Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 2/07 uku. 20
  • Vipi kuhusu viapo vya kujiepusha na ngono?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Vipi kuhusu viapo vya kujiepusha na ngono?
  • Amkeni!—2007
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Ngono ya Mdomo Ni Ngono?
    Vijana Huuliza
  • Viapo vya Ubikira Ni Nini?
    Vijana Huuliza
  • Nitawaelezaje Wengine Msimamo Wangu Kuhusu Ngono?
    Vijana Huuliza
  • Zungumza na Watoto Wako Kuhusu Ngono
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2007
g 2/07 uku. 20

Vipi kuhusu viapo vya kujiepusha na ngono?

KATIKA miaka ya karibuni, viapo vya kudumisha ubikira au kujiepusha na ngono, kama vile “Sitafanya ngono kabla ya ndoa,” vimekuwa maarufu miongoni mwa vijana. Viapo hivyo vinaonyesha miradi mizuri inayopatana na maagizo ya Biblia. (1 Wakorintho 6:18; Waefeso 5:5) Lakini, wengi wanashuku kufanikiwa kwa viapo hivyo. Kulingana na uchunguzi mmoja asilimia 60 ya vijana walivunja viapo vyao kabla ya mwaka kwisha.

Isitoshe, inahangaisha kujua kile ambacho vijana wanamaanisha wanapotumia maneno “kujiepusha na ngono” na “ubikira.” Charlene C. Gian- netti na Margaret Sagarese wanaandika hivi katika kitabu chao Boy Crazy!: “Wataalamu wanahusianisha kuongezeka kwa ngono ya kinywa na hata ngono ya mkundu, na vijana kuwa na lengo la kubaki mabikira. Wao huamini kwamba kwa kuwa hawajafanya ngono kwa njia ya asili hiyo si ngono.”

Maoni hayo yameenea sana. Baada ya kuhoji zaidi ya vijana elfu moja, mwandishi mmoja alisema hivi: “Inaonekana kwamba labda mmoja au wawili kati ya vijana mia moja ndiye aliyeona ngono ya kinywa kuwa ngono.” Aliongeza hivi: “Unahitaji kujua kuwa huenda hivyo ndivyo mtoto wako anavyofikiri.”

Wale wanaofuata viwango vya Biblia wanatambua kuwa ngono ya kinywa na ngono ya mkundu ni ngono. Sheria ya Biblia inayosema “mjiepushe na uasherati” inatia ndani namna zote za mahusiano ya ngono haramu.—1 Wathesalonike 4:3.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki