Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 4/06 kur. 10-11
  • “Wafungwa kwa Sababu ya Imani Yao”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Wafungwa kwa Sababu ya Imani Yao”
  • Amkeni!—2006
  • Habari Zinazolingana
  • Kuendeleza Imani Pamoja na Mume Wangu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Kutegemezwa Katika Majaribu Makali Mno
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Ushuhuda kwa Imani Yao
    Amkeni!—1996
  • Nilitegemezwa kwa Kumwamini Mungu Kabisa
    Amkeni!—2001
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2006
g 4/06 kur. 10-11

“Wafungwa kwa Sababu ya Imani Yao”

NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI POLAND

HATA leo, bado maneno Arbeit Macht Frei (Kazi Huweka Huru) huonekana kwenye malango ya chuma ya kambi ya mateso ya Auschwitz huko kusini mwa Poland, kilometa 60 hivi kutoka mpaka wa Cheki.a Hata hivyo, maneno hayo hayaonyeshi mambo yaliyowapata wengi walioingia kambini humo kati ya mwaka wa 1940 na 1945. Katika kipindi cha miaka hiyo, Wanazi waliwaua zaidi ya watu milioni moja huko Auschwitz. Hata hivyo, kuna kikundi kimoja ambacho kingeweza kuachiliwa huru wakati wowote.

Walipaswa kutimiza matakwa gani ili waachiliwe huru? Mfungwa yeyote ambaye alikuwa Shahidi wa Yehova na ambaye alitia sahihi hati iliyosema kwamba yeye si Shahidi tena angeachiliwa huru. Mashahidi wengi walifanya nini? Mwanahistoria István Deák anasema kwamba “walikuwa kama Wakristo wa karne ya kwanza ambao waliona ni afadhali waliwe na simba badala ya kumtolea maliki wa Roma dhabihu ndogo kwenye madhabahu.” Bila shaka msimamo wao unapaswa kukumbukwa, na kwa hakika umekumbukwa.

Kwa miezi miwili, kuanzia Septemba 21, 2004, kulikuwa na maonyesho kwa ajili ya Mashahidi wa Yehova peke yao ambayo yalifanywa kwenye ukumbi mkuu wa Jumba la Makumbusho la Serikali huko Auschwitz-Birkenau. Maonyesho hayo yalikuwa na kichwa kinachofaa “Wafungwa kwa Sababu ya Imani Yao—Mashahidi wa Yehova na Utawala wa Nazi.” Maonyesho hayo yalikuwa na mabango 27 ya kihistoria. Mabango hayo yalionyesha azimio thabiti la Mashahidi la kudumisha msimamo wa Kikristo wa kutokuwamo wakati wa utawala wa Nazi.

Wageni wengi waliguswa moyo na nakala ya barua ambayo Deliana Rademakers wa Uholanzi aliandika akiwa gerezani. Akiandikia familia yake, alisema: “Niliweka nadhiri ya kufanya mapenzi ya Yehova . . . . Iweni hodari na wajasiri. Yehova yuko pamoja nasi.” Mnamo 1942, Deliana alipelekwa uhamishoni Auschwitz, ambako alikufa majuma matatu hivi baadaye.

Kulikuwa na jumla ya Mashahidi 400 hivi huko Auschwitz. Watatu kati yao ambao bado wako hai walikuwako wakati wa kufunguliwa kwa maonyesho hayo. Walisimulia mambo yaliyowapata na kujibu maswali ya waandishi wa habari. Walionyesha ujasiri uleule ambao uliwawezesha kuvumilia hali katika kambi hiyo.

Katika kitabu chake, Imprisoned for Their Faith—Jehovah’s Witnesses in Auschwitz Concentration Camp, mtafiti Teresa Wontor-Cichy wa Jumba la Makumbusho la Serikali aliandika hivi: “Msimamo wa kikundi hiki kidogo ulikuwa na uvutano mzuri kwa wafungwa wengine. Azimio lao la kusimama imara siku baada ya siku liliwasadikisha wengine kwamba wanaweza kushikilia imara kanuni wanazoamini chini ya hali zozote zile.”

Ukweli ni kwamba kufungwa gerezani na kuuawa si jambo geni kwa wafuasi wa Yesu Kristo, ambaye yeye mwenyewe alikamatwa na kuuawa kwa sababu ya imani yake. (Luka 22:54; 23:32, 33) Yakobo, aliyekuwa mtume wa Yesu, aliuawa pia. Mtume Petro alifungwa gerezani, na mtume Paulo alipigwa na kufungwa gerezani mara nyingi.—Matendo 12:2, 5; 16:22-25; 2 Wakorintho 11:23.

Vivyo hivyo, Mashahidi wa Yehova huko Ulaya waliweka mfano mzuri wa imani katika Mungu miaka ya 1930 hadi ya 1940. Inapendeza kuona kwamba imani yao imetambuliwa huko Auschwitz.

[Maelezo ya Chini]

a Kambi ya Auschwitz ilikuwa na sehemu tatu—Auschwitz I (kambi kuu), Auschwitz II (Birkenau), na Auschwitz III (Monowitz). Vyumba vingi vya gesi vyenye sifa mbaya vilikuwa huko Birkenau.

[Picha katika ukurasa wa 10]

Mashahidi watatu ambao walikuwa katika kambi ya mateso ya Auschwitz wakiwa wameshika bango lenye kichwa cha maonyesho

[Picha katika ukurasa wa 11]

Deliana Rademakers, na barua aliyoandika akiwa gerezani

[Hisani]

Inset photos: Zdjȩcie: Archiwum Państwowego Muzeum Auschwitz-Birkenau

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 10]

Tower: Dziȩki uprzejmości Państwowego Muzeum Auschwitz-Birkenau

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki