Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 7/07 uku. 30
  • Je, Ni Kweli Waliishi Miaka Mingi Hivyo?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Ni Kweli Waliishi Miaka Mingi Hivyo?
  • Amkeni!—2007
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Kweli Watu wa Nyakati za Biblia Waliishi Kwa Muda Mrefu Sana?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Tuliumbwa Tuishi Milele
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu Wote)—2019
  • Je, Maandishi ya Noa Yana Maana Kwetu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Methusela Mlimani
    Amkeni!—2004
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2007
g 7/07 uku. 30

Je, Ni Kweli Waliishi Miaka Mingi Hivyo?

Kulingana na Biblia, Adamu aliishi miaka 930, Sethi aliishi miaka 912, na Methusela miaka 969, yaani alibakisha miaka 31 tu afikishe umri wa miaka elfu moja! (Mwanzo 5:5, 8, 27) Je, miaka hiyo inalingana na miaka yetu, au je, kama wengine wanavyodokeza ilikuwa mifupi zaidi labda kama miezi?

Uthibitisho unaopatikana katika Biblia unaonyesha hiyo ilikuwa miaka halisi inayolingana na ya wakati huu. Hebu fikiria hili: Ikiwa mwaka wa zamani ungekuwa sawa na mwezi wa sasa, watu wafuatao wangezaa walipokuwa na umri mdogo sana. Kenani angezaa kabla ya kufikia umri wa miaka sita, na Mahalaleli na Enoko wakiwa na miaka mitano hivi.—Mwanzo 5:12, 15, 21.

Isitoshe watu wa kale walitofautisha kati ya siku, miezi, na miaka. (Mwanzo 1:14-16; 8:13) Kwa kweli, matukio ya wakati wa Noa yanatusaidia kukadiria urefu wa mwezi. Ukilinganisha Mwanzo 7:11, 24 na Mwanzo 8:3, 4 utaona kwamba miezi mitano ni siku 150, yaani ukihesabu tangu siku ya 17 ya mwezi wa pili hadi siku ya 17 ya mwezi wa saba. Kwa hiyo, inaonekana Noa alitumia mwezi wenye siku 30. Nayo miezi 12 ilifanyiza mwaka.—Mwanzo 8:5-13.a

Lakini iliwezekanaje watu waishi miaka 900 na zaidi? Biblia inatuambia kwamba Mungu aliwaumba wanadamu waishi milele na dhambi ya Adamu ilileta kutokamilika na kifo kwa wanadamu. (Mwanzo 2:17; 3:17-19; Waroma 5:12) Wale walioishi kabla ya Gharika hawakuwa mbali na ukamilifu kama sisi tulivyo, na hilo lilichangia urefu wa maisha yao. Kwa mfano, kulikuwa na tofauti ya vizazi saba tu kati ya Methusela na Adamu.—Luka 3:37, 38.

Hata hivyo, karibuni Yehova Mungu ataondoa ishara yoyo- te ya dhambi ya Adamu kwa wote wanaodhihirisha imani katika damu ya Mwana wake, Yesu Kristo. “Mshahara ambao dhambi hulipa ni kifo, lakini zawadi ambayo Mungu hutoa ni uzima wa milele kupitia Kristo Yesu Bwana wetu.” (Waroma 6:23) Naam, kuna wakati ambapo hata miaka 969 ya Methusela itaonekana michache sana!

[Maelezo ya Chini]

a Ona buku la 2 la Insight on the Scriptures, ukurasa wa 1214, lililochapishwa na Mashahidi wa Yehova.

[Picha katika ukurasa wa 30]

1000

Methusela

Adamu

Sethi

900

800

700

600

500

400

300

200

100

Umri wa kawaida leo

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki