na Wazazi Wangu?
    Majibu Ya Maswali 10 Ambayo Vijana Huuliza
  • Nizungumze Jinsi Gani na Wazazi Wangu?
    Amkeni!—2009
  • Ninaweza Kuzungumza Jinsi Gani na Wazazi Wangu?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2006
g 3/06 uku. 3

Tamaa ya Kupendwa

Hapo zamani za kale katika jiji ambalo leo ni sehemu fulani ya nchi ya Uturuki kulikuwa na msichana aliyeitwa Lea. Lea hakuwa mrembo, lakini dada yake mdogo Raheli alikuwa mrembo.

RAHELI alikutana na mwanamume aliyempenda sana hivi kwamba alikubali kumfanyia baba yake kazi kwa miaka saba ili amwoe. Hata hivyo, usiku wa harusi, baba ya wasichana hao alimwoza Lea badala ya dada yake. Hatujui Lea alihisije kuhusu njama ya baba yake, lakini lazima awe alijua kwamba hiyo haikuwa njia nzuri ya kuanza maisha ya ndoa.

Alipogundua kilichotokea, bwana harusi aliteta. Baba alimweleza kwamba ilikuwa desturi yao kumwoza kwanza msichana mkubwa. Baadaye mwanamume huyo alimwoa pia yule msichana mdogo. Hivyo, Lea alijikuta ameolewa kwa hila na mwanamume ambaye alimpenda dada yake mdogo. Lazima Lea awe alihuzunika sana kuona dada yake akipendwa zaidi! Lea hakuwa na uchumba wenye upendo naye alikuwa na kumbukumbu chache tu zenye kufurahisha kuhusu siku ya harusi yake. Lazima awe alitamani kupendwa kama Raheli! Kwa hiyo, kwa sababu ya hali ambazo hangeweza kuzuia, huenda mara nyingi Lea alijihisi kuwa hapendwi wala hatakikani.a

Kwa kiasi fulani, watu wengi leo wanaweza kuelewa hali ya Lea. Sote tunahitaji kupenda na kupendwa. Labda tunatamani kupata mwenzi atakayetupenda. Tunataka pia kupendwa na wazazi wetu, watoto wetu, ndugu na dada zetu, na marafiki. Kama vile Lea, huenda tukaona wengine wakipendwa hali sisi hatupendwi.

Tangu utotoni sisi husikia hadithi za mahaba kuhusu watu wenye kuvutia ambao hupendana na kuishi raha mustarehe. Waimbaji huimba kwa hisia nyingi kuhusu upendo; washairi husifu upendo. Hata hivyo, mtafiti mmoja aliandika hivi kuhusu upendo: “Hakuna shughuli au utendaji wowote ambao huanzishwa mtu akiwa na matumaini na matarajio makubwa kama upendo. Hata hivyo, mara nyingi sana upendo hushindwa kufaulu.” Kwa kweli, mara nyingi mahusiano yetu ya karibu ndiyo hufanya mioyo yetu ishuke na kutuhuzunisha badala ya kutuletea shangwe ya kudumu. Katika nchi kadhaa, asilimia 40 hivi ya watu wote waliofunga ndoa hutalikiana, na wenzi wengi wa ndoa ambao hawajatalikiana hawana furaha.

Katika nchi nyingi, idadi ya familia zenye matatizo na zile zenye mzazi mmoja ambapo watoto pia wameathiriwa imeongezeka. Hata hivyo, watoto hasa wanahitaji kuwa katika familia yenye kujali na yenye upendo. Hivyo basi, kwa nini watu hawapendani? Tunaweza kupata wapi habari kuhusu sifa hiyo yenye thamani? Makala zinazofuata zitajibu maswali hayo.

[Maelezo ya Chini]

a Simulizi hili linapatikana katika sura ya 29 na ya 30 ya kitabu cha Biblia cha Mwanzo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki